Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV


Kuna mwingine nae umemsahau mungu alamlaze mahali pema. Huyo ni HASSAN NKUMBA. Nilikuwa napenda sana anavyosoma taarifa ya Habari.
 

Asante sana kaka Paschal Mayalla kwa kuutoa ukweli wenyewe. Wengine tulikuwa tunasikia juu ya suala hilo la kuzungukiana hapo hapo RTD, sasa wewe umetupa first hand information. Anyway hali hiyo ipo katika taasisi nyingi tu labda tofauti tu ni kuwa mlikuwa mnafanya kazi muda wote hadi usiku kucha.
 
Kuna wengine walipata ajali na kufariki (nafikiri gari iligongwa na treni hapo dsm miaka ya 70's) mmoja wapo alijulikana kwa jina la Ally Saheh. Kipindi hicho ilisemekana Bandarini na TBC kulikuwa na ushirikina wa kupitiliza!

Mkuu TBC haikuwepo kipindi hicho.
Acha kupotosha...
 
Pius Nyamko, alikuwa kocha wa Pamba, nilisoma na binti yake Prisca Pius Nyamko, sijui yuko wapi nw dayz


Mimi na marehemu baba yangu tulikuwa washabiki kisawasawa wa Pamba ya Mwanza TP Lindanda wanakawekamo!
Kupitia Pamba FC nilikuwa shabiki mkubwa sana wa Dominic Chilambo!!! RIP my father , RIP Dominic Chilambo , RIP Pius Nyamko (mnamjua?)
 
Mkuu TBC haikuwepo kipindi hicho.
Acha kupotosha...
Mkuu Bramo, sio wengi wanaofahamu kuwa RTD iliitwa TBC kabla haijawa RTD na sasa hilo jina la TBC ni imelirudia tuu, sio jipya, tofauti ni mwanzo ilikuwa Tanganyika, sasa Tanzania!. Kwa watu wa miaka ile, licha ya kubadilishwa jina kuitwa RTD, paper work zote ziliendelea kuwa TBC!. Tena baadhi ya stationaries mpaka mimi naondoka zilikuwa za Government of Tanganyika!.
 
Jamani mmenikumbusha mbali sana mbona kama vile ninaona maisha huko tulikotoka ndiko kuzuri?
Nitafieni na PASKAL MAYALA original na kipindi chake cha kitimoto ndani ya itv miaka hiyo yuko wapi huyu bwana?
 
Jamani mmenikumbusha mbali sana mbona kama vile ninaona maisha huko tulikotoka ndiko kuzuri?
Nitafieni na PASKAL MAYALA original na kipindi chake cha kitimoto ndani ya itv miaka hiyo yuko wapi huyu bwana?

Pascal Mayalla yupo. Tunamsubiri aje kuiongoza Kurugenzi ya Mawasiliano kwa weledi.
 
Last edited by a moderator:
Nimemkumbuka Malima Ndelema, huyu alikuwa bingwa wa kipindi cha ngoma za asili za makabila mbalimbali, sijui yu hai bado au sijui yu wapi sasa huyu mtu.

Ni watu waliokuwa wanakupa sababu na kukulazimisha kusikiliza radio tofauti kabisa na sasa!

Malima Ndelema yuko TBC Taifa anaendelea kuchapa kazi. May Day kitaifa ya mwaka huu tulikuwa naye Mbeya.Pascal Mayala amenikumbusha mengi ikiwa ni pamoja na swali tulilokuwa tukijiuliza tangu miaka ya 80
 
huyu bwana yuko wapi? Ninakumbuka enzi hizo na kipindi cha kiti moto cha itv enzi za mrema na juma duni hajji hicho kipindi kilipgwa marufuku na serekali tokea wakati huo sikumwona tena
kaka huyu aliyeleta huu uzi ndiyeCC: Pascal Mayalla
 
Last edited by a moderator:
Pascal Mayalla yupo. Tunamsubiri aje kuiongoza Kurugenzi ya Mawasiliano kwa weledi.
Mkuu Mzito Kabwela, ni kweli bado nipo, ila kiukweli hapa nilipofika, sio kuwa najidai, bali niliishaivuka hiyo stage!, yaani niko over and above hiyo posti unayoitaja!, niliacha kutumwa tangu mwaka 2002!, mimi sasa ni kuku wa kienyeji, with 10+ years ya kuchakura, I don't see my self kama naweza kufugika na kusubiri kuletewa chakula kwa kutumwa tena na yeyote no matter who s/he is!.
Pascal.
 

ina maana huyu ndie pasco mayalla ninaye mfahamu mie? He jamani
 
Deborah Mwenda,kipindi hicho nilikuwa sikosi mama na mwana
 
ina maana huyu ndie pasco mayalla ninaye mfahamu mie? He jamani
Pascal Mayalla ni jina tuu, lakini wako Pascal Mayalla wengi.
Mimi ni yule Pascal Mayalla aliyekuwa RTD, pia namfahamu Pascal Mayalla fulani alikuwa JWTZ, yupo mwingine alisoma Urusi, kuna mwingine alisoma India, kuna mmoja aliishi US pale Maryland na mpaka leo mke wake yuko kule, kuna Pascal Mayalla aliyekuwa mtangazaji wa Kitimoto, yuko yule aliyekuwa TBC akifanya program za CCM, yuko Pascal Mayalla fulani ni mshauri wa siasa wa ubalozi wa Uingereza nchini, kuna Pascal Mayalla fulani ni mwandishi wa habari wa kujitegemea, kuna Pascal Mayalla fulani alisoma sheria kwa miaka 4 pale UDSM, hadi kuna Pasco wa jf, naye nasikia pia sometimes akichanganywa na Pascal Mayalla, hivyo inategemea huyo unayemfahamu wewe ni yupi!, unaweza ukawa unamfahamu yule Pasco wa jf, ukifikiri ndiye Pascal Mayalla Mtangazaji, kumbe ni watu wawili tofauti!.
Pasco.
 

Paschal....

Habari yako mkuu wangu....

Mkuu naomba pia kujua walipo watangazaji mahiri wa RTD na STZ enzi hizo....

Rosemary Mkangara...

Nathan Rwehabura-Mara ya mwisho alikuwa Sahara comm....

Othman Matata....

Kassim Mikongoro...

Daniel Msangya....

Wilson Malosha....

Geoffrey Erneo....

Abdallah Mlawa.....

Yusuph Omar Chunda (mzee wa methali na nahau huyu)....STZ

Makame Abdallah...STZ

Nkwabi Ng'wanakilala - Alikuwa Director wa RTD huyu....Nadhani hata wewe ulikuwa chini yake....

Nikutakie siku njema mkuu....

Bala.
 

Mkuu Mayala sahihisho. Taji hayupo tena TBC. Wakat akiwa pale alikuwa ni mkuu wa idhaa ya kiingereza (TBC international) sio TBC FM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…