Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Mkuu Sherrif Arpaio, yes ndie mimi!, hapo uliponiona DTV ndio nilikuwa nimeishaachana na RTD!.Mkuu wewe ndo Yule Pascal Mayalla alikuwa mtangazaji kule DTV miaka ya 1990s?
Pascal.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu Sherrif Arpaio, yes ndie mimi!, hapo uliponiona DTV ndio nilikuwa nimeishaachana na RTD!.Mkuu wewe ndo Yule Pascal Mayalla alikuwa mtangazaji kule DTV miaka ya 1990s?
Wanabodi,
Baada ya Kifo cha Mtangazaji Nguli nchini, Uncle J. Nyaisanga, naomba kuchukua fursa hii, kufanya reflection ndogo ya Watangazaji wa RTD waliotangulia mbele ya haki. Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.
Naomba nisizungumzie kulitowatoa duniani, wala hatima ya familia zao walizoziacha huku nyuma maana sio tuu nitazidi kuogopa, bali pia tutazidi kuumia!. Just imagine, kijitaasisi kidogo kama RTD chenye ofisi yake pale BH-Pugu Road kupoteza idadi kubwa hivi ya watumishi wake (tena hawa ninaowataja ni Watangazaji tuu!, achilia watumishi wengine!. Sii bure!, ila lazima tukubali ni kazi ya Mungu, na kazi ya Mungu haina makosa!.
Hii list sio walikufa lini ni random, nikiwakumbuka wengine nitawaongeza!
Tukianzia na
- David Wakati
- Abdul Masudi (Jawewa)
- Eli Mbotto
- Stephen Mlatie
- Siwatu Luanda
- Salama Mfamao
- Salim Seif Nkamba (Mjomba)
- Michael Katembo
- Nelly Kidella
- Halima Mchuka,
- Omar Jongo
- Tumboi Tamimu Risasi
- Mohamed Ng'ombo
- Abisai Stephen (Uronu)
- Stephen Lymo.
- Nadhir Mayoka
- Juma Ngodae
- Rukia Machumu
- Karim Besta
- Henrick Michael Libuda
- Idrissa Sadalah
- Bati Kombwa
- Iddi Rashid Mchatta
- Dominic Chilambo
Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.
Pia sio vibaya kuwaulizia wale watangazaji wa siku nyingi ambao hatujui walipo, ili kama nao wametangulia tuyaingize majina yao.
RIP All the Fallen Heroes wa Tasnia ya Utangazaji Tanzania!,
Pascal.
-Ezekiel Malongo
-Mswima Elnest
Mkuu kwelitupu, kiukweli ukweli ni kitu kigumu, ila mimi ni mkweli!. Nilipojiunga, nilielezwa kuhusu uchawi!, bahati mbaya siamini kuwa uchawi upo!. Kiukweli uchawi upo, ila ni kwa wanaoamini tuu kuwa uchawi upo!, kwa sisi tusioamini, kwetu uchawi haupo!.
Wala siamini sababu ya vifo ni uchawi, ila pia naomba kuutoa ukweli mchungu kuhusu RTD ya enzi hizo!.
Ulikuwa unajua saa tuu ya kuingia kazini, ya kutoka huijui!. Mimi nakumbuka siku nikiingia asubuhi, unafuatwa saa 9 usiku, unapaswa kutoka saa 6 mchana, ila ukitoka ndipo ueanze kuandaa vipindi vyako!, kunawakati unaingia saa 9 usiku, unatoka saa 6 usiku siku inayofuata!.
Tulipoanza kazi Mjomba (SS Mkamba), akatuhusia mkitaka salama hapa, hawa akinadada waangalieni tuu!, msiwasogelee kwa sababu macho yote yako kwao!. Mimi na Abou tukamhakikishia Mjomba kuwa hilo kweli haliwezekani, kwa sababu, hao "wadada" wenyewe tuliwaona wachovu tuu!.
Baada ya kupita miezi 6, kumbe watu mnaokuwa nao kila siku, mara wa kwanza kuanza "kuona" ni Abou!, tukasema kumbe ful;ani ni mzuri hivi!, huku na kule, "akafika mahali!", kufumba kufumbua, Abou kahamidshiwa Nachingwea!.
Huko hata hoteli kuku ni mpaka ulipie kabla ndipo upikiwe!.
Ikaja zamu yangu!, ilikuwa ni balaa!, Mwanzoni tulianzia vile vi gesti Buguruni!, mambo yalipokolea, gesti mbali!, ni kila mahali, kuanzia "washroom!', studio!, juu ya meza ya ofisi!, kwenye ngazi!, hadi Telefon room!.
Mwanzo mwanzo tulitumia!, tulipozoeana, hatukukumbuka tena!. Wengi wa watumishi wa RTD wenye watoto, baba zao wako hapo hapo!. Kuna wengine wetu tumesurvive kwa kudra tuu ya Mwenyeezi Mungu!, tatizo kubwa la watangazaji wa zamani ni kuponzwa na umaarufu!, kujifungia studio kwa masaa mengi na watu wale wale hadi kujikuta kwenye Zero Grazing!, Ukisikia mtangazaji wa kike kaolewa, ujue aliyependa ni huyo mtangazaji wa kike!, yaani ili uoe mtangazaji, lazima kwanza mtangazaji huyo ndio akupende wewe!, vinginevyo! ukipenda wewe! jua.. ( japo nakiri sio wote).
Hii "zero graizing!" could be the main cause!.
Ila pia naomba kuwahakikishieni, pamoja na yote hayo, chanzo cha vifo sio UKIMWI!, kwa sababu Ukimwi ni "ukosefu tuu wa kinga mwilini!, yaani mtu hawezi kufa kwa "ukimwi" kwa kasabu ukimwi sio ugonjwa!, ila ukishakosa hiyo kinga mwilini, mwili wako unakuwa dhaifu na kuwa rahisi kushikwa na ugonjwa ambao ndio hupelekea kifo!.
Pasco.
Kuna wengine walipata ajali na kufariki (nafikiri gari iligongwa na treni hapo dsm miaka ya 70's) mmoja wapo alijulikana kwa jina la Ally Saheh. Kipindi hicho ilisemekana Bandarini na TBC kulikuwa na ushirikina wa kupitiliza!
Kama nimepotosha sema ukweli. Ilikuwa inaitwaje ili na wengine wafahamu basi! Hapa ni sehemu ya kuelimishana pia.Mkuu TBC haikuwepo kipindi hicho.
Acha kupotosha...
Mimi na marehemu baba yangu tulikuwa washabiki kisawasawa wa Pamba ya Mwanza TP Lindanda wanakawekamo!
Kupitia Pamba FC nilikuwa shabiki mkubwa sana wa Dominic Chilambo!!! RIP my father , RIP Dominic Chilambo , RIP Pius Nyamko (mnamjua?)
Mkuu Bramo, sio wengi wanaofahamu kuwa RTD iliitwa TBC kabla haijawa RTD na sasa hilo jina la TBC ni imelirudia tuu, sio jipya, tofauti ni mwanzo ilikuwa Tanganyika, sasa Tanzania!. Kwa watu wa miaka ile, licha ya kubadilishwa jina kuitwa RTD, paper work zote ziliendelea kuwa TBC!. Tena baadhi ya stationaries mpaka mimi naondoka zilikuwa za Government of Tanganyika!.Mkuu TBC haikuwepo kipindi hicho.
Acha kupotosha...
Jamani mmenikumbusha mbali sana mbona kama vile ninaona maisha huko tulikotoka ndiko kuzuri?
Nitafieni na PASKAL MAYALA original na kipindi chake cha kitimoto ndani ya itv miaka hiyo yuko wapi huyu bwana?
Nimemkumbuka Malima Ndelema, huyu alikuwa bingwa wa kipindi cha ngoma za asili za makabila mbalimbali, sijui yu hai bado au sijui yu wapi sasa huyu mtu.
Ni watu waliokuwa wanakupa sababu na kukulazimisha kusikiliza radio tofauti kabisa na sasa!
Pascal Mayalla yupo. Tunamsubiri aje kuiongoza Kurugenzi ya Mawasiliano kwa weledi.
kaka huyu aliyeleta huu uzi ndiyeCC: Pascal Mayallahuyu bwana yuko wapi? Ninakumbuka enzi hizo na kipindi cha kiti moto cha itv enzi za mrema na juma duni hajji hicho kipindi kilipgwa marufuku na serekali tokea wakati huo sikumwona tena
Mkuu Mzito Kabwela, ni kweli bado nipo, ila kiukweli hapa nilipofika, sio kuwa najidai, bali niliishaivuka hiyo stage!, yaani niko over and above hiyo posti unayoitaja!, niliacha kutumwa tangu mwaka 2002!, mimi sasa ni kuku wa kienyeji, with 10+ years ya kuchakura, I don't see my self kama naweza kufugika na kusubiri kuletewa chakula kwa kutumwa tena na yeyote no matter who s/he is!.Pascal Mayalla yupo. Tunamsubiri aje kuiongoza Kurugenzi ya Mawasiliano kwa weledi.
Mkuu Mzito Kabwela, ni kweli bado nipo, ila kiukweli hapa nilipofika, sio kuwa najidai, bali niliishaivuka hiyo stage!, yaani niko over and above hiyo posti unayoitaja!, niliacha kutumwa tangu mwaka 2002!, mimi sasa ni kuku wa kienyeji, with 10+ years ya kuchakura, I don't see my self kama naweza kufugika na kusubiri kuletewa chakula kwa kutumwa tena na yeyote no matter who s/he is!.
Pascal.
Pascal Mayalla ni jina tuu, lakini wako Pascal Mayalla wengi.ina maana huyu ndie pasco mayalla ninaye mfahamu mie? He jamani
Mkuu Mzito Kabwela, ni kweli bado nipo, ila kiukweli hapa nilipofika, sio kuwa najidai, bali niliishaivuka hiyo stage!, yaani niko over and above hiyo posti unayoitaja!, niliacha kutumwa tangu mwaka 2002!, mimi sasa ni kuku wa kienyeji, with 10+ years ya kuchakura, I don't see my self kama naweza kufugika na kusubiri kuletewa chakula kwa kutumwa tena na yeyote no matter who s/he is!.
Pascal.
Hiki ni kikosi cha first 11 ya Radio One.
Waliokaa kutoka Kushoto ni Charles Hilary kwa sasa yuko BBC-London
Mikidadi Mahamod (Brother) sasa ni Mkurugenzi wa Radio Uhuru, Mzungu Mike Ross, na Uncle J. Nyaisangah.
Waliosimama toka kushoto, Deo Mshigeni yuko US, Monica Mfumia yuko UK, Florah Nducha ni Mkuu wa UN Radio New York, Vicky Msina, ni PRO wa BOT, Aboubakar Liongo yuko DW-Radio ya Ujerumani, Lilian Mbaga sasa ni Mkurugenzi wa TGNP, Sunday Shomari yuko VOA na Taji Liundi sasa ni Meneja wa PRT ya TBC.