Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Mkuu Makah, asante sana kwa hii historia adimu sana na sijui kama imeandikwa popote!.

Amini usiamini licha ya kufanya kazi RTD na kusikia kisa cha vifo vya watangazaji waliogongwa na treni, sikuwahi kuyafahamu majina yao ndio leo nimeyasikia, thanks.

Hata Mama Debora Mwenda sikuwahi kuijua maiden name yake ya Chihota wala her Zimbabwean connection, sasa nimejumlisha moja na moja cha kisa ya yule binti yake bingwa wa keki za harusi kupenda kuolewa na mwanamume wa Zimbabwe tuu!.

Kiukweli hatuna kabisa historia ya utangazaji Tanzania, huyo Khadija Said ndio namsikia kwako!.

Pascal.
 

Suleiman Hega atakuwa anamkumbuka - kama una mawasiliano naye nina imani atakuwa anamkumbuka Khadija. hata kuna kipindi miaka 10 ya Uhuru watangazaji wastaafu walikaribishwa kutangaza nilimsikia huyu mama
 

halima mchuka alikua ananivutia sana akitangaza soka jamani,we missed her alot r.i.p mama.
 
Suleiman Hega atakuwa anamkumbuka - kama una mawasiliano naye nina imani atakuwa anamkumbuka Khadija. hata kuna kipindi miaka 10 ya Uhuru watangazaji wastaafu walikaribishwa kutangaza nilimsikia huyu mama
Tumeingia RTD Hegga ameishaondolewa kisa ni lile sakata la Bakwata na Balukta!.
 
Umenikumbusha mbali sana mkuu mayalla!! Nimependa pia ulivyotoa ukweli wako wa moyoni juu ya utata wa vifo vilivyokuwa vikitawala Rtd .
Mungu akulinde na ujasiri wako!!!
 
Umenikumbusha mbali sana mkuu mayalla!! Nimependa pia ulivyotoa ukweli wako wa moyoni juu ya utata wa vifo vilivyokuwa vikitawala Rtd .
Mungu akulinde na ujasiri wako!!!
Sio ujasiri tu na bahati pia..c umeona kuna sehemu kasema kuna siku zingine walikua hawatumii k.i.nga wanaburura tu...nikumshukuru mungu tu.
 
Kweli aise, mtangazaji alikuwa hawezi kuanza kipindi hadi amtambulishe fundi mitambo na anapomaliza kipindi lzm amshukuru.... wapi Lando Mabula

...Ni Orlando Mabula, kama sikosei. Hiyo lando ni kama nickname wanayomuita wenzake wakiwa Mzigoni.
 
Ila kuna mtangazaji pia alikuwa akitangaza KBC pale Kenya akiitwa Leonard Mambombotela, nilimuhusudu sana huyo mzee. Hiyo nakumbuka ni miaka ya 1987.

...Leonard Mambo Mbotela. Kipindi chake mashuhuri kilichovuma Afrika Mashariki ni 'Je Huu ni Uungwana?'

Bado anadunda. Tafuta Video ya Erick Wainaina wa Kenya ya 'Nchi ya Kitu Kidogo' utamuona ile sehemu Erick anapoimba 'Nauliza na Mbotela...' ndio yule!
 

Izengo Bujaga Kadagho!Alitangaza kwa ufasaha sana vita vya USA na Iraq mwaka 1992!

Kuna kabuli juzi nimeliona pale Chang'ombe kwa jina hili;alifariki dunia nguli huyu?
 

Ahmed Jongo::::::"Abeid Mziba yupo chini kashika kichwa;Nahisi kapigwa kwenye medulla Oblangata"

Watangazaji wetu siku hizi hata mm nawashinda!Hawa wa zamani walikuwa mafundi mno hadi leo kuwasikiliza kwenye Radio

Taarifa ya Habari asome Jacob Tesha lzm usimame kwenye dirisha la Baba nijue kuna nn!Home tuliamini Tesha anasoma kama kuna breaking news tu
 
Kweli aise, mtangazaji alikuwa hawezi kuanza kipindi hadi amtambulishe fundi mitambo na anapomaliza kipindi lzm amshukuru.... wapi Lando Mabula

Hapo lzm uwataje wazee wa OB Van Noel Namaloe na Fred Kwilasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…