Mkuu Makah, Asante. Hawa kina Chihota hawa, Je walikuwa na Undugu wowote na Yule Norman Chihota ambaye katika kipindi hicho alikuwa akitamba sana kwenye Riadha hasa kwenye mbio za Mita 400 akiiwakilisha TZ kwenye michuano mingi ya kimataifa ya riadha??
Sarah Dumba, sijui yuko wapi?
Nimemkumbuka Malima Ndelema, huyu alikuwa bingwa wa kipindi cha ngoma za asili za makabila mbalimbali, sijui yu hai bado au sijui yu wapi sasa huyu mtu.
Ni watu waliokuwa wanakupa sababu na kukulazimisha kusikiliza radio tofauti kabisa na sasa!
Na huyu aliekuwa mtangazaji wa kipindi cha michezo EZEKIEL MARONGO YUKO WAPI?
Acha uongo Kipindi Cha chaguo la msikilizaji kilikuwepo tena kama sikosei saa nane mchana siku ya jumamosi
Kweli aise, mtangazaji alikuwa hawezi kuanza kipindi hadi amtambulishe fundi mitambo na anapomaliza kipindi lzm amshukuru.... wapi Lando Mabula
Lando mabula anapatikana kigamboni, Kilevi (pombe) imemuharibu!
Acha uongo Kipindi Cha chaguo la msikilizaji kilikuwepo tena kama sikosei saa nane mchana siku ya jumamosi
...Ram, nawe Utaonekana ni wa Juzi Juzi tu! Kwa kipindi kirefu wakati Watangazaji hawa Nguli wakitamba hewani taarifa ya Habari ilikuwa ni Saa MOJA Asubuhi, Saa SABA Mchana, Saa MBILI Usiku, Saa NNE Usiku Sauti ya Mapinduzi ZBar na Saa TANO Usiku Taarifa ya Habari ya Masaa 24 kisha baada ya hapo kama ni Alhamisi kinafuata kipindi cha MISAKATOO! ambacho kilikuwa maalumu kwa ajili ya nyimbo mpya za bendi iliyokuwa imeenda kurekodi nyimbo zake mpya RTD siku chache kabla!
Sio Chaguo la msikilizaji, bali kilikuwa kinaitwa Ombi lako, na pia hakikuwa siku zote, siku zingine tulikuwa tunatupiwa mashairi (Malenga wetu),
CC: jazba
mmemsahau Khalid Ponera/ zilipendwaWanabodi,
Baada ya Kifo cha Mtangazaji Nguli nchini, Uncle J. Nyaisanga, naomba kuchukua fursa hii, kufanya reflection ndogo ya Watangazaji wa RTD waliotangulia mbele ya haki. Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.
Naomba nisizungumzie kulitowatoa duniani, wala hatima ya familia zao walizoziacha huku nyuma maana sio tuu nitazidi kuogopa, bali pia tutazidi kuumia!. Just imagine, kijitaasisi kidogo kama RTD chenye ofisi yake pale BH-Pugu Road kupoteza idadi kubwa hivi ya watumishi wake (tena hawa ninaowataja ni Watangazaji tuu!, achilia watumishi wengine!. Sii bure!, ila lazima tukubali ni kazi ya Mungu, na kazi ya Mungu haina makosa!.
Hii list sio walikufa lini ni random, nikiwakumbuka wengine nitawaongeza!
Tukianzia na
- David Wakati
- Abdul Masudi (Jawewa)
- Eli Mbotto
- Stephen Mlatie
- Siwatu Luanda
- Salama Mfamao
- Salim Seif Nkamba (Mjomba)
- Michael Katembo
- Nelly Kidella
- Halima Mchuka,
- Omar Jongo
- Tumboi Tamimu Risasi
- Mohamed Ng'ombo
- Abisai Stephen (Uronu)
- Stephen Lymo.
- Nadhir Mayoka
- Juma Ngodae
- Rukia Machumu
- Karim Besta
- Henrick Michael Libuda
- Idrissa Sadalah
- Bati Kombwa
- Iddi Rashid Mchatta
- Dominic Chilambo
- Hassan Mkumba
- Khadija Said
- Ally Saleh
- Kwegier Munthali
- Leonard Mtawa
Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.
Pia sio vibaya kuwaulizia wale watangazaji wa siku nyingi ambao hatujui walipo, ili kama nao wametangulia tuyaingize majina yao.
RIP All the Fallen Heroes wa Tasnia ya Utangazaji Tanzania!,
Pascal.
Mkuu Ponera, natanguliza pole maana majina yanafanana, sikujua kuwa hata Khalid Ponera katangalia!, ilikuwa lini?!. Nakumbuka wakati wa RTD alikuwa akiishi Ilala Flat na mkewe mmoja akifanya kazi Tea Bleanders!.mmemsahau Khalid Ponera/ zilipendwa
Ogah, lengo ni kuwakumbuka waliotangulia mbele ya haki!. Hao wote uliowataja wapo labda kama lengo ni kuulizia wako wapi, nitakusaidia kidogo.Salim Mbonde
...kuna dada (sasa hivi atakuwa ni Mmama) alikuwa anatangaza sana External Service of RTD
Mohamed/Omar Jongo? (nafikiri akina Jongo walikuwepo wawili)...au ni Ahmed Kipozi?
Abdul Ngalawa/Ngarawa
Mikidadi Mahmood
Mohamed Akhnan
wa juzi juzi Charles Hillary, Betty Chalamila (Mkwasa), Sued Mwinyi na Aboubakary Liongo
pascal, hawa nao huwakumbuki? Dastan Tido Mhando, Chama omari Matata, Godfrey Mngodo, Teckla Gumbo, (Salim?- Mume wa Zamzam Maalim),Ahmed Kipozi, Julius Nyaisanga, Sango Kipozi, Abdul Omar Masudi, Mshindo Mkeyenge etcWanabodi,
Baada ya Kifo cha Mtangazaji Nguli nchini, Uncle J. Nyaisanga, naomba kuchukua fursa hii, kufanya reflection ndogo ya Watangazaji wa RTD waliotangulia mbele ya haki. Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.
Naomba nisizungumzie kulitowatoa duniani, wala hatima ya familia zao walizoziacha huku nyuma maana sio tuu nitazidi kuogopa, bali pia tutazidi kuumia!. Just imagine, kijitaasisi kidogo kama RTD chenye ofisi yake pale BH-Pugu Road kupoteza idadi kubwa hivi ya watumishi wake (tena hawa ninaowataja ni Watangazaji tuu!, achilia watumishi wengine!. Sii bure!, ila lazima tukubali ni kazi ya Mungu, na kazi ya Mungu haina makosa!.
Hii list sio walikufa lini ni random, nikiwakumbuka wengine nitawaongeza!
Tukianzia na
- David Wakati
- Abdul Masudi (Jawewa)
- Eli Mbotto
- Stephen Mlatie
- Siwatu Luanda
- Salama Mfamao
- Salim Seif Nkamba (Mjomba)
- Michael Katembo
- Nelly Kidella
- Halima Mchuka,
- Omar Jongo
- Tumboi Tamimu Risasi
- Mohamed Ng'ombo
- Abisai Stephen (Uronu)
- Stephen Lymo.
- Nadhir Mayoka
- Juma Ngodae
- Rukia Machumu
- Karim Besta
- Henrick Michael Libuda
- Idrissa Sadalah
- Bati Kombwa
- Iddi Rashid Mchatta
- Dominic Chilambo
- Hassan Mkumba
- Khadija Said
- Ally Saleh
- Kwegier Munthali
- Leonard Mtawa
- Khalid Ponera
Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.
Pia sio vibaya kuwaulizia wale watangazaji wa siku nyingi ambao hatujui walipo, ili kama nao wametangulia tuyaingize majina yao.
RIP All the Fallen Heroes wa Tasnia ya Utangazaji Tanzania!,
Pascal.
Ogah, lengo ni kuwakumbuka waliotangulia mbele ya haki!. Hao wote uliowataja wapo labda kama lengo ni kuulizia wako wapi, nitakusaidia kidogo.
Salim Mbonde -amestaafu juzi juzi
...kuna dada (sasa hivi atakuwa ni Mmama) alikuwa anatangaza sana External Service of RTD -Hanna Mayige sasa ni Mwakilishi wa Mkurugenzi kituo cha Songea.
Mohamed/Omar Jongo? (nafikiri akina Jongo walikuwepo wawili) uko right kina Jongo wako wawili, Ahmad Jongo amestaafu na Omar Jongo (RIP)
Ahmed Kipozi ni DC-Bagamoyo
Abdul Ngarawa -ni msataafu.
Mikidadi Mahmood-Ni Mkurugenzi wa Radio Uhuru
Mohamed Akhnan simkumbuki labda ulimaanisha Mohamed Dahman yuko Sauti ya Ujerumani.
Charles Hillary yuko BBC
Betty Chalamila (Mkwasa) ni DC Bahi
Sued Mwinyi bado yuko TBC Kipindi cha Majira
Aboubakary Liongo alikuwa Ujerumani amerudi bongo.
Pascal.
sawa nashukuru....lakini ninayemzungunzia mimi...inawezekana alishastaafu kwa sasa...nafikir alishawahi kuwa Mkurugenzi kipindi fulani.....jina bado limenitoka.....
Sanga?