Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

pascal, hawa nao huwakumbuki? Dastan Tido Mhando, Chama omari Matata, Godfrey Mngodo, Teckla Gumbo, (Salim?- Mume wa Zamzam Maalim),Ahmed Kipozi, Julius Nyaisanga, Sango Kipozi, Abdul Omar Masudi, Mshindo Mkeyenge etc

Ahmed Kipozi na Sango Kipozi are they couples?

Esha Mihidimi Nilimsikia Wakati Tbc Inaanza Nikajua Ni Mtangazaji Wa Juz Juzi, Akatangaza Siku Kadhaa, Nilipenda Saaaaana.............. Si Akaondoka Ghafla, Yaani Hata Sijui Yuko Wapi?
 
Esha Mihidimi Nilimsikia Wakati Tbc Inaanza Nikajua Ni Mtangazaji Wa Juz Juzi, Akatangaza Siku Kadhaa, Nilipenda Saaaaana.............. Si Akaondoka Ghafla, Yaani Hata Sijui Yuko Wapi?

Eshe Muhidini mke wa Maulid Kitenge? Hayupo tena TBC?
 
Namkumbuka Mtangazaji Wetu Ihinga Pita Makolongo, Tulimpagawisha Na Ulanzi Wa Kule, Alitangaza Kifo Cha Jambazi Muvemba. Nyakati Zenye Uchungu Mwingi, Naumia Mnapo Nipa Raha Za Enzi Hizo
 
Hiki ni kikosi cha first 11 ya Radio One.
Waliokaa kutoka Kushoto ni Charles Hilary kwa sasa yuko BBC-London
Mikidadi Mahamod (Brother) sasa ni Mkurugenzi wa Radio Uhuru, Mzungu Mike Ross, na Uncle J. Nyaisangah.

Waliosimama toka kushoto, Deo Mshigeni yuko US, Monica Mfumia yuko UK, Florah Nducha ni Mkuu wa UN Radio New York, Vicky Msina, ni PRO wa BOT, Aboubakar Liongo yuko DW-Radio ya Ujerumani, Lilian Mbaga sasa ni Mkurugenzi wa TGNP, Sunday Shomari yuko VOA na Taji Liundi sasa ni Meneja wa PRT ya TBC.

Jamani yuko wapi mtangazaji huyu Sekione Kitojo
 
Kuna wakati alikuwa Tume ya Uchaguzi ya Kiravu, sasa hasikiki tena , labda amekua freelance ? Pengine Pasco aje kutusaidia
Ni media manager wa Mlimani Media na mkufunzi wa utangazaji wa IJMC.
Pascal.
 
Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Shule ya Mawasiliano ya Umma, zamani ikiitwa DSJ
Ni TSJ na sio DSJ!. Ndicho tulichosoma sisi, kilikuwa Ilala Shariff Shamba ndani ya campus ya BASATA, kilipohamishiwa UDSM, eneo liule ndipo kikaanzishwa DSJ.
Pascal.
 
Mkuu Bramo hajapotosha.
Marehemu Ally Saleh ni cousin wangu.
Alifariki wakitoka kazini na gari ya TBC kwa kugongwa na treni kwenye crossing ya Ilala Shaurimoyo.
Walikuwa watatu:-
Ally Saleh, Kwege Munthali na mwingine jina limenitoka.

Mkuu kipindi hiko ilikuwa ni RTD, TBC inatoka wapi tena Mkuu.

cc Pascal Mayalla
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Bramo hajapotosha.
Marehemu Ally Saleh ni cousin wangu.
Alifariki wakitoka kazini na gari ya TBC kwa kugongwa na treni kwenye crossing ya Ilala Shaurimoyo.
Walikuwa watatu:-Ally Saleh, Kwege Munthali na mwingine jina limenitoka.
Matembele, asante kunikumbusha hiki kisa na majina na majina ya watangazaji hawa, by the time tunajoin RTD, kiliishatokea zamani kikihusishwa na ushirikina!.

Details haziko very clear ni walikuwa wanatoka shift au wanaingia shift ila gari ni landrover 110, ilikuwa na watu 8, watangazaji 4, fundi mitambo 3 na dereva, walipofika rail crossing gari ikazimika katikati ya reli, treni inakuja huku ikipiga honi, dereva na mtu wa mbele walifungua milangoi wakashuka, na wale watu watatu wawili nyuma pia wakashuka, walibaki watangazaji wanne waliokuwa wamekaa siti ya kati!, wote wanne walifia papo hapo!. Majina mawili ndio hayo, bado wawili wengine. Naomba yeyote mwenye details kuhusu ajali hii, atakumbushe vizuri, ila majina nimeta update kule mwanzao!.
Pascal.
 
Mkuu kipindi hiko ilikuwa ni RTD, TBC inatoka wapi tena Mkuu.

cc Pascal Mayalla

Wakati na baada ya uhuru ilkuwa inaitwa
Tanganyika Broadcasting Corporation (TBC).
Ikajaitwa Radio Tanzania Dar (RTD)
Baadae ikarudi kuitwa TANZANIA Broadcasting Corporation.
Mie sio wa dot.com... Nimeyaona yote hayo kwa macho yangu.
 
Last edited by a moderator:
Matembele, asante kunikumbusha hiki kisa na majina na majina ya watangazaji hawa, by the time tunajoin RTD, kiliishatokea zamani kikihusishwa na ushirikina!.

Details haziko very clear ni walikuwa wanatoka shift au wanaingia shift ila gari ni landrover 110, ilikuwa na watu 8, watangazaji 4, fundi mitambo 3 na dereva, walipofika rail crossing gari ikazimika katikati ya reli, treni inakuja huku ikipiga honi, dereva na mtu wa mbele walifungua milangoi wakashuka, na wale watu watatu wawili nyuma pia wakashuka, walibaki watangazaji wanne waliokuwa wamekaa siti ya kati!, wote wanne walifia papo hapo!. Majina mawili ndio hayo, bado wawili wengine. Naomba yeyote mwenye details kuhusu ajali hii, atakumbushe vizuri, ila majina nimeta update kule mwanzao!.
Pascal.

Asante Pascal.
Nitajaribu kumuuliza dadake marehemu Ally Saleh kama ana kumbukumbu ya wengine.
Ajali ni kama ulivyoieleza. Landrover ni early model nadhani 108.
Mw. Mungu awaweke pema peponi.
 
Kipindi hiko kulikuwa na vipindi vinavyogusa jamii jamani,watoto walivutwa na mama na mwana,kuna kipindi cha wakati wa kazi,kipindi cha salamu za wagonjwa yaani hadi raha ,mungu awaweke mahali pema watangazaji waliotangulia mbela za haki,wakati nikiwa nafanya kazi Abood media mkoani Morogoro nikiwa na miezi mitatu pale radio na Abood Tv ndipo karim besta akafariki dunia,mungu awaweke mahali pema peponi ,
 
Nakumbuka.
Marehemu Abdul Baker ......
na kile kipindi chake cha Mazungumzo Baada Ya Habari. Ilkuwa unaweza kukosa Taarifa ya Habari, lakini ni lazima uwahi saa mbili na robo usiku hiki kipindi.
 
Duh mmenikumbusha mbali sana.nilikuwa nakipenda sana tena sana kipindi cha mama na mwana.sikumbuki jina la mtangazaji ebu nikumbusheni wajf.nilikuwa sikosi kipindi .yaani nakosa raha nisipokisikiliza .hivi yupo yule mtanganzaji?? Pia kile kipindi cha zilipendwa kila jumapili nilikipenda sana
kama sikosei yule mama alikuwa anaitwa deborah mwenda,yaani acha bwana zile ndio zilikuwa enzi za utangazaji,kwa tuliokuwa watoto kipindi kile kukosa kipindi cha mama na mwana ilikuwa kosa kubwa!
 
Back
Top Bottom