Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Nimemkumbuka Hassan Mgumba kama sijakosea jina na kipindi chake cha matukio ya wiki
enzi hizo kwa sisi wa mpakani tunaipata RTD usiku pekee tena kwenye shortwave
Tulitegemea zaidi raidio za Kenya.
Kuna mwingine anaitwa Mrekoni alikuwa na kipindi chake kizuri cha karibu mgeni au mgeni wetu alifariki majuzi
He was talented.

Siyo Hassan Mgumba, jima lake halisi ni Hassam Mkumba alikuwa pia msomaji mzuri wa taarifa za habari
 
Watangazaji wengine wa zamani wa RTD waliowahi kuwa maarufu ni pamoja na Abdallah Majullah (alikuwa akitangaza mpira pamoja, Kipindi cha michezo n.k, Geofrey Erneo (Kipindi cha klabu raha leo akishirikiana na Enock Ngombale, alikuwa mahili pia katika kipindi cha majira na Harakati. Kipindi cha Mwanamuziki wetu n.k) Wilson Malosha (huyu alikuwa maarufu kwa matangazo ya vikao vya Bunge toka Dodoma) bila kumsahau Zawadi Machibya ambaye kwa sasa yuko BBC London.
 
Nimemkumbuka Malima Ndelema, huyu alikuwa bingwa wa kipindi cha ngoma za asili za makabila mbalimbali, sijui yu hai bado au sijui yu wapi sasa huyu mtu.

Ni watu waliokuwa wanakupa sababu na kukulazimisha kusikiliza radio tofauti kabisa na sasa!

Yaah Malima ni miongoni mwa watangazaji waliokuwa creative sana katika vipindi vyake. Vipindi maarufu alichokuwa akikitangaza kilikuwa kinaitwa 'Tumbuizo asilia na Mkoa kwa Mkoa'

 
List imemsahau Radio DJ wa kwanza wa enzi hizo:-
Said Omar Kassongo.

Nakumbuka mitumbuizo yake na story nyiiiingi. Ama kweli wametangulia watu wa ukweli!
Asante kwa kunikumbusha, Saidi Omari Kassongo mmoja wa watangazaji maarufu miaka ile ya mwishoni mwa miaka ya 60. Kwenye bandiko langu namba 209 nilimataja kimakosa kama Salim(?) Asante sana
 
Takribani miaka kumi hv iliyopita,kabla rtd haijabadilishiwa jina na kuitwa tbc 2,alikuwepo mtangazaji mahiri wa habari za michezo na msoma taarifa za hbr nguli aliyeitwa ezekiel malongo.Huyu mwanahabari alinikosha sana enzi zake lkn siku hz simsikii kabisa na siju alikimbilia wapi.Mwenye taharifa zaidi kumhusu anijuze.
huyu mtu nimemuona zaidi ya mara tano mahali kwenye ofisi ya umma, ana makovu kama mtu alienguka na pikipiki, amechakaaa, ananuka pombe, na inasadikiwa ni mwandishi kanjanja.
 
Baada ya kutimuliwa RTD (now TBC Taifa, maana pale Eda Sanga alikiuwa anamvumilia sana na mambo yake ya kulewa chakali ndo anakuja kazini), alikuwa anasimamia magari ya wanafunzi wa shule za Filbert Bayi (ambaye ni mjomba wake), akafukuzwa baada ya kuanza kuwakaza wanafunzi, then akawa dalali wa tiketi za mabasi pale Ubungo bus Terminal, napo akaacha, baadae akawa anashinda pale bar ya Rambo Manzese.

Kwa sasa yupo tu mtaani, ila kachoka sana, ukimuona utamuonea huruma kama vile mgonjwa.
 
Ndio mitihani ya maisha, ila akimpata mtu akampatia ushauri nasaha anaweza akajirudi na kupata kazi tena kwani media sasa hivi zipo kibao
 
Baada ya kutimuliwa RTD (now TBC Taifa, maana pale Eda Sanga alikiuwa anamvumilia sana na mambo yake ya kulewa chakali ndo anakuja kazini), alikuwa anasimamia magari ya wanafunzi wa shule za Filbert Bayi (ambaye ni mjomba wake), akafukuzwa baada ya kuanza kuwakaza wanafunzi, then akawa dalali wa tiketi za mabasi pale Ubungo bus Terminal, napo akaacha, baadae akawa anashinda pale bar ya Rambo Manzese.

Kwa sasa yupo tu mtaani, ila kachoka sana, ukimuona utamuonea huruma kama vile mgonjwa.

Mkuu sio kama ni mgonjwa ni mgonjwa tena sana, sema kwa Tanzania yetu hii kila mtu anakufa na chake. lakini jamaa anahitaji matibabu ya akili na ulevi wa kupindukia.
 
Huyu Jamaa nilimuona Bar 1 akiwa na Mzee Kisocky mbele yao kukiwa na "Nyagi" lakini hajachoka kihivyo!
 
Jamaa yupo fresh tu anakula bia zake hamuibii mtu wala hamuombi mtu, kijiwe chake mara nyingi ni samora nipo jirani nae sana, ni brother wangu na tunaonana karibu kila iitwapo siku.
 
Alikua Beki mstaarabu wa kupanda na kushuka.Nilimpenda sana.Vipi kuhusu Doctor Roy Maganga wa RFA,aling'ara sana katika kipindi cha Sitasahau.Sjui Kwa sasa yuko wapi.
 
inasikitisha sana nilikutana somewhere in dar es salaam last year nilitambulishwa kwake na rafiki yangu sikuamini macho yangu karibia chozi linitoke kwa kweli tumuuombee tu jamani ila JAMANI POMBE MBAYA
 
Back
Top Bottom