Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Baada ya kutimuliwa RTD (now TBC Taifa, maana pale Eda Sanga alikiuwa anamvumilia sana na mambo yake ya kulewa chakali ndo anakuja kazini), alikuwa anasimamia magari ya wanafunzi wa shule za Filbert Bayi (ambaye ni mjomba wake), akafukuzwa baada ya kuanza kuwakaza wanafunzi, then akawa dalali wa tiketi za mabasi pale Ubungo bus Terminal, napo akaacha, baadae akawa anashinda pale bar ya Rambo Manzese.

Kwa sasa yupo tu mtaani, ila kachoka sana, ukimuona utamuonea huruma kama vile mgonjwa.

nilikuwa mdogo sana wakat namsikia bek wa kupanda na kushuka hyo ndio raha ya kuhesabu vizibo
 
Jamaa yupo fresh tu anakula bia zake hamuibii mtu wala hamuombi mtu, kijiwe chake mara nyingi ni samora nipo jirani nae sana, ni brother wangu na tunaonana karibu kila iitwapo siku.

kwa namna ulivyojitahidi kumtetea inaonekana mpo katika status moja na wewe huenda nichapombe na mzugaji kama yeye. jamaa anahitaji msaada sio mtu wa kumtetea kwa ulivyoandika hapa wote mpo kwenye denial stage. jamaa kachoka na anakimbia watu wote wa maana, atajohook na mtu anaetaka kumtapeli na asiemjua tuu. au ataendelea kuwa na anaowajua but wenye upofu wa pombe kama yeye in short amechoka vibaya sanaaaa.
 
Mwaka juzi alikuwa anaonekana sana katika baa za ubungo na viunga vyake ingawa alikuwa hajachoka kivile na mara ya mwisho kabisa nilimwona kwenye sport kizaazaa ITV.
 
back in days namsikiliza jamaa ilikua ni kipindi cha michezo saa moja RTD tena kwenye redio ya mlinzi wa shule, siku asipokuepo ktk hicho kipindi basi wanafunzi wanaomzunguka yule mlinzi wanapungua. Wish you quick recovery E. Malongo.
 
akiwa first ladiiii Halima Mchuka
 
Alikua kampan moja na j mkaa100 kweye viti virefu..mwenzie mzoefu yy ikala kwake
 
Wanabodi,

Baada ya Kifo cha Mtangazaji Nguli nchini, Uncle J. Nyaisanga, naomba kuchukua fursa hii, kufanya reflection ndogo ya Watangazaji wa RTD waliotangulia mbele ya haki. Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.

Naomba nisizungumzie kulitowatoa duniani, wala hatima ya familia zao walizoziacha huku nyuma maana sio tuu nitazidi kuogopa, bali pia tutazidi kuumia!. Just imagine, kijitaasisi kidogo kama RTD chenye ofisi yake pale BH-Pugu Road kupoteza idadi kubwa hivi ya watumishi wake (tena hawa ninaowataja ni Watangazaji tuu!, achilia watumishi wengine!. Sii bure!, ila lazima tukubali ni kazi ya Mungu, na kazi ya Mungu haina makosa!.

Hii list sio walikufa lini ni random, nikiwakumbuka wengine nitawaongeza!
Tukianzia na

  1. David Wakati
  2. Abdul Masudi (Jawewa)
  3. Eli Mbotto
  4. Stephen Mlatie
  5. Siwatu Luanda
  6. Salama Mfamao
  7. Salim Seif Nkamba (Mjomba)
  8. Michael Katembo
  9. Nelly Kidella
  10. Halima Mchuka,
  11. Omar Jongo
  12. Tumboi Tamimu Risasi
  13. Mohamed Ng'ombo
  14. Abisai Stephen (Uronu)
  15. Stephen Lymo.
  16. Nadhir Mayoka
  17. Juma Ngodae
  18. Rukia Machumu
  19. Karim Besta
  20. Henrick Michael Libuda
  21. Idrissa Sadalah
  22. Bati Kombwa
  23. Iddi Rashid Mchatta
  24. Dominic Chilambo
  25. Hassan Mkumba
  26. Khadija Said
  27. Ally Saleh
  28. Kwegier Munthali
  29. Leonard Mtawa
  30. Khalid Ponera

Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.
Pia sio vibaya kuwaulizia wale watangazaji wa siku nyingi ambao hatujui walipo, ili kama nao wametangulia tuyaingize majina yao.

RIP All the Fallen Heroes wa Tasnia ya Utangazaji Tanzania!,

Pascal.

Umenikumbusha mbali sana. Enzi hizooo!!!
 
Matembele, asante kunikumbusha hiki kisa na majina na majina ya watangazaji hawa, by the time tunajoin RTD, kiliishatokea zamani kikihusishwa na ushirikina!.

Details haziko very clear ni walikuwa wanatoka shift au wanaingia shift ila gari ni landrover 110, ilikuwa na watu 8, watangazaji 4, fundi mitambo 3 na dereva, walipofika rail crossing gari ikazimika katikati ya reli, treni inakuja huku ikipiga honi, dereva na mtu wa mbele walifungua milangoi wakashuka, na wale watu watatu wawili nyuma pia wakashuka, walibaki watangazaji wanne waliokuwa wamekaa siti ya kati!, wote wanne walifia papo hapo!. Majina mawili ndio hayo, bado wawili wengine. Naomba yeyote mwenye details kuhusu ajali hii, atakumbushe vizuri, ila majina nimeta update kule mwanzao!.
Pascal.

Hii ajali inaelekea ina versions nyingi. Niliyonayo ni kuwa ajali ilitokea majira ya saa kumi/kumi na moja jioni hapohapo rail crossing ya Shaurimoyo. Na wahusika walikuwa ndani ya gari dogo la Mtangazaji Kwegier Munthali ambaye ndo akiliendesha na Ally Salehe pembeni akisoma gazeti. Nyuma alikuwa amekaa Hilda Mwaipopo na fundi mitambo ambaye jina limenitoka. Kwegier na Ally Salehe walikuwa trapped na walikufa kwa moto wakati Hilda Mwaipopo na fundi mitambo waliponea chupuchupu.

Hilda Mwaipopo alikuja hamia Kenya ambako aliolewa na sijui yu wapi dakika hii.

Hapo shaurimoyo pametokea ajali kadhaa siku hizo sijui siku hizi.
 
Sara Dumba, Jacob Tesha, Seleman Hega, Danstan Tido Mhando, Seleman Kumchaya, Peter Makorongo, Charles Hillary,

Omary Jongo, Ahmed Jongo, Sango Kipozi, Masoud Masoud, Aloisia Isabula,Aloisia Maneno, Debora Mwenda, Mikidadi Mahamoud, Juma Nkamia, Swedi Mwinyi, Ahmed Kipozi, Dominic Chilambo, Bati Kombwa, Nadhir Mayoka, Abdallah Majura,

Michael Katembo,Abisae Steven, Abdallah Mlawa,Nassoro Nsekeli,Bujaga Izengo Kadago,David Wakati,Khalid Ponera,Christina Chokunogela,Ahmed Kipozi,Siwatu Luwanda,Salim Seif Nkamba,Salama Mfamao,Bartholomew `Bati’ Kombwa

Ahmed Jongo,Dominic Chilambo,ngalieni Mpendu,Sekioni Kitojo,Chisunga Steven, Tumbo Risasi,
Edda Sanga,Mikidadi Mahmoud,Mshindo Mkeyenge.

Hii ilikuwa Lineup ya kutisha sio ujinga wa kipindi hiki hakuna ethics wala nini...................Wengine ongezeni.

Nawasilisha.
 
Line-up ya ukweli ingawa kuna majina yamejirudia.
Yupo mmoja amesahaulika, mwenyeji wa Rufuji nimemsahau jina.
 
Sara Dumba, Jacob Tesha, Seleman Hega, Danstan Tido Mhando, Seleman Kumchaya, Peter Makorongo, Charles Hillary,

Omary Jongo, Ahmed Jongo, Sango Kipozi, Masoud Masoud, Aloisia Isabula,Aloisia Maneno, Debora Mwenda, Mikidadi Mahamoud, Juma Nkamia, Swedi Mwinyi, Ahmed Kipozi, Dominic Chilambo, Bati Kombwa, Nadhir Mayoka, Abdallah Majura,

Michael Katembo,Abisae Steven, Abdallah Mlawa,Nassoro Nsekeli,Bujaga Izengo Kadago,David Wakati,Khalid Ponera,Christina Chokunogela,Ahmed Kipozi,Siwatu Luwanda,Salim Seif Nkamba,Salama Mfamao,Bartholomew `Bati’ Kombwa

Ahmed Jongo,Dominic Chilambo,ngalieni Mpendu,Sekioni Kitojo,Chisunga Steven, Tumbo Risasi,
Edda Sanga,Mikidadi Mahmoud,Mshindo Mkeyenge.

Hii ilikuwa Lineup ya kutisha sio ujinga wa kipindi hiki hakuna ethics wala nini...................Wengine ongezeni.

Nawasilisha.

Umechemsha hapo kwa Juma Nkamia,hajawahi kuwa mtangazaji wa kusifia kiasi cha kumkumbuka.
 
^^
Ezeckieli Malongo.. Katika misimu ya kombe la Dunia, anaweka vionjo, anakwenda..anakwenda..la la laaa (kumbe mpira upo katikati ya uwanja)
^^
 
Swedi mwinyi aisee...jamaa ana kipaji cha ajabu cha utangazaji hasa anapotangaza mipira utapenda hawa wa sasa wanajitahidi kwa mbali ingawa maadili yao yako chini mnoo
 
Swedi mwinyi aisee...jamaa ana kipaji cha ajabu cha utangazaji hasa anapotangaza mipira utapenda hawa wa sasa wanajitahidi kwa mbali ingawa maadili yao yako chini mnoo

Gooooooo...anakosa, Zamoyoni Mogela anapiga mpira ule unapita sentimita chache ya mwamba wa goli yapata urefu wa unyayo wa binti yangu mariam.......kionjo murua toka kwa sweeed bin mwinyi. Dah jamaa nlikua namkubali sana pamoja na jamaa mmoja alikua anatangazia Radio One, Aboubakar Liongo..
 
Back
Top Bottom