Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Mkuu Makah, Asante. Hawa kina Chihota hawa, Je walikuwa na Undugu wowote na Yule Norman Chihota ambaye katika kipindi hicho alikuwa akitamba sana kwenye Riadha hasa kwenye mbio za Mita 400 akiiwakilisha TZ kwenye michuano mingi ya kimataifa ya riadha??

Haswa - wale na Norman ni baba mmoja na mama mmoja - Norman alikuwa mdogo kwa hao wawili na mdogo wao mwingine akiitwa Gershom.
 
mi naona nyota hapa, namfaham charles hilary tu ila inatia faraja sana tukiwa tunakumbuka tulipotoka. aminia
 
Nimemkumbuka Malima Ndelema, huyu alikuwa bingwa wa kipindi cha ngoma za asili za makabila mbalimbali, sijui yu hai bado au sijui yu wapi sasa huyu mtu.

Ni watu waliokuwa wanakupa sababu na kukulazimisha kusikiliza radio tofauti kabisa na sasa!

Mkuu, sema tu hakukuwa na option nyingine ya kupata habari zaidi ya kusikiliza radio (RTD) na kusoma magazeti ya MZALENDO, DAILY NEWS, MFANYAKAZI, KIONGOZI, MWENGE nk.
 
Na huyu aliekuwa mtangazaji wa kipindi cha michezo EZEKIEL MARONGO YUKO WAPI?

If not mistaken, huyu Ezekiel Marongo niliwahi kumuona kule mkoani Shinyanga mwaka 2005 nikiwa ktk shughuli zangu.
Nadhani ni fundi mitambo ktk FM Radio moja hivi ya Roman Catholic, jina la Radio hiyo hata sikumbuki.
Nakumbuka alikuwa pamoja na Marcus Jacob, na Abdallah Tirata ambao sasa wako Star TV - Mwanza.
 
Kweli aise, mtangazaji alikuwa hawezi kuanza kipindi hadi amtambulishe fundi mitambo na anapomaliza kipindi lzm amshukuru.... wapi Lando Mabula

Lando mabula anapatikana kigamboni, Kilevi (pombe) imemuharibu!
 
Acha uongo Kipindi Cha chaguo la msikilizaji kilikuwepo tena kama sikosei saa nane mchana siku ya jumamosi

Kwa nini unashindwa kukosoa mtu bila kusema hilo la uongo? nidanganye ili nipate nini? siku ya Jumamosi saa nane kulikuwa na KIPINDI CHA MAMA NA MWANA, Chaguo la msikilizaji kilikuwa ni Radio 1, RTD kulikuwa na ombi lako
 
Nilichosema mimi ni kuwa hakukuwa na kipindi cha nyimbo za asili saa saba mchana kama mchangiaji mmoja alivosema hapo juu, saa saba mchana kulikuwa na taarifa ya habari. Mie sio wa juzi babadesi naweza kukutajia kuanzia jumatatu hadi jumapili jina la kipindi na mtangazaji wake na kinachukua muda gani, naweza kosea kidogo sana coz its longtime

...Ram, nawe Utaonekana ni wa Juzi Juzi tu! Kwa kipindi kirefu wakati Watangazaji hawa Nguli wakitamba hewani taarifa ya Habari ilikuwa ni Saa MOJA Asubuhi, Saa SABA Mchana, Saa MBILI Usiku, Saa NNE Usiku Sauti ya Mapinduzi ZBar na Saa TANO Usiku Taarifa ya Habari ya Masaa 24 kisha baada ya hapo kama ni Alhamisi kinafuata kipindi cha MISAKATOO! ambacho kilikuwa maalumu kwa ajili ya nyimbo mpya za bendi iliyokuwa imeenda kurekodi nyimbo zake mpya RTD siku chache kabla!
 
Ni kweli mwanzoni kbs kipindi kiliitwa ombi lako lakini kilikuja kubadilishwa jina na kuwa Chaguo la msikilizaji, muulize Malima Ndelema atakwambia

Sio Chaguo la msikilizaji, bali kilikuwa kinaitwa Ombi lako, na pia hakikuwa siku zote, siku zingine tulikuwa tunatupiwa mashairi (Malenga wetu),

CC: jazba
 
Last edited by a moderator:
Wanabodi,

Baada ya Kifo cha Mtangazaji Nguli nchini, Uncle J. Nyaisanga, naomba kuchukua fursa hii, kufanya reflection ndogo ya Watangazaji wa RTD waliotangulia mbele ya haki. Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.

Naomba nisizungumzie kulitowatoa duniani, wala hatima ya familia zao walizoziacha huku nyuma maana sio tuu nitazidi kuogopa, bali pia tutazidi kuumia!. Just imagine, kijitaasisi kidogo kama RTD chenye ofisi yake pale BH-Pugu Road kupoteza idadi kubwa hivi ya watumishi wake (tena hawa ninaowataja ni Watangazaji tuu!, achilia watumishi wengine!. Sii bure!, ila lazima tukubali ni kazi ya Mungu, na kazi ya Mungu haina makosa!.

Hii list sio walikufa lini ni random, nikiwakumbuka wengine nitawaongeza!
Tukianzia na

  1. David Wakati
  2. Abdul Masudi (Jawewa)
  3. Eli Mbotto
  4. Stephen Mlatie
  5. Siwatu Luanda
  6. Salama Mfamao
  7. Salim Seif Nkamba (Mjomba)
  8. Michael Katembo
  9. Nelly Kidella
  10. Halima Mchuka,
  11. Omar Jongo
  12. Tumboi Tamimu Risasi
  13. Mohamed Ng'ombo
  14. Abisai Stephen (Uronu)
  15. Stephen Lymo.
  16. Nadhir Mayoka
  17. Juma Ngodae
  18. Rukia Machumu
  19. Karim Besta
  20. Henrick Michael Libuda
  21. Idrissa Sadalah
  22. Bati Kombwa
  23. Iddi Rashid Mchatta
  24. Dominic Chilambo
  25. Hassan Mkumba
  26. Khadija Said
  27. Ally Saleh
  28. Kwegier Munthali
  29. Leonard Mtawa

Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.
Pia sio vibaya kuwaulizia wale watangazaji wa siku nyingi ambao hatujui walipo, ili kama nao wametangulia tuyaingize majina yao.

RIP All the Fallen Heroes wa Tasnia ya Utangazaji Tanzania!,

Pascal.
mmemsahau Khalid Ponera/ zilipendwa
 
mmemsahau Khalid Ponera/ zilipendwa
Mkuu Ponera, natanguliza pole maana majina yanafanana, sikujua kuwa hata Khalid Ponera katangalia!, ilikuwa lini?!. Nakumbuka wakati wa RTD alikuwa akiishi Ilala Flat na mkewe mmoja akifanya kazi Tea Bleanders!.
Nimeupdate main list
Pascal.
 
Salim Mbonde
...kuna dada (sasa hivi atakuwa ni Mmama) alikuwa anatangaza sana External Service of RTD
Mohamed/Omar Jongo? (nafikiri akina Jongo walikuwepo wawili)...au ni Ahmed Kipozi?
Abdul Ngalawa/Ngarawa
Jacob Tesha
Halima Kihemba?
Mikidadi Mahmood
Mohamed Akhnan

wa juzi juzi Charles Hillary, Betty Chalamila (Mkwasa), Sued Mwinyi na Aboubakary Liongo
 
Ogah, lengo ni kuwakumbuka waliotangulia mbele ya haki!. Hao wote uliowataja wapo labda kama lengo ni kuulizia wako wapi, nitakusaidia kidogo.

Salim Mbonde -amestaafu juzi juzi

...kuna dada (sasa hivi atakuwa ni Mmama) alikuwa anatangaza sana External Service of RTD -Hanna Mayige sasa ni Mwakilishi wa Mkurugenzi kituo cha Songea.

Mohamed/Omar Jongo? (nafikiri akina Jongo walikuwepo wawili) uko right kina Jongo wako wawili, Ahmad Jongo amestaafu na Omar Jongo (RIP)

Ahmed Kipozi ni DC-Bagamoyo
Abdul Ngarawa -ni msataafu.
Mikidadi Mahmood-Ni Mkurugenzi wa Radio Uhuru
Mohamed Akhnan simkumbuki labda ulimaanisha Mohamed Dahman yuko Sauti ya Ujerumani.
Charles Hillary yuko BBC
Betty Chalamila (Mkwasa) ni DC Bahi
Sued Mwinyi bado yuko TBC Kipindi cha Majira
Aboubakary Liongo alikuwa Ujerumani amerudi bongo.

Pascal.
 
Wanabodi,

Baada ya Kifo cha Mtangazaji Nguli nchini, Uncle J. Nyaisanga, naomba kuchukua fursa hii, kufanya reflection ndogo ya Watangazaji wa RTD waliotangulia mbele ya haki. Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.

Naomba nisizungumzie kulitowatoa duniani, wala hatima ya familia zao walizoziacha huku nyuma maana sio tuu nitazidi kuogopa, bali pia tutazidi kuumia!. Just imagine, kijitaasisi kidogo kama RTD chenye ofisi yake pale BH-Pugu Road kupoteza idadi kubwa hivi ya watumishi wake (tena hawa ninaowataja ni Watangazaji tuu!, achilia watumishi wengine!. Sii bure!, ila lazima tukubali ni kazi ya Mungu, na kazi ya Mungu haina makosa!.

Hii list sio walikufa lini ni random, nikiwakumbuka wengine nitawaongeza!
Tukianzia na

  1. David Wakati
  2. Abdul Masudi (Jawewa)
  3. Eli Mbotto
  4. Stephen Mlatie
  5. Siwatu Luanda
  6. Salama Mfamao
  7. Salim Seif Nkamba (Mjomba)
  8. Michael Katembo
  9. Nelly Kidella
  10. Halima Mchuka,
  11. Omar Jongo
  12. Tumboi Tamimu Risasi
  13. Mohamed Ng'ombo
  14. Abisai Stephen (Uronu)
  15. Stephen Lymo.
  16. Nadhir Mayoka
  17. Juma Ngodae
  18. Rukia Machumu
  19. Karim Besta
  20. Henrick Michael Libuda
  21. Idrissa Sadalah
  22. Bati Kombwa
  23. Iddi Rashid Mchatta
  24. Dominic Chilambo
  25. Hassan Mkumba
  26. Khadija Said
  27. Ally Saleh
  28. Kwegier Munthali
  29. Leonard Mtawa
  30. Khalid Ponera

Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.
Pia sio vibaya kuwaulizia wale watangazaji wa siku nyingi ambao hatujui walipo, ili kama nao wametangulia tuyaingize majina yao.

RIP All the Fallen Heroes wa Tasnia ya Utangazaji Tanzania!,

Pascal.
pascal, hawa nao huwakumbuki? Dastan Tido Mhando, Chama omari Matata, Godfrey Mngodo, Teckla Gumbo, (Salim?- Mume wa Zamzam Maalim),Ahmed Kipozi, Julius Nyaisanga, Sango Kipozi, Abdul Omar Masudi, Mshindo Mkeyenge etc
 
Ogah, lengo ni kuwakumbuka waliotangulia mbele ya haki!. Hao wote uliowataja wapo labda kama lengo ni kuulizia wako wapi, nitakusaidia kidogo.

Salim Mbonde -amestaafu juzi juzi

...kuna dada (sasa hivi atakuwa ni Mmama) alikuwa anatangaza sana External Service of RTD -Hanna Mayige sasa ni Mwakilishi wa Mkurugenzi kituo cha Songea.

Mohamed/Omar Jongo? (nafikiri akina Jongo walikuwepo wawili) uko right kina Jongo wako wawili, Ahmad Jongo amestaafu na Omar Jongo (RIP)

Ahmed Kipozi ni DC-Bagamoyo
Abdul Ngarawa -ni msataafu.
Mikidadi Mahmood-Ni Mkurugenzi wa Radio Uhuru
Mohamed Akhnan simkumbuki labda ulimaanisha Mohamed Dahman yuko Sauti ya Ujerumani.
Charles Hillary yuko BBC
Betty Chalamila (Mkwasa) ni DC Bahi
Sued Mwinyi bado yuko TBC Kipindi cha Majira
Aboubakary Liongo alikuwa Ujerumani amerudi bongo.

Pascal.

sawa nashukuru....lakini ninayemzungunzia mimi...inawezekana alishastaafu kwa sasa...nafikir alishawahi kuwa Mkurugenzi kipindi fulani.....jina bado limenitoka.....
 
Back
Top Bottom