Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Mkuu,umenitoa machozi.

Kulikuwa na watangazaji mahiri kama kina Bujaga Izengo Kadago,Omar Jongo,Ahmed Jongo,Nadhir Mayoka,Rashid Idd Mchata,Edda Sanga,Salah Dumba,Bett Chalamila,Sunday Shomari,Omar Liongo,Abdalah Majura na wengine wengi tu
 
RIP Dada Sarah Dumba.

Paskali
 
Ilikua mpira ukitangazwa na Ahmed jongo na Charles hilary utapenda uusikilize tu! Utamsikia Charles hilary kabla ya mpambano anakwambia;

"Eeeh! Refalee wa leo ni Meja gwaza Mapunda wa Morogoro" Dominic chilambo alikua akipenda kusema;

"Uwanja umenona,watu ni wengi kwelikweli,Polisi ni wengi pia!!

RTD ilikua ni radio ya wote aiseeee! Kitambo sana!
 
Hivi kile kipindi cha MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI kilikua kikiletwa na mtangazaji gani? Kwa mwenye kujua atujuze please!
 
Nimemkumbuka Malima Ndelema, huyu alikuwa bingwa wa kipindi cha ngoma za asili za makabila mbalimbali, sijui yu hai bado au sijui yu wapi sasa huyu mtu.

Ni watu waliokuwa wanakupa sababu na kukulazimisha kusikiliza radio tofauti kabisa na sasa!
Sasa hivi ni u know what n'm sayin..kubana pua na kulamba lamba midomo.Hawa watoto wa kiume,shida saana.Niliacha siku nyingi kusikiliza radio.
 
Vipindi:
1.0 Kutoka Umoja wa mataifa (UN)
2.0 Mbiu ya Mikoa
3.0 Wakati wa kazi
4.0 Mgeni wetu
5.0 Kipindi cha wagonjwa/salaam za wagonjwa
6.0. Bendi zetu
7.0 matangazo ya vifo
8.0 Club raha leo
9.0 Tumwabudu Mungu
10.0 Ana kwa Ana
11.0 Majira
12.0 ''kipindi cha nyerere' (ilikuwa baada ya taarifa ya habari ya saa 2 usiku)
 
Daaah!! Heshima kwako mkuu,asante sana kwa huo wimbo,nimejikuta nausikiliza huku nimejaa majonzi telee!! Kitambo sana Mkuu.
 
Mh hii post ya mwaka 2013. Lkn ina jina la aliyefariki jana. Hii ikoje?
 

Wakuu hebu tukumbushane enzi zile za Radio Tanzania, enzi ambazo Radio ndio ilikuwa kila kitu katika suala zima la kupata habari. Tukumbushane watangazaji mahiri wa enzi zile, vipindi vizuri pamoja na vituko mbalimbali ambavyo huwezi kuvisahau enzi za RTD.

Karibuni...
 
Nakumbuka usomaji wa taarifa ya habari wa Christi e Chakunegela saa nne usiku alisoma bila kukosea hata neno moja na taarifa ya habari ilikuwa kama vile inasomwa na software

Namkumbuka Mahokaaaaaaaa!!!!

Mikingamo mwendo wa kuchomeana utambi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…