Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu,umenitoa machozi.
Mtangazaji wa zaman wa RFA alikuwa anaendesha show za burudan kwa ss nakifiri yuko clouds FM team ya wahariri
Mkuu,umenitoa machozi.
Enzi hizo za kuchaguzi mkuu kulikuwa na jamaa anaitwa SPENCER LAMECK alikuwa anareport vizuri sana asee
Prince Baina Kamukulu (R.I.P)
EZEKIEL MWALONGO
Moses Justin (R.I.P)
FLORA NDUCHA
ROSE CHITALA......
RIP Dada Sarah Dumba.ALIYEKUWA mkuu wa wilaya ya Njombe na mwanahabari mkongwe Bi Sarah Dumba amefariki dunia ghafla akiwa wilayani Njombe mkoa wa Njombe.
Mkuu huyu wa Wilaya amefariki usiku huu kwa Presha na mwili wake umehifadhiwa Hospitali ya Wilaya ya Njombe, Kibena
Sasa hivi ni u know what n'm sayin..kubana pua na kulamba lamba midomo.Hawa watoto wa kiume,shida saana.Niliacha siku nyingi kusikiliza radio.Nimemkumbuka Malima Ndelema, huyu alikuwa bingwa wa kipindi cha ngoma za asili za makabila mbalimbali, sijui yu hai bado au sijui yu wapi sasa huyu mtu.
Ni watu waliokuwa wanakupa sababu na kukulazimisha kusikiliza radio tofauti kabisa na sasa!
Vipindi:
1.0 Kutoka Umoja wa mataifa (UN)
2.0 Mbiu ya Mikoa
3.0 Wakati wa kazi
4.0 Mgeni wetu
5.0 Kipindi cha wagonjwa/salaam za wagonjwa
6.0. Bendi zetu
7.0 matangazo ya vifo
8.0 Club raha leo
9.0 Tumwabudu Mungu
10.0 Ana kwa Ana
11.0 Majira
12.0 ''kipindi cha nyerere' (ilikuwa baada ya taarifa ya habari ya saa 2 usiku)
Daaah!! Heshima kwako mkuu,asante sana kwa huo wimbo,nimejikuta nausikiliza huku nimejaa majonzi telee!! Kitambo sana Mkuu.Huyu alikuwa sister wangu sana, wimbo wake wa mwisho kabla hajaanza kuumwa uliitwa "Ousmane Bakayoko", siku ya kifo chake nilimpigia wimbo "Salama" wa Marijani Rajab
Nkizisikia nyimbo hizi, namkumbuka sana Salama!.
Nawe Mkumbuke.
Marijani Raajab - Salama - YouTube
Pascal
Mh hii post ya mwaka 2013. Lkn ina jina la aliyefariki jana. Hii ikoje?Wanabodi,
Baada ya Kifo cha Mtangazaji Nguli nchini, Uncle J. Nyaisanga, naomba kuchukua fursa hii, kufanya reflection ndogo ya Watangazaji wa RTD waliotangulia mbele ya haki. Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.
Naomba nisizungumzie kulitowatoa duniani, wala hatima ya familia zao walizoziacha huku nyuma maana sio tuu nitazidi kuogopa, bali pia tutazidi kuumia!. Just imagine, kijitaasisi kidogo kama RTD chenye ofisi yake pale BH-Pugu Road kupoteza idadi kubwa hivi ya watumishi wake (tena hawa ninaowataja ni Watangazaji tuu!, achilia watumishi wengine!. Sii bure!, ila lazima tukubali ni kazi ya Mungu, na kazi ya Mungu haina makosa!.
Hii list sio walikufa lini ni random, nikiwakumbuka wengine nitawaongeza!
Tukianzia na
- David Wakati
- Abdul Masudi (Jawewa)
- Eli Mbotto
- Stephen Mlatie
- Siwatu Luanda
- Salama Mfamao
- Salim Seif Nkamba (Mjomba)
- Michael Katembo
- Nelly Kidella
- Halima Mchuka,
- Omar Jongo
- Tumboi Tamimu Risasi
- Mohamed Ng'ombo
- Abisai Stephen (Uronu)
- Stephen Lymo.
- Nadhir Mayoka
- Juma Ngodae
- Rukia Machumu
- Karim Besta
- Henrick Michael Libuda
- Idrissa Sadalah
- Bati Kombwa
- Iddi Rashid Mchatta
- Dominic Chilambo
- Hassan Mkumba
- Khadija Said
- Ally Saleh
- Kwegier Munthali
- Leonard Mtawa
- Khalid Ponera
- Ben Kiko
- Restuta Bukholi
- Sarah Dumba
Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.
Pia sio vibaya kuwaulizia wale watangazaji wa siku nyingi ambao hatujui walipo, ili kama nao wametangulia tuyaingize majina yao.
RIP All the Fallen Heroes wa Tasnia ya Utangazaji Tanzania!,
Pascal.
NB. Pia unaweza Kupata Taarifa za Baadhi ya Watangazi waliotutoka hapa.
Tribute to David Wakati, Kikwete, Mengi, Nchimbi na ...
Tribute to David Wakati: His Legacy Will Live On!
Mzee David Wakati Katutoka Leo Translate this page
Tribute To Uncle J. Nyaisanga: Jee Unamkumbuka kwa Lipi?!. Kuagwa ...
TBC haikumtendea haki marehemu David Wakati - Jamii Forums
- Tribute to Halima Mchuka: Alikuwa Mtu wa Watu!
Halima Mchuka hatunae duniani - Page 2 - JamiiForums
Hii RTD unaikumbuka? - JamiiForums
Msiba wa halima mchuka hauna nafasi tbc - JamiiForums
Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa RTD - Jamii Forums
Topic: Nimewakumbuka hawa pia..................zamani... - Jamii ...
Mtangazaji Maarufu wa RTD Amefariki Dunia Asubuhi Hii ..