Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Pia kulikuwa na kipindi cha muziki wa mwambao. Taarab laini zina jumbe nzitinzito ndani yake ila wameweka mafumbo mpk unaumia kichwa siku hizi mambo hadharani
 
Kama sijakosea ni Juma Kilaza
 
Dada Sango upo wapi nakukumbuka Dom wakati mmehamishiwa kule na mmeo. Sauti ya Sango na Ahamed ilikuwa inakosha jamani. Dada Sango kama upo humu ni PM tujuzane ya zama zile.
 
Jamani wazee wenzngu munamkumbuka Ben Kiko?


Ben Kiko alifariki mwaka juzi nadhani...


Daaah namkumbuka kumbe alifariki maskini

Jamani, sina uhakika naweza kukosolewa, maana enzi hizo sikuwa na access ama control ya radio - kila kitu kuhusu radio kilikuwa chini ya mzee,

Inasemekana jamaa (Ben Kiko) alikuwa reporter kwenye vita ya Kagera (alikuwa uwanja wa mapambano/ mstari wa mbele), bahati mbaya jeshi letu lilipata dhahama kwamba tulikuwa tunashambuliwa adui - jamaa alisikika akisema "ndg zangu tunashambuliwa hapa, tunapigwa jamani......" na maneno kama hayo. Kuona hivyo jamaa aliondolewa front na kurudishwa Tabora.
 
Hiyo hadithi hata mimi niliwahi kuisikia
 
Au Juma Mrisho wa Urafiki Jazz Band
We wangu nikimweka harudi. Naona gavana zimeanza kukaza hata hapa JF. Kuna mtu kasema tuanze mgomo naye kaonja yangu. Vipi tuungane tugome????
 
Nakumbuka ule wimbo wa salamu kwa wagonjwa...[emoji445] wakati umewadia wa salamu kwa wagoonjwaaa mahosipitalini tunawapa poleee [emoji445]
 
Reactions: bbc
Mie simjui huyo Juma. Anaitwa Juma nani?
 
Hiyo hadithi hata mimi niliwahi kuisikia
Ben baada ya Tabora alikaa sana Dodoma. Alijenga na kuishi hapo hata baada ya kuretire. Ben ninachokikumbuka sana ni yeye kuugua kipindu pindu mwaka 1989. Alilazwa kwenye kambi ya kipindu pindu na alisema kosa ni kula samaki wa kukaanga wabaridi. Kumbuka miaka ya kata mbuga Arusha to Moshi. Alitangaza majira kuhusu watu wa Dodoma kukata mabomba na kutengeneza hereni na bangiri. Ukiona Bangiriiii nyeusi na hereniii zake ujue ni mabomba ya majiiii Dodomaaaa!!!!!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…