Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV


Mkuu ongeza tangazo bima ....Bima yako,..kwa ajali..bima yako kwa majanga... na kulikuwa na promo ya mshikamanooo mshikamanoo...kumekuchaaa
 
Namkumbuka pia Edda Sanga wa kipindi cha mama na mwana pia alikuwa mmahiri sana wa kusoma habari pamoja na mtangazaji Mwafisi kwa habari walikuwa vizuri
....viashiria vyote kilikuwa kinanikonga kile cha Majira...na jingle ya uzazi wa mpango...wameiona nyota ya kijani ya uzazi wa mpango..zindukaa🙂
 
Mimi siyo wa zamani saana ila nakumbuka tuu haya machache:
-twende na wakati
-pilika pilika
-Michezo ba ezekiel marongo
-Mpira wachaa wee
 
Mazungumzo baada ya habari pamoja na maneno hayoooooo
Ivi yule jamaa wa mazungumzo baada ya habari na maneno hayo alikuwaga nani maana alikuwa na maneno kuntu sana yule jamaa! Yuko wapi na anajishughulisha na nini?
 
Pia kulikuwa na kipindi cha muziki wa mwambao. Taarab laini zina jumbe nzitinzito ndani yake ila wameweka mafumbo mpk unaumia kichwa siku hizi mambo hadharani
Pendoooo linauaa lasumbuaa walimwenguuu walimwenguuu walimwengu pendooo
 
Ivi yule jamaa wa mazungumzo baada ya habari na maneno hayo alikuwaga nani maana alikuwa na maneno kuntu sana yule jamaa! Yuko wapi na anajishughulisha na nini?
Mpendu na Shaban Kisu
 
Na katika kipindi cha majira hakuna aliemzidi Nsuma Ernest kusign out...alikuwa anavuta jina lake mimi ni Nsuuma Err... those were days aisee! 🙂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…