Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Ezekiel Malongo mwenye saut ya pooz na yapekee kwa kutangaza mpira ni hatar pia bila ya kumsaha Halima Mchuka mwanamama wa kwanza kutangaza mpira
 
"""Watoto ,watootoo wa Afrika ,karibuni kipindiii cha watoto, msikie nyimbo hadithi na mengineyo ,mambo muhumu na masomo, .....sogea karibu nasi tushikiane karibuni watotoooooooooooooooo woteeeeee ......nani anakumbuka hii nyimbo RTD? ???
 
Juma Kilaza
 
Saa mbili kasoro robo Michezo nilikuwa nikisikia tone ile back in 70's wow
Ninayo ile tune ila sijui jinsi ya kuipost hapa jf nipe namba yako nikutumie kwa whatsapp uiweke hapa jf ili wadau wengine nao wakumbukie
 
Mama na mwana
Dah ila mzee jangala na mwanae tomato walikua wanazingua
 
Reactions: ram
Nakumbuka watu walikua wanabet kabla ya taarifa ya habari walikua wanataja mtangazaji atakae soma hiyo habari ukipatia na mwenzio akakosea basi wewe utachukua pesa mlizoweka nikikumbuka nacheka sana
 
mkuu enzi hizo betri (ziliitwa mawe) zikikuwa rafiki sana kwa bajeti ya familia. kuna redio za mbao betri zikiwekwa kwenye kasha (cylinder ya plastic) na kutumika si chini ya miezi 6. kazi kubwa kuzichemsha kwenye maji na kuanika tu. ningali mdogo nilitumwa kununua mawe NATIONAL SPECIAL (za kijani) nikasahau, muuza duka kanifungashia za Burundi nikarudishwa kwa bakora. watu walitambua umuhimu wa hbr japo kulighubikwa na uhaba wa redio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…