Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Wakuu hebu tukumbushane enzi zile za Radio Tanzania, enzi ambazo Radio ndio ilikuwa kila kitu katika suala zima la kupata habari. Tukumbushane watangazaji mahiri wa enzi zile, vipindi vizuri pamoja na vituko mbalimbali ambavyo huwezi kuvisahau enzi za RTD.

Karibuni...
Ezekiel Malongo mwenye saut ya pooz na yapekee kwa kutangaza mpira ni hatar pia bila ya kumsaha Halima Mchuka mwanamama wa kwanza kutangaza mpira
 
"""Watoto ,watootoo wa Afrika ,karibuni kipindiii cha watoto, msikie nyimbo hadithi na mengineyo ,mambo muhumu na masomo, .....sogea karibu nasi tushikiane karibuni watotoooooooooooooooo woteeeeee ......nani anakumbuka hii nyimbo RTD? ???
 
wanafuta hawa mods ni yule wa Moro Juma ****** najua watafuta tena. Yule mzee aliyeimba "Njoo tucheze rumba rumba michangani aaaaaa rumba michanganiii" Hivi hakuwa mwanzilishi wa Cuban marimba kweli??? Wa moro. Jina wanalibana sababu ni sawa na wale alosema baba J. kuwa walifukuzwa. Weka singular badala ya wingi.
Juma Kilaza
 
Saa mbili kasoro robo Michezo nilikuwa nikisikia tone ile back in 70's wow
Ninayo ile tune ila sijui jinsi ya kuipost hapa jf nipe namba yako nikutumie kwa whatsapp uiweke hapa jf ili wadau wengine nao wakumbukie
 
Mama na mwana
Dah ila mzee jangala na mwanae tomato walikua wanazingua
 
  • Thanks
Reactions: ram
Nakumbuka watu walikua wanabet kabla ya taarifa ya habari walikua wanataja mtangazaji atakae soma hiyo habari ukipatia na mwenzio akakosea basi wewe utachukua pesa mlizoweka nikikumbuka nacheka sana
 
1465713192114.jpg
 
mkuu enzi hizo betri (ziliitwa mawe) zikikuwa rafiki sana kwa bajeti ya familia. kuna redio za mbao betri zikiwekwa kwenye kasha (cylinder ya plastic) na kutumika si chini ya miezi 6. kazi kubwa kuzichemsha kwenye maji na kuanika tu. ningali mdogo nilitumwa kununua mawe NATIONAL SPECIAL (za kijani) nikasahau, muuza duka kanifungashia za Burundi nikarudishwa kwa bakora. watu walitambua umuhimu wa hbr japo kulighubikwa na uhaba wa redio.
 
Back
Top Bottom