Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Kipindi cha starehe na BP kikiongozwa na uncle J Nyaisanga mungu ailaze roho yake mahali Pema.
 
Siku hizi hawa Facebook wanasikiliza akina kibonde na wazee wa kukojoza basi
Mkuu umefanya nicheke! Wazee wa kukojoza hahhhhh! Social media imeteka akili za watu. Enzi hizo ulikuwa unasubiri kwa hamu kusikiliza taarifa ya habari, michezo n.k kuna kipindi nilikuwa nakipenda sana 'tuimbe sote'
 
Mkuu umefanya nicheke! Wazee wa kukojoza hahhhhh! Social media imeteka akili za watu. Enzi hizo ulikuwa unasubiri kwa hamu kusikiliza taarifa ya habari, michezo n.k kuna kipindi nilikuwa nakipenda sana 'tuimbe sote'
Kweli mkuu, social media imeharibu utaratibu wa mambo mengi sana.

Ndg yangu hicho kipindi cha tuimbe sote nadhani pia kilisadia sana kumtangaza captain Komba (RIP), na mzee Mwinamila "kuleni chakula bora cha kuujenga mwili, na kulala pawe Bora...."
 
Je cha ngoma zetu na yule rafiki yake na Ben Kiko sikumbuki jina ngoja nilitafute.Alipenda kuwaweka wajaluo na ngoma zao halafu ataweka wahaya halafu wakurya. Alikuwa mchokozi wa watani. Ni mtu wa kusini alishatangulia mbele ya haki ila alikuwa na sauti nzuri saaana.
 
Hadithi zake kama mfalme binti chura, ua jekundu.. Yaani ilikua as if unaangalia filamu

Niliwahi kusoma kitabu cha binti chura nikiwa darasa la 3, ilikuwa bonge la stori yule mama sijui yuko wapi....
 
Yaani jamani utoto bwana. Mi nakumbuka nikiwa darasa la pili nikawa naenda saa nane shule wakati wengie woote ( broethers& sisters) wanaenda asubuhi. Sasa mimi naachwa na houseboy na housegirl. sasa housegirl anaenda sokoni ananichukua nakumbuka tunapitia nyumba Fulani ( hizi zilikuwa za serekali) na yetu ilikuwa ya serekali maeneo yanaitwa uzunguni, sitataja Mkoa isiwe identified. Basi sasa ndio najua huyo housegirl alikuwa anaenda kwa BF napewa fizzes ( sidhani kama sasa zipo) ileinawekwa kwenye maji unakunywa kama juice ( note: sio kuwa nyumbani havikuwepo basi tu utoto) napewa na buiscuit nakunywa wao wana- disappear. Jamani haya mambo unaweza andika kitabu!
 
Kipindi cha ngoma za asili na Mkoa kwa Mkoa navikumbuka sana na natamani hata leo nipate fursa ya kuzisikiliza nyimbo za makabila mbali mbali
Na Michael Katembo ( RIP) alikichangamsha kipindi!
 
Reactions: Auz
Nakumbuka mengi tu, jambooo, tuimbe sote, mwanamziki wetu, misakato, mkoa kwa mkoa, pole kwa kazi, mchana mwema, ombi lako, jioni njema, sukitaa, ATC hewani, mahokaa, mama na mwana, mchezo wa redio wa kina mzee jongo na jangala na vingine kibao. Watangazaji mahiri kama siwatu Luanda (RIP), abdallah ngalawa, Michael Katembo, David Wakati, Budyaga Izengo Kadago, somebody Aswile huyu alikuwa mke wa mchezaji wa Yanga Godwin Aswile bila kuwasahau wawakilishi wa mikoani Adisai Steven, Ben kiko, Dominic Chilambo, ilikuwa raha sana siku hizo
 
nakumbuka kuwa mjomba alikuwa anakuja usiku kusikiliza taarifa kisa mama ana hitachi
 
Unamkumbuka mtoto wa mzee jangala! Mshamu... Zilikuwa haziivi kabisa na Baba yake.
Tutumie kibuku uuuu ni pombe bora, tumia kibuku ni pombe bora, ngoja nirudi nije nighani kama yule dada[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kweli kabisa, huko KBC unakutana na harambeeee
 
Unamkumbuka mtoto wa mzee jangala! Mshamu... Zilikuwa haziivi kabisa na Baba yake.
Tutumie kibuku uuuu ni pombe bora, tumia kibuku ni pombe bora, ngoja nirudi nije nighani kama yule dada[emoji23] [emoji23] [emoji23]
you made my evening.
 
Reactions: ram
Ua jekundu ilikiwa sikosi.. unasimuliwa mpaka inahisi unaangalia video ya kinachosimuliwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…