Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Michael Katembo
 
Malenga wetu bana
 
Tumbuizo asilia zilikuwa zinapigwa nyimbo za makabila yote tz

Wooh.... good memories kwakweli, yaani it can't happen again
Tulikuwa tunawajua watangazaji wote kwa sauti zao tu, kabala hata hajataja jina, unajua huyu ni Aleicia Maneno au christine chokunogela, au Siwatu Luanda (she was cute kwa sura na sauti yake pia) na wengine wengi....
 
Mkuu umefanya nicheke! Wazee wa kukojoza hahhhhh! Social media imeteka akili za watu. Enzi hizo ulikuwa unasubiri kwa hamu kusikiliza taarifa ya habari, michezo n.k kuna kipindi nilikuwa nakipenda sana 'tuimbe sote'

Kwenye hiki kipindi kwaya za jeshi na mashirika mbali mbali ndio utazisikia humu, Marehemu Komba nae alianzia mbali tangu "Tuimbe Sote"
 

Kuna kipindi likuwa lazima tusikilize shuleni, kile cha masomo sikumbuki kinaitwaje ila mnasikiliza mwanzo mwisho baadae mwalimu anaanza kuuliza maswali kutokana na kilichofundishwa.
Kipindi cha wakati wa kazi, kilikuwa marvelous hiki kilikuwa kinawahoji wafanyakazi wa mashirika mbali mbali jinsi wanavyofanya kazi, so ilikuwa ni rahisi kujua mashirika yanafanya kazi gani, changamoto wanazokutana nazo n.k
 
Wazungu wanasema "Old is Gold" tulikua pembeni ya babu zetu tukifatisha wasoma habari.

Na kuna kale kamwimbo ukikasikia tu unajua mida wa kuamka kwenda shule...daah kalikia kanakata stim zooote.
 
Duuh wazee hadi matangazo ya vifo mlikua hamyakosi
 
Wazungu wanasema "Old is Gold" tulikua pembeni ya babu zetu tukifatisha wasoma habari.

Na kuna kale kamwimbo ukikasikia tu unajua mida wa kuamka kwenda shule...daah kalikia kanakata stim zooote.
Unadhani 42_0007, Old is Gold indeed!
 
Lakini yoote Tisa ukisikia sauti ya David WAKATI wacha kabisa. alijua anatangaza nini!!
halafu lugha waliijua barabara. kiswahili sanifu. sio cha mtaani.
ukija kwemya mpira - raha tupu
mkute ahmed Jongo
Salim Mbonde
mikidadi mahamood
dominic Chilambo
baadaye abubakar Lyongo

taarifa za majira- Ben Kiko- mnakumbuka wakati wa vita vya kagera alitoa live mpaka wakamrudisha nyuma
( WAKAJA WAKAMUOWA....... endelea...)

Yapo mengi.
 
Zile ngoma zilizokuwa zikipigwa kama kiashiria cha kuanza kwa taarifa ya habari, kilikuwa kiashirio cha watoto kukaa kimya vinginevyo tulikula bakora toka kwa wakubwa.
Kwakweli zamani kila kitu kilikua kwenye mpangilio..
 
Kipindi cha Lugha Ya Kiswahili nilipenda sana wimbo(jingle) yake
"Tanzania Bara na Visiwani....ya Taifa hili lugha...." Nimesahau unavyoendelea.

Pia kipindi cha rushwa. Wimbo wake
"Wito nautoa kwa taifa zima, tuchukie rushwa kwani ni adui...."

Pia Mahoka na Pwagu na Pwaguzi.

Mchezo Wa redio nilikuwa nampenda mwigizaji mmoja akiitwa Matuga.
.
 
Dah! Huo wimbo wa salam za wagonjwa hospitalini ulikuwa unanikosha sana!
 
Kulikuwa na igizzo moja na mtu mmoja alikiwa anaitwa sande aliye kuwa dereva wa magari ya mzigo akapata ukimwi. Aisee then kulikuwa na kina jangala anzi hizo,mzee pwagu etc
 
1. Nakukumbuka kile kipindi cha ATC hewani .... basi mie nikisikia ule mngurumo wa ndege mie roho kwatu kama nimepanda vile.
2. Kahawa ni mali, yule mama sijui anaitwa Bernadeta Kulaya alikuwa mtangazaji...lafudhi ya kichaga
3. Mama na Mwana.... hasa ikiwepo hadithi za binti chura mie raha.
4. Kile kipindi cha mchana mwema, salamu ...nikisika tu najua niwakati wa uji kunyeka
5. Sikiliza Bwana Umeme....
6. Kipindi cha Jambo
7. Halafu Zilipendwa
8. Kile pindi cha dini Jumapili hasa mida ya Jion, ilikuwa simanzi kwangu
9. Ila nilikuwa sipendi kipindi cha salam...wakianza hapo watatajana weee mpaka inakera
10. Majira
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…