Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Mchezo wa mzee Jangala ikidhaminiwa na pombe aina ya chibuku, nakumbuka nyimbo, idara yetu ya uhamiaji nalo jukumu kubwa saanaaaa kuwakaribishaa kuwasafirishaa na kulinda mipaka yetu[emoji441][emoji443][emoji443][emoji445][emoji445]

Watoto wasafi moyonii ni nyoota za macho ya wazaziiiiii[emoji445][emoji445][emoji445][emoji443][emoji443][emoji441]

Shamba aaanii shambaani shambaani mazaoo boora shambaani, haya twendenii shaambanii wananchi tukaalimeee [emoji443] [emoji444] [emoji446] [emoji447]

Wanawakee wa Tanzania wazuuuriii saaaanaaa, wanawakeeee tanzaniaa maendeleo tanzaniaaaa[emoji445][emoji443][emoji441][emoji443][emoji445]

Kuleni chakula boora cha kuujenga muili naku.... Pa kulala pawe boraa[emoji443][emoji445][emoji441]

Wakati umewadia wa salam za wagonjwa hosipitalinii leo tunawapa poleee, ajuaye bwana Mungu kwa mfu kuwa mzima mgonjwa kuwa salamaa leo tunawapa polee[emoji445][emoji445][emoji443][emoji445][emoji445][emoji441]

Wananchiiiii tujifunzeni ushirikaaaaa wananchi tujifunzeni ushirikaaaaa [emoji441][emoji445][emoji445][emoji445][emoji445]

Jamani vitaa imetangazwaa jamaaa wananchi wote tuwe imara, vijijini na mjini msisite kuwasema walanguzi[emoji445][emoji445][emoji445]


Matangazo sasa
1. Tumaa vifurushiii barua na pesa vitu mbalimbali vifike harakaaa tena kwa uhakikaaa, itumie sasaa shirika la posta na simu tanzaaaaniaaa ndio tegemeo letuu.

2. Hebu jitokezeee jioneshe simamaa mbelee za watuuu

3. Tairi general kutoka arushaaa tanzaaaaniaaa

4. Revolaaa revolaaaaa revolaaaaaa revolaaaaaaaa

5. Wee acha kula mali ya umma wee acha kujitafuna tafuna weeeee, wachaaaaaaaaa

6. Tumia chibuku ndio pombe bora, radha ya chibuku hujulikana, sifa moja na nyinginezo ni kulinda hadhi ya mnywaji

7. Komoooooaaaaa aaa komooooaaaa komoaaaa

8. Benki ya akiba ya posta ndio yako, benki ya akiba ya posta ni kwa watanzaniaaa woooote wakubwa kwa wadogo... Wananchi unaweza kufungua akaunti ya kawaaida, akaunti ya muda na akaunti ya muda maaalum.. Usingoje kesho ooo fungua akaunti yako leooo

Watangazaji hahaha Mama Deborah, Dominic Chilambo
Nimejikuta napata sweet memories tu
Umetisha
 
Nakumbuka nilikua sifaham maana ya kipindi cha "club raha leo shoooow" kikinikera kweli kikianza! Na hakuna station nyingine kubadilisha labda tuweke cassete ya UB40! Time hizo baba awe hajarudi home lkn, akirudi hatuna tena access na radio! Those were days
Heri yako wewe ulikuwa na option ya cassette, sisi ilikuwa only Radio basi, nakumbuka kitu kikubwa brand ya "National Panasonic". Iwapo hupendi kipindi/ program fulani option ilikuwa ni kuchagua KBC Nairobi, na huko KBC ulikuwa unaombea usikutane na ile miziki yao ya "kanindo"
 
Nakumbuka nilikua sifaham maana ya kipindi cha "club raha leo shoooow" kikinikera kweli kikianza! Na hakuna station nyingine kubadilisha labda tuweke cassete ya UB40! Time hizo baba awe hajarudi home lkn, akirudi hatuna tena access na radio! Those were days
Nyie mlikuwa watish mna cassete? Nilikuja kuiona baba mdogo alikuwa mwalimu alipoinunua lakini hiyo ilikuwa tape recorder anaenda anarecord watu kwenye bar. Sisi ni redio tu ila tuliona tumewini sana.
 
1 Taarifa ya habari na ile ngoma ya yule mzee asiyeona na ngoma kumi
2. Wakati wa kazi. "ujuzi niliupata hapa hapa kazini"
3. Hii ni kwaresimaa.
4. Lala salama.
5. Vipindi vya masomo ya shule za msingi tukikaa darasa zima watoto 40 na kusikiliza mwalimu wa redio. Wengine hata hiyo redio ilikuwa haisikiki vizuri lakini ilikuwa lazima mhu!
6. Kipindi cha wagonjwa. (Ajuaye bwana Mungu kwa mzima kuwa mfu, mgonjwa kuwa salaaaama leo tunatoa pole).
7. Mchezo wa Redio (Mkataa pema pabaya panamwita) Sikosi hapo. watu mnakaa kana kwamba mnawaona akina Jangala na wenzie na yule mwenye sauti kubwa na yule mama aliyekuwa na roho mbaya. Mtu unamchukia mtu hata bila kuona sura yake.
8. Mpiraa. Nakumbuka Yanga ilikuwa inacheza na Simba 74 tulipiga teke redio ya baba mimi na kaka yangu. Tulikula mkong'oto.
9. Hotuba za Mwalimu. Kila wakisema anaongea na wazee wa Dar ujue kuna kitu. Hapo hatutoki kama tupo likizo, wazee wote wa jirani wanakuja kwetu ili wasililize hotuba. Shuleni boarding kulikuwa na redio moja inazunguka kila bweni kila week.
10. Mchana na usiku mwema na miziki yake!! We acha akina Mbaraka Mwinshehe, Juma ******, Marijani Rajab, Western Jazz, Ndala Kasheba, Polisi Jazz, JKT, Tankat Almasi, Taarab nk. Samahani nimeandika mengi lakini ni kama therapy kutoa haya ya sasa kichwani. Big up mtoa mada.
Mzee mbona hapo kwenye Juma haisomeki ni Juma gani huyo?
 
mazungumzo baada ya habari
kiipindi cha wagonjwa, ujumbe wa leo n.k kwa kuwa RTD ilikuwa pekee basi wanasiasa wa wakati ule walineemeka na kutukuka sana. Ni kipindi CCM ilijijenga kwa watu wote kwa mikutano yao, nyimbo za kina Komba, hotuba za viongozi n.k
Watangazajji waliotajwa ongeza na Kina Jacob Tesha kwa kusoma habari.
Mshindo Mkeyenge na Ahmedi Jongo muruwa kwenye matangazo ya mpira.
 
Mzee mbona hapo kwenye Juma haisomeki ni Juma gani huyo?
wanafuta hawa mods ni yule wa Moro Juma kilaza najua watafuta tena. Yule mzee aliyeimba "Njoo tucheze rumba rumba michangani aaaaaa rumba michanganiii" Hivi hakuwa mwanzilishi wa Cuban marimba kweli??? Wa moro. Jina wanalibana sababu ni sawa na wale alosema baba J. kuwa walifukuzwa. Weka singular badala ya wingi.
 
wanafuta hawa mods ni yule wa Moro Juma ****** najua watafuta tena. Yule mzee aliyeimba "Njoo tucheze rumba rumba michangani aaaaaa rumba michanganiii" Hivi hakuwa mwanzilishi wa Cuban marimba kweli??? Wa moro. Jina wanalibana sababu ni sawa na wale alosema baba J. kuwa walifukuzwa. Weka singular badala ya wingi.
Juma nani mbona sikuelewi?
 
  • Jamani external service na Legandary Edda Sanga, ilikuwa burudani

  • Watangazaji wa kike na sauti murua, thank God wengine bado wapo: Alacia Maneno, Christine Chokunegela, Betty Chalamila n.k

  • Julius Nyaisanga (RIP) wakati anaripoti sherehe mbalimbali utapenda
  • Misakato
  • Mazungumzo baada ya habari
 
Wawapeleke wacheza pool sasa tuone au wale wa mbukwenyi kwenye mataa.
Wacheza pool walichanganyikiwa JPM alipowabia wakuu wa Mikoa wahakikishe pool hazichezwi mchana.
 
Back
Top Bottom