Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Mchezo wa radio wenye maadili ya kutosha saa 2:30 usiku kama sikosei hivi!
TWENDE NA WAKATI mixer ka mdundo fulani hivi nduuu! nduuuu! nduuu!
nilikuwa skai mbali na radio ya mkuliwa
NATIONAL!
Kha!kumbe ulifunguka masikio mapema ehe?
Maana mpaka akina mzee mundu unawajua na jangala unaqajua?au umehadithiwa nn?
 
Kwa upande wa vipindi nilipenda sana Chaguo la msikilizaji j3 hadi ij sa8 mchana, mama na mwana j1 sa9 alasiri, Salaam za wagonjwa j2 sa4 asubuhi, Igizo la Twende na wakati wakiwemo kina Kidawa j4 sa3 usiku.

sasa hapo kwenye chaguo la msikilizaj ndo umegonga kwenye moyo
sasa kipindi hicho mi nilikuwa mdogo darasani tunaingia saa nane kamili
so nilikuwa tagea nikiumwa tu! Saa nane nakuwa mzima ua waalimu utasikiwa wameenda wizarani kikao/kuchukua mishaara! Bas naaribu kanda za dingi kwa kurekodi! Alafu wimbo wa Awilo Longomba haukos kweny hicho kipind
eei! Eei! Eeeei! Aaaaawilo longombaa! Wee tu!
 
Kha!kumbe ulifunguka masikio mapema ehe?
Maana mpaka akina mzee mundu unawajua na jangala unaqajua?au umehadithiwa nn?

we umesema me kitoto! Sasa nina miaka 23! Sasa unataka kuniambia humu jf watoto wa 90 hadi 95???? Tena kweny jukwaa kubwa hasa la MMU!

Sio nimehadithiwa nilikuwa nasikiliza mwenyewe nailikuwa nafuatilia ajabu nilikuwa skos mzee! Levo zngine hizi unafkir watoto wenu sasa hivi hata taarifa ya habari ya kuangalia tu kweny tv
hawataki wanazima tv wanataka wakina kanumba! Wakati sis hata za kuchungulia dirishan kwa jiran zilikuwa dili!!
 
sasa hapo kwenye chaguo la msikilizaj ndo umegonga kwenye moyo
sasa kipindi hicho mi nilikuwa mdogo darasani tunaingia saa nane kamili
so nilikuwa tagea nikiumwa tu! Saa nane nakuwa mzima ua waalimu utasikiwa wameenda wizarani kikao/kuchukua mishaara! Bas naaribu kanda za dingi kwa kurekodi! Alafu wimbo wa Awilo Longomba haukos kweny hicho kipind
eei! Eei! Eeeei! Aaaaawilo longombaa! Wee tu!

"Hujambo msikilizaji, ndani ya studio uko nami Malima Ndelema, kipindi ni chaguo la msikilizaji...."
Ni baadhi ya maneno ya huyo mtangazaji ambaye kwa sasa sijui yuko wapi. Baada ya kipindi hiki kufa pale rtd nikahamia Radio one nikawa nasikiliza kipindi kama hicho siku ya j1 sa7 mchana hadi sa9 alasiri chini ya mwanadada mahiri Rose Chitara aka RC COMPUTER. Moja ya mbwembwe zake ni kama hivi..
"2-7-0-0-5-8-8, nipigie kisha chagua kibao unachotaka kisha ntakiachia hewani, kabla ya kuruhusu simu nitaanza na kuponi ya CHIDCHID CHITENDA yeye ameomba wimbo wa.... umburudishe CHESKO MZEE WA MATUNDA akiwa.."
 
Mama na Mwana...

Halaf kipindi hiki kiliendeshwa na mwanamama mmoja mwenye sauti ya malezi kwa watoto sijui alikua anaitwa nani? Alikua akisimulia hadithi za kuvutia, alikua akianza na maneno, "PAUKWA..., hapo zamani za kale palikua na..."
 
Namkumbuka mzee Dominic Chilambo ,RIP huyu alikua anatangaza kipindi cha Ngoma za asili ,

Namkumbuka Julius Nyaisanga na kipindi chake Cha Muziki kilikua kinaanza saa 4 hivi
 
Namkumbuka mzee Dominic Chilambo ,RIP huyu alikua anatangaza kipindi cha Ngoma za asili ,

Namkumbuka Julius Nyaisanga na kipindi chake Cha Muziki kilikua kinaanza saa 4 hivi

Hivi kumbe Nyaisanga (babu wa kimanzichana) alishawahi kua rtd!
 
nakumbuka yale magoma ya marehemu mzee morice nyunyusa......
 
Mama na mwana enzi hizo bila kusahau chei chei shangazi na maneno hayo!kweli RTD ni kiboko
 
Mama na mwana enzi hizo bila kusahau chei chei shangazi na maneno hayo!kweli RTD ni kiboko

Kumbe nawe ulikuwepo enzi za cheichei shangazi studio akiwemo mwanamama ELISIA ISABURA. Aisee kitambo sana.
 
Mnaikumbuka 'mikingamo', 'club raha leo show' pia mchezo wa kuigiza wa kiinua mgongo ukichezwa na mzee jangala kikidhaminiwa na dar brew watengenezaji wa pombe safi kibuku (enzi hizo lkn)
 
Pwagu na Pwaguzi ilikuwa kiboko!
Vile vile mazungumzo baada ya habari hasa wakati wa vita vya Kagera! Msomaji nafikiri alikuwa Abdul Ngalawa!
 
Mnaikumbuka 'mikingamo', 'club raha leo show' pia mchezo wa kuigiza wa kiinua mgongo ukichezwa na mzee jangala kikidhaminiwa na dar brew watengenezaji wa pombe safi kibuku (enzi hizo lkn)

Duh!umenikumbusha enzi za jangala na Mzee mundu na kulikuwa na mchezo wa kina Mzee bomu na Mama myaone!enzi zile ilikuwa raha
 
MISAKATO bwana. Leo Ijumaa usiku kuanzia saa 4.15 usiku. Tulikuwa hatulali maana zilikuwa ni nyimbo mpya za bendi moja.
 
Kwa sisi wa zamani kidogo kulikua na external service iliyokua na kipindi "from me to you" (siku hizi mngeandika 4m me 2 U, lol!) hiki kilikua jumapili. Unakaa na redio yako na tepu tayari kurekodi nyimbo.
Halafu kwenye idhaa ya biashara kulikua na kipindi cha national panasonic, sikumbuki jina lake lakini dj wake alikua uncle J
halafu kwa ngoma za asilii kulikua na kipindi cha M Katembo
kwenye burudani ya usanii kulikua na pwagu na pwaguzi.
Baada ya taarifa ya habari kulikua na "mazungumzo baada ya habari"
baadae sana kulikua na mikingamo, kipindi cha kutoa majungu hewani
 
Back
Top Bottom