Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Dah, kitambo sana enzi za kina Hendrick Maiko Libuda, lakini nasahau jina la yule
Mtangazaji alitangaza mechi ya simba na Atletico sports Aviacao ya Angola ambayo
ilikuwa na wachezaji wakali kama Kanka wemba, Abilio Amanali, Gito, Libenge, Bravo
Yanda, Nero sijui nelo n.k


Wakati huo simba ilikuwa ni kina Abdul Mashine, Mohammed Mwameja, Hussein Masha, Yamadhani Leny
Damian Kimti, Mteze John Rungu, Malota Soma, Edward Chumila n.k


Umenifanya nivikumbuke vipindi maarufu kama HISIA NA MUZIKI, MAHOKA, PWAGU NA PWAGUZI
PITIO LA KITABU NA SAIF D KIANGO N.K

Debora mwenda sitamsahau kamwe kwa kukifanya kipindi cha mama na Mwana
kipendwe hata na watu wazima......... acha Bwana hadithi tamu kama Ua Jekundu,
Binti chura, Kibibi jitu n.k Enzi zimepita sasa watoto wanacheza viduku.

Pia ninawakumbuka waigizaji kama Mzee MUNDU, Mshamu, Matuga n.k

lidenge mkuu umemsahau wa aviacao
 
Salama Mfamao RIP
Aloysia Isabula
Aloysia Maneno
Peter Makorongo
Suleiman Kumchaya
Juma Ngondae RIP
Mshindo Mkeyenge
Abdallah Mlawa
Siwatu Luanda RIP
Salim Mbonde
Omary Masoud RIP
Pascal Mayalla
Adam Mwaibabile
etc....
 
Kwa vijana wa zamani. Unakumbuka nini unapopitia majina haya? Je, yuko wapi kwa sasa? Unamkumbuka katika kipindi kipi kilichokufurahisha?

1. Bujaga Izengo Kadago
2. Debora Mwenda
3. Sarah Dumba
4. Julius Nyaisanga
5. Charles Hillary
6. Eshe Mhidini
7. Frolian Kaiza
8. Tumbo Risasi
9. David Wakati
10. Halima Kihemba
11. Betty Mkwasa
12. January Costantine
13. Lando Mabula
14. Ben kiko
15. Abubakary Lyongo
16. Sued Mwinyi
17. Abisai Stevin
18. Nswima Ernest
19. Malima Ndelema
20. Richard Leo
21. Ahmed Jongo
22. Christina Chokunogela (Christine Chakunegela)
23. Shaban Kissu
24. Jacob Tesha
25. Sallim Mbonde
26. Sekion Kitojo
27. Omary Jongo
28. Abdalla Majura

Omary Jongo na Hilary, uwanja wa taifa!
 
Umenikumbusha mbali sana kaka wakati huo sh. mia inaitwa nyanga. Anyways mnayakumbuka na matangazo ya biashara na vipindi yaliyokuwa yanarushwa RTD kipindi hicho?

1. TANGAZO LA PEDI ZA JESI:
Wanawake kuweni na furahaaa, furahaaa, wakati wote popote na jesi,
Jesi, pedi mpya za kike za njano, ni nyororo raha kuvaa wakati wote......

2. TANGAZO LA DAWANOL
Mgongo wangu waniuma maumivu teleee, dawa ya maumivu dawa yenye nguvu dawa ni dawanol

3. TANGAZO LA SABUNI YA MSHINDI. n.k

MATANGAZO YA VIPINDI:

1. MASHIRIKA YA TAIFA: Mashirika ya taifa Tanzania yapo Mengi... na matangazo mengine mengi. Huwa natamani sana siku moja niende pale RTD nikaombe nipewe hayo matangazo niwe nayasikiliza tu mwenyewe ili niwe nakumbuka utotoni...DA INANIKUMBUSHA MBALI SANA

Unakumbuka tangazo la baiskeli za shangshein? ".......Anashangiliwa na umati wa watu....."
 
kwenye mwaka 2010 Anko J aljkuwa anatangaza Abood tv. Morogoro. kwasasa sipo moro so sijajua kama bado yupo hapo au tena amehama
 
Tangazo lingine ni WATOTO HAWA BWANA,....... KULA WANAKULA, KUVAA WANAVAA LAKINI MMMMMMMMHHHHHH
Tangazo la sabuni MSHINDI. SABUNI KOMOA. NA MBUNI. BILA KULISAHAU TANGAZO LA KIBUKU OYEE, KIBUKU HONGERA HONGERA
 
Tangazo lingine ni WATOTO HAWA BWANA,....... KULA WANAKULA, KUVAA WANAVAA LAKINI MMMMMMMMHHHHHH
Tangazo la sabuni MSHINDI. SABUNI KOMOA. NA MBUNI. BILA KULISAHAU TANGAZO LA KIBUKU OYEE, KIBUKU HONGERA HONGERA

.....na matangazo ya dawa
 
masoooouuud masoouud wakuu msisahau na Tido mhando
Kama kumbukumbu zangu ziko sahihi, Datsan Tido Mhando alitangaza kwa ufundi mkubwa sana game ya fainali ya Kombe la Afrika mwaka 92 kati ya Ghana na Ivory Coast. Ilikuwa fainali ya aina yake kwani dakika 120 hazikutoa mshindi na hadi penati 11/11 hakuna mshindi. Ni fainali ya kihistoria sana katika kombe la Afrika kwa kweli na ilinibidi nitafute sababu za kuchelewa kurejea shule(Boarding) ili kumalizia fainal hizi mwezi Januari (kama niko sahihi). Ilikuwa kuliko TV; Anakwenda kupiga Aka, kama utakumbuka vizuri ndugu msikilizaji huyu ndiye aliyepiga penati ya kwanza ya Ivory Coast, hebu tusikilize-Gooooooooooooooooooo...Sasa ni zamu ya Ghana, anakosaaaa!!!!!!! Ivory Coast wanatawazwa mabingwa wapya wa Afrika ikiwa ni kwa mara ya kwanza.
 
Umemsahau EZEKIEL MALONGO mpira upo katikati ya uwanja yy ansema gooooooooooooooolkick

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Tangazo la "ubwabwa huu, unanikumbusha mbali sana masikini, mawka 47..."

Daa! hivi yule mama aliyeigiza na mzee Kipara hilo tangazo alikuwa anaitwa nani? "si useme tu CRDB wamekuja kuchukua lory lao"
 
Tangazo la kiwi la Hebu jitokeeze simamaaa imaraaa mbele ya watuuuu!! Hapa sasa inafata Rap! Nakwenda kupata mng'aro wa kipekee na ni mng'aro wa ajabuu niko njiani nimeupata hakika humeremetaa, humeremeta kwa kiwii na hung'ara kwa kiwi! Na tangazo la revola lile la Revolaaaa Revolaaa revolaaaa kwa sauti za kivampire lishawahi kunishtua usingizini nilikuwa naota nilitoka mbio nikidhani wachawi kumbe tangazo la revola kwa kweli sijasahau hiyo siku hadi leo mdau unanikumbusha RTD
 
Enzi hizo mpira kina Abuubakar Lyongo na Charles Hilary na wadhamini sabuni ya komoa na wimbo wao wa nipeni maji nifue eheee na sabuni ya komoaaa ahhhh, ahahaaaa ahaaa ahahaaaa na Abood na mwimbo wao wa Abood bus service Abood bus service ulioimbwa na Varda Arts ile bendi ya wahindi sijui hata if its still existing na Dawanol na wimbo wao wa ukionaaa maumivuuu maumivu teleee dawa ya maumivu dawa yenye nguvu dawa ni dawanooool. Duh looong tym thanx mdau kutukumbusha
 
Watangazaji wa zamani saana ni kama. NASSOR NSEKELI, HAWA MALIPULA. MOHAMED NGAYONGA, RASHID SEIF NASSOR, MSHINDO MKEYENGE, JUMA NGONDAE NA WAKATI HUO FUNDI MITAMBO NI NOEL NAMALOWE, JACOB AYIMBA NK
 
  • ATC Hewaniiiiiiiiiii!
  • NASACOoooooo!
  • Utumie Kibukuu, ndio pombe bora! Tumia,kibuku.......Hapo mnasubiri vitu vya mzee Jangara!
  • Malima Ndelema;Mkoa kwa Mkoa mida ya (saa nne au tano asubuhi) nilikuwa natoroka shule ili nisikilize hiki kipindi na kwa kweli kilichangia sana kuiweza jiografia na historia kwa shule za msingi!
  • Hii ni Kwaresma (mida ya saa nne usiku).
 
1. Bujaga Izengo Kadago-Michezo lakini alikuwa anakera habari nzuri anaweka mwisho; pia matukio
2. Debora Mwenda-Mama na mwana
3. Sarah Dumba-majira
4. Julius Nyaisanga-DJ Show, sjui pia na kile Starehe na BP
5. Charles Hillary-
6. Eshe Mhidini-Chaguo la msikilizaji
7. Frolian Kaiza-Pia habari za uchambuzi wa nje(not sure)
8. Tumbo Risasi-Huyu sjui Ruvuma vile
9. David Wakati-Mtalaam huyu
10. Halima Kihemba-Morogoro
11. Betty Mkwasa
12. January Costantine
13. Lando Mabula-Chaguo la msikilizaji
14. Ben kiko-Kanda ya Kati/Dodoma
15. Abubakary Lyongo-Michezo sjui na burudan not sure
16. Sued Mwinyi-Nini palee, Penaaaaat, hapana, hapana ni Kona
17. Abisai Stevin-Huyu sjui ni Rukwa au Ruvuma
18. Nswima Ernest-Huyu Mbeya na Rukwa; maarufu Nswima Eeeerrrrnest
19. Malima Ndelema-Mkoa kwa Mkoa, masihara meeeengi
20. Richard Leo-Kanda ziwa/Kigoma
21. Ahmed Jongo-Goooooooooooooooooooooooh, lalaalalala, gooooooooooooh; nini, Goal Kick!
22. Christina Chokunogela-Habari ila hovyo
23. Shaban KIssu-Mazungumzo baada ya Habari na mwenziwe Angaliani Mpendu
24. Jacob Tesha-Habari murua, na External Service
25. Sallim Mbonde-Majira na Matukio
26. Sekion Kitojo-Taarifa ya Habari na Habari za matukio ya nje kama vita ya Kuwait na Iraq
27. Omary Jongo.

Ongeza na Hawa:
28. Fauzia T. Ismail Aboud-Taarifa ya Habari
29. Dominick Chilambo-kwa wana T.P. lindanda
30. Siwatu Luanda
31. Halima Mchuka
32. Titus Philipo
33. Yusuf Omar Chunda-Zanzibar huyu
34. Sjui ni nani alikuwa anaendesha kile cha Club raha leo show; Full uzalendo kipindi hicho,
Haya bwana wacha wajuzi waje wakuchambulie hapa. Ila ilikuwa inapendeza sana, as if uzalendo ulikuwapo kidogo
Yuko radio abood. Morogoro
 
Back
Top Bottom