Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

kile kipindi cha mama na mwana kilikuwa kikitangazwa na nani vile? Nalog off
 
Sara Dumba, Jacob Tesha, Seleman Hega, Danstan Tido Mhando, Seleman Kumchaya, Peter Makorongo, Charles Hillary, Omary Jongo, Ahmed Jongo, Sango Kipozi, Masoud Masoud, Aloisia Isabula,Aloisia Maneno, Debora Mwenda, Mikidadi Mahamoud, Juma Nkamia, Swedi Mwinyi, Ahmed Kipozi, Dominic Chilambo, Bati Kombwa, Nadhir Mayoka, Abdallah Majura, Michael Katembo,Abisae Steven, Abdallah Mlawa,Nassoro Nsekeli,Bujaga Izengo Kadago,David Wakati,Khalid Ponera,Christina Chokunogela,Ahmed Kipozi,Siwatu Luwanda,Salim Seif Nkamba,Salama Mfamao,Bartholomew `Bati’ Kombwa
Ahmed Jongo,Dominic Chilambo,ngalieni Mpendu,Sekioni Kitojo,Chisunga Steven
Edda Sanga,Mikidadi Mahmoud,Mshindo Mkeyenge....................Wengine ongezeeni

Wapi Tumbo Risasi wa kipindi cha majira!!
 
Mmenikumbusha mbali sana! khaaaaaaa! Mipira ikiwa inachezwa usiku!!
 
Wanabodi,

Baada ya Kifo cha Mtangazaji Nguli nchini, Uncle J. Nyaisanga, naomba kuchukua fursa hii, kufanya reflection ndogo ya Watangazaji wa RTD waliotangulia mbele ya haki. Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.

Naomba nisizungumzie kulitowatoa duniani, wala hatima ya familia zao walizoziacha huku nyuma maana sio tuu nitazidi kuogopa, bali pia tutazidi kuumia!. Just imagine, kijitaasisi kidogo kama RTD chenye ofisi yake pale BH-Pugu Road kupoteza idadi kubwa hivi ya watumishi wake (tena hawa ninaowataja ni Watangazaji tuu!, achilia watumishi wengine!. Sii bure!, ila lazima tukubali ni kazi ya Mungu, na kazi ya Mungu haina makosa!.

Hii list sio walikufa lini ni random, nikiwakumbuka wengine nitawaongeza!
Tukianzia na

  1. David Wakati
  2. Abdul Masudi (Jawewa)
  3. Eli Mbotto
  4. Stephen Mlatie
  5. Siwatu Luanda
  6. Salama Mfamao
  7. Salim Seif Nkamba (Mjomba)
  8. Michael Katembo
  9. Nelly Kidella
  10. Halima Mchuka,
  11. Omar Jongo
  12. Tumboi Tamimu Risasi
  13. Mohamed Ng'ombo
  14. Abisai Stephen (Uronu)
  15. Stephen Lymo.
  16. Nadhir Mayoka
  17. Juma Ngodae
  18. Rukia Machumu
  19. Karim Besta
  20. Henrick Michael Libuda
  21. Idrissa Sadalah
  22. Bati Kombwa
  23. Iddi Rashid Mchatta
  24. Dominic Chilambo
  25. Hassan Mkumba
  26. Khadija Said
  27. Ally Saleh
  28. Kwegier Munthali
  29. Leonard Mtawa
  30. Khalid Ponera
  31. Ben Kiko
  32. Restuta Bukholi
  33. Sarah Dumba

Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.
Pia sio vibaya kuwaulizia wale watangazaji wa siku nyingi ambao hatujui walipo, ili kama nao wametangulia tuyaingize majina yao.

RIP All the Fallen Heroes wa Tasnia ya Utangazaji Tanzania!,

Pascal.

NB. Pia unaweza Kupata Taarifa za Baadhi ya Watangazi waliotutoka hapa.

Tribute to David Wakati, Kikwete, Mengi, Nchimbi na ...

Tribute to David Wakati: His Legacy Will Live On!
Mzee David Wakati Katutoka Leo Translate this page



Tribute To Uncle J. Nyaisanga: Jee Unamkumbuka kwa Lipi?!. Kuagwa ...

TBC haikumtendea haki marehemu David Wakati - Jamii Forums


  1. Tribute to Halima Mchuka: Alikuwa Mtu wa Watu!
    Halima Mchuka hatunae duniani - Page 2 - JamiiForums
    Hii RTD unaikumbuka? - JamiiForums
    Msiba wa halima mchuka hauna nafasi tbc - JamiiForums
    Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa RTD - Jamii Forums
    Topic: Nimewakumbuka hawa pia..................zamani... - Jamii ...


    Mtangazaji Maarufu wa RTD Amefariki Dunia Asubuhi Hii ..
 
Ben Kiko, sijui yuko wapi huyu jamani
Alesia maneno na Alesia Isabula nadhani bado wapo TBC taifa
Watangazaji wa zamani walikuwa watangazaji kweli
Chezea Michael Katembo na Kipindi cha mkoa kwa mkoa
Nilikuwa nampenda Siwatu Luanda(RIP)nakumbuka alifariki nikiwa drs la tano miaka hiyo
 
Chilambo Dominic, jamaa alikuwa anaipenda FC Pamba yaani alikuwa na passion mpaka inatia raha akitangaza mechi za Pamba
RIP

Huyu mzee alikuwa ni mnazi mkubwa wa soka la Tanzania wakati huo wa Ligi daraja la kwanza...

Kwa waliopata kumsikiliza akitangaza mpira bila shaka watakubaliana nami alikuwa anavutia kumsikiliza...

Na kwa wakati huo alikuwa akishirikiana vyema na watu kama Omary Jongo, Swedy Mwinyi na wengineo...
 
Duh mmenikumbusha mbali sana.nilikuwa nakipenda sana tena sana kipindi cha mama na mwana.sikumbuki jina la mtangazaji ebu nikumbusheni wajf.nilikuwa sikosi kipindi .yaani nakosa raha nisipokisikiliza .hivi yupo yule mtanganzaji?? Pia kile kipindi cha zilipendwa kila jumapili nilikipenda sana
 
Ni hoja nzuri,
Lakini wenye tasnia wenyewe wamefanya nini? nina maana wana habari wenyewe , je wanafikirin atatoka mtu nje awafanyie kumbukumbu bali ni wao wenyewe kuonesha njia?
David Wakati alikuwa mwisho!!!- akitangaza utasikilza tu
mpirani- Sisi Moja wao... ( Ahmed Jongo!!) -- nakumbuka siku Peter Tino alipowafunga wazambia na kutupela Nigeria.... mnakumbuka? WACHA KABISA!!
Salum Mbonde!!
Then Uncle J Nyaisanga
wanahabari wa leo wasikilize hata matamshi ya maneno. walijua lugh ya kiswahili fasaha! Ahmed Kipozi Msimsahau na enzi ya Mikingamo... ( tuambie nani yuko wapai anafanya nini..... Mdudu rushwa!!) yote yamebakia yakirindima masikioni mwetu ,.... YEAH Pascal you have apoint
Swali: Tuambie.. nani aanze, yuko wapi na anafanya nini ili kuenzi wanahabari wa nchi hiiii?)
 
Kaka Pascal Mayalla naomba ututambulishe wengine kupitia picha hizi:

Watangazaji-wa-Zamani-RTD.jpg
 
Last edited by a moderator:
nilikuwa nakipenda sana tena sana kipindi cha mama na mwana.sikumbuki jina la mtangazaji ebu nikumbusheni wajf.nilikuwa sikosi kipindi .yaani nakosa raha nisipokisikiliza .hivi yupo yule mtanganzaji??

Mama Deborah Mwenda na wakati mwingine Aloycea Maneno
 
Kuna wengine walipata ajali na kufariki (nafikiri gari iligongwa na treni hapo dsm miaka ya 70's) mmoja wapo alijulikana kwa jina la Ally Saheh. Kipindi hicho ilisemekana Bandarini na TBC kulikuwa na ushirikina wa kupitiliza!
 
Mama Debora Mwenda
Unakumbuka zile hadithi? jumamosi ikifika saa nane mchana watoto wote tuko kwenye radio, na mashuleni tulikuwa na club za mama na mwana

Duh mmenikumbusha mbali sana.nilikuwa nakipenda sana tena sana kipindi cha mama na mwana.sikumbuki jina la mtangazaji ebu nikumbusheni wajf.nilikuwa sikosi kipindi .yaani nakosa raha nisipokisikiliza .hivi yupo yule mtanganzaji?? Pia kile kipindi cha zilipendwa kila jumapili nilikipenda sana
 
Paschal Mayala tambulisha watangazaji hapo juu lakini pia naomba utafute picha ya Siwatu Luanda jamani I real love this mama jamani, alikuwaga na sauti tamu sana akiwa anatangaza utadhani ana mafua
 
David+Wakati.bmp


Mzee David Wakati enzi za ujana wake.

Pamoja na vipindi vingine alikuwa maarufu zaidi kwenye kipindi cha Nipe habari.
 
Back
Top Bottom