Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Tujikumbushe watangazaji wa zamani wa Redio na TV

Wanabodi,

Baada ya Kifo cha Mtangazaji Nguli nchini, Uncle J. Nyaisanga, naomba kuchukua fursa hii, kufanya reflection ndogo ya Watangazaji wa RTD waliotangulia mbele ya haki. Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.

Naomba nisizungumzie kulitowatoa duniani, wala hatima ya familia zao walizoziacha huku nyuma maana sio tuu nitazidi kuogopa, bali pia tutazidi kuumia!. Just imagine, kijitaasisi kidogo kama RTD chenye ofisi yake pale BH-Pugu Road kupoteza idadi kubwa hivi ya watumishi wake (tena hawa ninaowataja ni Watangazaji tuu!, achilia watumishi wengine!. Sii bure!, ila lazima tukubali ni kazi ya Mungu, na kazi ya Mungu haina makosa!.

Hii list sio walikufa lini ni random, nikiwakumbuka wengine nitawaongeza!
Tukianzia na

  1. David Wakati
  2. Abdul Masudi (Jawewa)
  3. Eli Mbotto
  4. Stephen Mlatie
  5. Siwatu Luanda
  6. Salama Mfamao
  7. Salim Seif Nkamba (Mjomba)
  8. Michael Katembo
  9. Nelly Kidella
  10. Halima Mchuka,
  11. Omar Jongo
  12. Tumboi Tamimu Risasi
  13. Mohamed Ng'ombo
  14. Abisai Stephen (Uronu)
  15. Stephen Lymo.
  16. Nadhir Mayoka
  17. Juma Ngodae
  18. Rukia Machumu
  19. Karim Besta
  20. Henrick Michael Libuda
  21. Idrissa Sadalah
  22. Bati Kombwa
  23. Iddi Rashid Mchatta
  24. Dominic Chilambo

Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.
Pia sio vibaya kuwaulizia wale watangazaji wa siku nyingi ambao hatujui walipo, ili kama nao wametangulia tuyaingize majina yao.

RIP All the Fallen Heroes wa Tasnia ya Utangazaji Tanzania!,

Pascal.
bro.pascal ABDALLAH MLAWA tunae ?
 
Mkuu Capt Tamar, japo umechanganya kidogo majina, mimi ndiye mwenyewe haswa!, verified, nilikuwa mtangazaji wa vipindi vya burudani kwenye redio, nilipoingia kwenye TV nilijikita kwenyue siasa, na huko ndiko ninaelekeza nguvu zangu zote kulisadia taifa langu!. Amini nakuambia, kwenye sisa ndiko utapatana sana na mimi kama unapenda siasa za ukweli, na sio hizi za uwongo, unafiki, fitna, majungu na ushabiki wa watu/vyama bila substance behind!. Najipanga kutoa somo la siasa za kweli!. Soon!.
Pascal.

Thanks man! But until then,we still have the mountains to climb,mkuu pascal unapozungumzia siasa za UNAFIKI unakuwa umesimama kwenye jukwaa lipi hasa?kwa sababu kwa Tanzania hii na siasa zake,ukiondoa unafiki utakuwa umeiondoa siasa yenyewe,so is news industry,so is religious institutions,SO IS TANZANIANS,una mengi ya kutufunda brother,usipokuwa----ukiamua kuwa mkweli, hii mada ni tamu mno,japo ina huzunu ndani yake!!tusiipotoe.
 
Last edited by a moderator:
We Pascal ina maana sie mafundi uwa hatukubukwi. Au unataka nife kwanza ndo mtatukumbuka. Umewasahau mafudi kama vile Domitla Urassa, Juma Bungara. Bundala, Mzee Juma Sereka, Konsalva Mwereke nk. Ndio hao waliokufanya usikike na upate umaarufu kwa kukuandalia lineup ya mziki na kurekebisha sauti yako wakati wako pale studio Red na Studio Blue. Bila hao ngoma za ZIPOMPAPOMBA husingetamba nazo wewe
bila ya kuwasahau ALLY SAID TUNKU NA NOEL MALOE
 
NAMJUA ABDU MASUDI na David wakati TUU KWA SURA LAKINI WENGINE SIWAJUI HATA MMOJA KWA SURA hata nikikutana nao new York au Tel Aviv. halafu miaka ya mwanzononi ya 70's, kulikuwa na kipindi cha mbiu za mikoa na mazungumzo baada ya habari. Vipindi hivi vilijaa maneno ya kudanganya umma kuliko kitu chochote duniani. Vilijaa matusi kwa mabepari na uongo wa maendeleo vijijini. Utasikia wakulima wa pamba geita wamepata bilion nane za mauzo ya pamba! au wakulima wa miwato kwimba wamepata milion arobaini ! au wakulima wa pareto njombe wamepata bilion tisini! ukigawana pesa hizo kwa idadi ya kila mmoja utakuta kila mkulima kapata shilingi alfu nane tuu!

nakumbuka mazungumzo baada ya habari yaliyokuwa yanasema,: "weweee, mitaji haramu ya kujijengea mali umeipata wapi weweeee!" au yale ya " baba baba, unafanya nini hapo ulipo"

hawa watangazaji wa iliyokuwa RTD nawapa hongera ya kupotosha umma kuliko kuelimisha watu! Ujamaa ulikuwa ni sumu kwa umma kuliko hata ukimwi!
ABDUL OMAR MASUDI alikua mahiri ktk kipindi cha michezo cha saa 2 kasorobo usiku
 
Wanabodi,
Baada ya Kifo cha Mtangazaji Nguli nchini, Uncle J. Nyaisanga, naomba kuchukua fursa hii, kufanya reflection ndogo ya Watangazaji wa RTD waliotangulia mbele ya haki. Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.

Naomba nisizungumzie kulitowatoa duniani, wala hatima ya familia zao walizoziacha huku nyuma maana sio tuu nitazidi kuogopa, bali pia tutazidi kuumia!. Just imagine, kijitaasisi kidogo kama RTD chenye ofisi yake pale BH-Pugu Road kupoteza idadi kubwa hivi ya watumishi wake (tena hawa ninaowataja ni Watangazaji tuu!, achilia watumishi wengine!. Sii bure!, ila lazima tukubali ni kazi ya Mungu, na kazi ya Mungu haina makosa!.

...............Huyu Mungu TUNAMSINGIZIAGA SANA. Nadhani muda mwingi huwa anacheka tu! We Paschal shukuru umeondoka pale bado mdogo. Ungemkuta alieanzisha haya maafa labda na wewe usingekuwepo leo. Mtoto wa kizaramo kaifyeka RTD si mchezo. Na hii mifano imo maofisi mengi ya serikali, mashirika ya umma na hata binafsi. Kitendo cha kuzungukana na kung'ang'ania mtu mmoja. Kinatekeza sana watu hapa Tanzania.

Nahisi una maanisha Salama Mfamao? Nimepitia thread yote hakuna mahala mtu kamtaja kama kumbukumbu. Mungu amlaze mahala pema peponi
 
Mkuu kwelitupu, kiukweli ukweli ni kitu kigumu, ila mimi ni mkweli!. Nilipojiunga, nilielezwa kuhusu uchawi!, bahati mbaya siamini kuwa uchawi upo!. Kiukweli uchawi upo, ila ni kwa wanaoamini tuu kuwa uchawi upo!, kwa sisi tusioamini, kwetu uchawi haupo!.

Wala siamini sababu ya vifo ni uchawi, ila pia naomba kuutoa ukweli mchungu kuhusu RTD ya enzi hizo!.

Ulikuwa unajua saa tuu ya kuingia kazini, ya kutoka huijui!. Mimi nakumbuka siku nikiingia asubuhi, unafuatwa saa 9 usiku, unapaswa kutoka saa 6 mchana, ila ukitoka ndipo ueanze kuandaa vipindi vyako!, kunawakati unaingia saa 9 usiku, unatoka saa 6 usiku siku inayofuata!.

Tulipoanza kazi Mjomba (SS Mkamba), akatuhusia mkitaka salama hapa, hawa akinadada waangalieni tuu!, msiwasogelee kwa sababu macho yote yako kwao!. Mimi na Abou tukamhakikishia Mjomba kuwa hilo kweli haliwezekani, kwa sababu, hao "wadada" wenyewe tuliwaona wachovu tuu!.

Baada ya kupita miezi 6, kumbe watu mnaokuwa nao kila siku, mara wa kwanza kuanza "kuona" ni Abou!, tukasema kumbe ful;ani ni mzuri hivi!, huku na kule, "akafika mahali!", kufumba kufumbua, Abou kahamidshiwa Nachingwea!.
Huko hata hoteli kuku ni mpaka ulipie kabla ndipo upikiwe!.

Ikaja zamu yangu!, ilikuwa ni balaa!, Mwanzoni tulianzia vile vi gesti Buguruni!, mambo yalipokolea, gesti mbali!, ni kila mahali, kuanzia "washroom!', studio!, juu ya meza ya ofisi!, kwenye ngazi!, hadi Telefon room!.

Mwanzo mwanzo tulitumia!, tulipozoeana, hatukukumbuka tena!. Wengi wa watumishi wa RTD wenye watoto, baba zao wako hapo hapo!. Kuna wengine wetu tumesurvive kwa kudra tuu ya Mwenyeezi Mungu!, tatizo kubwa la watangazaji wa zamani ni kuponzwa na umaarufu!, kujifungia studio kwa masaa mengi na watu wale wale hadi kujikuta kwenye Zero Grazing!, Ukisikia mtangazaji wa kike kaolewa, ujue aliyependa ni huyo mtangazaji wa kike!, yaani ili uoe mtangazaji, lazima kwanza mtangazaji huyo ndio akupende wewe!, vinginevyo! ukipenda wewe! jua.. ( japo nakiri sio wote).

Hii "zero graizing!" could be the main cause!.

Ila pia naomba kuwahakikishieni, pamoja na yote hayo, chanzo cha vifo sio UKIMWI!, kwa sababu Ukimwi ni "ukosefu tuu wa kinga mwilini!, yaani mtu hawezi kufa kwa "ukimwi" kwa kasabu ukimwi sio ugonjwa!, ila ukishakosa hiyo kinga mwilini, mwili wako unakuwa dhaifu na kuwa rahisi kushikwa na ugonjwa ambao ndio hupelekea kifo!.

Pasco.

Kimsingi unakubaliana na hoja ya Mwanjelwa? Ebu tuelezee, huyu Salama Mfamao alikuwa kama yeye, uhusiano na wafanyakazi kikazi na mvuto? Tunashukuru sana kwa ufafanuzi wa issues amabazo kila mmoja anapenda jua
 
Wanabodi,
Baada ya Kifo cha Mtangazaji Nguli nchini, Uncle J. Nyaisanga, naomba kuchukua fursa hii, kufanya reflection ndogo ya Watangazaji wa RTD waliotangulia mbele ya haki. Jee unawakumbuka?, unakumbuka vipindi vyao?!, unawakumbuka kwa lipi?!.

Naomba nisizungumzie kulitowatoa duniani, wala hatima ya familia zao walizoziacha huku nyuma maana sio tuu nitazidi kuogopa, bali pia tutazidi kuumia!. Just imagine, kijitaasisi kidogo kama RTD chenye ofisi yake pale BH-Pugu Road kupoteza idadi kubwa hivi ya watumishi wake (tena hawa ninaowataja ni Watangazaji tuu!, achilia watumishi wengine!. Sii bure!, ila lazima tukubali ni kazi ya Mungu, na kazi ya Mungu haina makosa!.

...............Huyu Mungu TUNAMSINGIZIAGA SANA. Nadhani muda mwingi huwa anacheka tu! We Paschal shukuru umeondoka pale bado mdogo. Ungemkuta alieanzisha haya maafa labda na wewe usingekuwepo leo. Mtoto wa kizaramo kaifyeka RTD si mchezo. Na hii mifano imo maofisi mengi ya serikali, mashirika ya umma na hata binafsi. Kitendo cha kuzungukana na kung'ang'ania mtu mmoja. Kinatekeza sana watu hapa Tanzania.

Mkuu hapa umenikuna kweli kweli..nilipoingia RTD kwa kipindi hiko kifupi kweli nilishudia mengi..namshukuru pia mwenyezi mungu kwa kunipa akili ya kukimbia ughaibuni na kuiacha hio kazi..akina Pascal na Aboubakar liongo nilipishana nao kidogo katika kujiunga rtd wao walinitangulia kidogo...kulikua na kupokezana sana hapo na nafikiri hilo ndo lilileta hilo janga hapo rtd....nakumbuka room ya kina Uncle J,alikuwepo Charlz Hillary ,Salama Mfamao.RIP na Siwatu Luanda hao walikaa karibu karibu...na wengine wengi tuu lakini sasa naona aliebaki mzima ni mzee wa macharanga ila wengine wote wametangulia mbele za haki inasadikika ni hapo tunapopendaga ndio kiini, huwezi amini watu tulikua tunapokezana vijiti ni balaa.
 
Mkuu Capt Tamar, japo umechanganya kidogo majina, mimi ndiye mwenyewe haswa!, verified, nilikuwa mtangazaji wa vipindi vya burudani kwenye redio, nilipoingia kwenye TV nilijikita kwenyue siasa, na huko ndiko ninaelekeza nguvu zangu zote kulisadia taifa langu!. Amini nakuambia, kwenye sisa ndiko utapatana sana na mimi kama unapenda siasa za ukweli, na sio hizi za uwongo, unafiki, fitna, majungu na ushabiki wa watu/vyama bila substance behind!. Najipanga kutoa somo la siasa za kweli!. Soon!.
Pascal.[/QUOT
Pascal utakua unanikumbuka sema ingawa sikukaa sana RTD..Malima Ndelema ndo alikua na yeye ananisaidia sana kunifundisha kazi na kunitafutia cassete za music,maana kwetu kumoja alipenda sana kuniita poti na yy ndo alinambiaga mama Yekin rip ananiwakia sana..kuna kipindi nilikuhisi unacharaza mkuu haahahaa but ndo hivyo nilikimbia zangu ughaibuni mapema sana hilo janga hata mm nisingeangalia lingenivaa mungu mkubwa.
 
Nahisi una maanisha Salama Mfamao? Nimepitia thread yote hakuna mahala mtu kamtaja kama kumbukumbu. Mungu amlaze mahala pema peponi
​Mkuu labda anaweza kuwa mtoto wa kizaramo mwingine kwa sababu Salama Mfamao wakati yupo na Pascal alikuwepo pia...hata Siwatu Luanda rip nafikiri alikua mtoto wa kizaramo maana alikua na umbo fulani hivi mwanaume yeyote lazima utamani na sauti yake sasa ilikua ni balaa!!alikua ni mwanamke wa haja...hayo mengine mmmmh sijui!
 
Kimsingi unakubaliana na hoja ya Mwanjelwa? Ebu tuelezee, huyu Salama Mfamao alikuwa kama yeye, uhusiano na wafanyakazi kikazi na mvuto? Tunashukuru sana kwa ufafanuzi wa issues amabazo kila mmoja anapenda jua
Mkuu Salama Mfamao rip alikua dada mpole aliepatana na kila mtu hivyo vingine sifahamu na kimvuto hakuwa anavutia vile alikua wa kawaida tu ,ila sasa best wake Siwatu Luanda rip huyo ndo alikua balaa alivutia sana kutokana na umbo lake ww acha tuu kwa mwanaume mzima ukipishana nae kwenye corridor lazima ugeuze kichwa kutaka kuangalia kulikoni mzigo mkubwa hivyo LOL..natumaini nimekujibu swali lako kabla ya Pascal hajaingia humu.
 
Hivi Deborah Mwenda ndie yule wa aliyerusha kipindi cha UA JEKUNDU? Nakumbuka wakati kipindi hicho kinarushwa hata watu wazima walikuwa wanajikusanya kusikiliza kipindi cha watoto!

Naam ndiye yeye mwenyewe mkuu, zilikuwepo hadithi nyngi tu mathalani Mbalamwezi Nyota Begani, Binti Chura, Ua Jekundu n.k
 
Nahisi una maanisha Salama Mfamao? Nimepitia thread yote hakuna mahala mtu kamtaja kama kumbukumbu. Mungu amlaze mahala pema peponi
Salama Nilimuita Dada, alitukaribisha hadi home kwake, kila nikiusikia wimbo wa Ousmane Bakayoko, namkumbuka Salama. Ni yeye aliutafsiri wimbo huo hewani tangu hapo kila ukipigwa namkumbuka!. Baada ya msiba, nilimtayarishia kipindi maalum na kumchezea wimbo wa "Salama" wa Marijan Rajabu!. Kiukweli alikuwa ni mwema sana na pia nilimwekea wimbo Vicky wa Vijana Jazz usemao "Nimeamini yanasosemwa na watu, wanaopendwa na wengi, hufa wangali vijana!".

Mkuu wewe ndo Yule Pascal Mayalla alikuwa mtangazaji kule DTV miaka ya 1990s?
 
Mkuu Capt Tamar, japo umechanganya kidogo majina, mimi ndiye mwenyewe haswa!, verified, nilikuwa mtangazaji wa vipindi vya burudani kwenye redio, nilipoingia kwenye TV nilijikita kwenyue siasa, na huko ndiko ninaelekeza nguvu zangu zote kulisadia taifa langu!. Amini nakuambia, kwenye sisa ndiko utapatana sana na mimi kama unapenda siasa za ukweli, na sio hizi za uwongo, unafiki, fitna, majungu na ushabiki wa watu/vyama bila substance behind!. Najipanga kutoa somo la siasa za kweli!. Soon!.
Pascal.[/QUOT
Pascal utakua unanikumbuka sema ingawa sikukaa sana RTD..Malima Ndelema ndo alikua na yeye ananisaidia sana kunifundisha kazi na kunitafutia cassete za music,maana kwetu kumoja alipenda sana kuniita poti na yy ndo alinambiaga mama Yekin rip ananiwakia sana..kuna kipindi nilikuhisi unacharaza mkuu haahahaa but ndo hivyo nilikimbia zangu ughaibuni mapema sana hilo janga hata mm nisingeangalia lingenivaa mungu mkubwa.
Mkuu Mauza uza, naomba nenda kanisome hapa Tribute to Halima Mchuka: Alikuwa Mtu wa Watu! - Jamii Forums
Mengine utajaza mwenyewe!.
Pascal.
 
Back
Top Bottom