Tujionee kwanza haya maajabu ya Kikokotoo kwa Watumishi wa Umma

Tujionee kwanza haya maajabu ya Kikokotoo kwa Watumishi wa Umma

Kama ni matumizi mabaya wabunge kwani hawana matumixi hayo mabaya?
Mbunge ana miaka 47 au 50 anapewa Pesa zake zote..
Ila Mwalimu ana miaka 60.anaambiwa atunziwe kwa sababu anamatumizi mabaya?

Hii haiingii akilini
Huu ni uonevu wa wazi kabisa kwa serikali kuwapangia wastaafu matumizi ya pesa zao.
 
Je mstaafu wa ngazi ya chini asipofariki baada ya miaka 12 anapata nini? Kitu kikubwa waastafu wangedai kuwekewa kikokotoo kinachotizama mfumoko wa bei za vitu (" inflation"). Kama hujawahi kufanya biashara au kukamata pesa mingi, ni vizuri uichukue kidogo kidogo huku siku zinaenda. Watu siku hizi wanaishi maisha marefu miaka 75 au 80 ni kitu cha kawaida sana.
Yaani mstaafu ikitokea akatoboa hiyo miaka 12, na makato nayo yanakomea hapo. Baada ya kuvuka miaka 72, mstaafu atalazimika kuishi kwa jasho lake!

Na ikitokea akafariki kabla ya hiyo miaka 12, fedha zake zinakuwa mali ya serikali. Watoto wake hawapewi chochote! Huu siyo wizi wa mchana huu! Na TUCTA eti walibariki!!!
 
Unaonaje ukiuweka ukweli Mkuu..
Formula

[1/580]×N×APE×12.5×33%

Where:
1/580 = accrual factor
APE = The best three years avarage salary
12.5 =Avarage life expectancy after retirement
33% = pension lumpsum at retirement
N = Number of months contributed
 
Uandike huo ukweli basi ili uongo wangu uonekane hadharani. Kinyume na hapo, basi nitaamini na wewe ni wale wale tu mnaowasababishia wastaafu maumivu, kwa sababu tu ya ubinafsi wenu.
Formula

[1/580]×N×APE×12.5×33%

Where:
1/580 = accrual factor
APE = The best three years avarage salary
12.5 =Avarage life expectancy after retirement
33% = pension lumpsum at retirement
N = Number of months contributed
 
Siyo wizi, pamoja na uchawa wangu wa kumtetea mwenyekiti wangu wa chama ila ukweli kikokotoo ni kizuri. Huyo mpumbavu kapiga mahesabu ya kijinga sana. Aacha kupotosha
Sasa mbona unanishambulia tu huku ukishindwa kuwashawishi wadau kuhusu uzuri wa hicho kikokotoo chenu? Na kwa nini wastaafu wengi wanakilalamikia?
 
Ndiyo maana hilo jamaa nimelitukana halina akili kabisa yaani anapotosha
Leo nitakusamehe kwa sababu tu ni muanzishaji wa huu mjadala. Kwa hiyo matarajio yangu ni kupata majibu sahihi ya kwa nini wastaafu wengi wanakilalamikia hiki kikokotoo chenu cha ujanja ujanja.
 
Inasikitisha hata hiyo 33% wanaipata kwa mbinde inachukua hata zaidi mwaka mzima . Wengi wanastaafu wakiwa hawana cha kuwaingizia kioato zaidi ya mshahara inawafanya waishi maisha ya dhiki sana wengine wanafariki bila hata kuonja jasho lao.
 
hivi ukifa kabla ya hiyo miaka 12 baada ya kustafu ,hela zilizobaki inakuwaje?

na kama wanasema wanataka kumsaidi mtu wa umma asitumie hela zake vibaya, na mfanyabiasha ,mkulima,mfugaji naye huwa wanamsaidiaje asitumie hela zake vibaya?
Ukifa kabla ya hiyo miaka hela zinakua zimekwenda na maji
 
Mkuu,
Jitahidi uwe unapata taarifa toka chanzo rasmi.

Hesabu za kikokotoo hazifanywi hivyo kama ulivyoandika wewe!
Naomba ufafanuzi basi! Je, wastaafu hawapewi 33% ya mafao yao wakati wa kustaafu?

Je, kiasi kinachobakia hawalipwi kila mwezi ndani ya miaka 12 pekee baada ya kustaafu? Na ikitokea mstaafu akafariki kabla ya hiyo miaka 12, je fedha zake zinabakia zinakwenda wapi?

Je, hiki kikokotoo kinawahusu pia Wabunge? Au wenyewe siyo watumishi wa umma? Je, hiki kikokotoo kinamhusu Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika mstaafu, pamoja na wale wajane wa wastaafu?

Na kama hakiwahusu, kwa nini kuwe na ubaguzi na wakati na hawa nao ni watumishi wa umma kama ilivyo kwa walimu na kada nyingine?

Naomba majibu tafadhali.
 
Wewe idiot huna elimu ya kikokotoo, ni mbumbu na lijinga. Kikokotoo ni kizuri sana. Imagine anayelipwa mil 1,300,000 kwa mwezi anakuja kupokea 46 mil kama lumpsum, na bado kila mwezi atapata kama 500k, hivi huyu mtu akiamua kuiwekeza hiyo 46m kwenye duka au mifugo si atatengeneza kama laki tano zingine ukijumlisha anapata kama mil moja, compare na wakati wa ajira ana pungukiwa hela kidogo tu. Na hapo anakuwa na uhakika na cashflow yake.
Huu wema wa kupangia matumizi ya fedha za mtu mnautoa wapi? Nyinyi fedha zenu anawapangia nani kama siyo muendelezo tu wa wizi wenu wa mchana!
 
Naomba ufafanuzi basi! Je, wastaafu hawapewi 33% ya mafao yao wakati wa kustaafu?

Je, kiasi kinachobakia hawalipwi kila mwezi ndani ya miaka 12 pekee baada ya kustaafu? Na ikitokea mstaafu akafariki kabla ya hiyo miaka 12, je fedha zake zinabakia zinakwenda wapi?

Je, hiki kikokotoo kinawahusu pia Wabunge? Au wenyewe siyo watumishi wa umma? Je, hiki kikokotoo kinamhusu Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika mstaafu, pamoja na wale wajane wa wastaafu?

Na kama hakiwahusu, kwa nini kuwe na ubaguzi na wakati na hawa nao ni watumishi wa umma kama ilivyo kwa walimu na kada nyingine?

Naomba majibu tafadhali.
Hawezi Kukujibu Lolote Huyo Ni Mtu Aliyekunywa Kangara Sasa Jambo Lipo Bayana Analeta Porojo. Ukiwa CCM Unatetea Kila Jambo Hata Linaloumiza Watu
 
Unaambiwa Mtumishi wa uuma wa ngazi ya chini aliyefanya kazi serikalini kwa zaidi ya miaka 30. Anapostaafu analipwa 33% tu ya mafao yake.

Yaani kama mtumishi hiyo wa umma alistahili kupata milioni 100 kama mafao (kumbuka hii ni pesa yake halali aliyokatwa kupitia mshahara wake kwa miaka yote hiyo 30+), basi atapatiwa kiasi cha shilingi milioni 33 tu. Na kiasi kinachobakia analipwa kila mwisho wa mwezi kwa muda wa miaka 12! Ikitokea mstaafu akafariki wakati wowote ule baada tu ya kustaafu, na hicho kiasi nacho kinakomea hapo hapo (Wizi wa mchana huu 🤭)
Halafu kichekesho zaidi ni kwamba hiki kikokotoo ni kwa baadhi tu ya Watumishi wa umma! Mfano walimu, Manesi, Maafisa ugani, nk.

Ukija kwa Vigogo wa ngazi za juu, mfano Wabunge; eti wenyewe hawahusiki na hiki kikokotoo! (Ona ubaguzi na upendeleo wa wazi huu 🤭) Ingawa na wenyewe eti ni watumishi wa umma!! Yaani wenyewe kila baada ya miaka 5 ya Ubunge wao, wanapatiwa mafao yao yote yanayokadiriwa kuwa kiasi cha shilingi milioni 250 za Kitanzania!

Ukija kwa vigogo wengine wa juu zaidi; mfano Rais, Makamu, Waziri Mkuu, Spika, na sasa wake wa hao vigogo; ikitokea wamestaafu! Wanapewa mafao yao yote! Na kila mwezi wanalipwa mshahara wa 80% kama ule wa Kigogo aliyeko madarakani kwa wakati huo kwa maisha yake yote! (Ubaguzi mwingine huu 🤭)

Swali la kujiuliza!! Kwa nini serikali mnawafanyia wafanyakazi wenu uonevu na wizi wa mchana kiasi hiki?

Mkiulizwa, mnatoa sababu za kipuuzi tu; eti wafanyakazi wakipewa hela zao zote kwa mkupuo wanaishia kuzitapanya na kutapeliwa, na mwisho wa siku wanakuwa masikini!! Sasa hao wafanyakazi wastaafu wakizitapanya hizo hela zao, nyinyi mnapata athari gani? Je, waliwaomba muwatunzie kupitia hicho kikokotoo chenu cha wizi?

Na kama mnaona ni muhimu kufanya hivyo, kwa nini msifanye mpaka kwa Wabunge? Je, ni kwa mini msitoe uhuru kwa Wastaafu kuchagua kama wanataka kupewa 33% pekee, au mafao yao yote?

Binafsi nimeandika haya malalamiko baada ya kushuhudia wastaafu fulani hivi niliopanda nao daladala sehemu fulani, wakilalamika kwa uchungu baada ya kulipwa mafao kiduchu kwa mfumo wenu huu kandamizi wa 33%.

Ushauri wangu kwa serikali; rejesheni mara moja kikokotoo cha zamani. Acheni kuwadhulumu wastaafu pesa zao.
Huu utaratibu ni mzuri sana. Nimeupenda na hongera kwa aliyeuweka. Kusema ukweli kumpa mfanyakazi eg sh milioni 100 zote kwa mkupuo ni hatari sana. Sh milioni 100 ni fedha nyingi sana kwa mlalahoi na anaweza kuzimia mara anapokabidhiwa kwa sababu alizoea kushika elfu laki mbili. Pia ni kuhatarisha afya ya watanzania na kuwafanya kunenepa kwa kula sana. Viongozi wakubwa ndiyo wanatakiwa kupewa fedha nyingi.
 
Back
Top Bottom