Tujionee kwanza haya maajabu ya Kikokotoo kwa Watumishi wa Umma

Kama ni matumizi mabaya wabunge kwani hawana matumixi hayo mabaya?
Mbunge ana miaka 47 au 50 anapewa Pesa zake zote..
Ila Mwalimu ana miaka 60.anaambiwa atunziwe kwa sababu anamatumizi mabaya?

Hii haiingii akilini
Huu ni uonevu wa wazi kabisa kwa serikali kuwapangia wastaafu matumizi ya pesa zao.
 
Yaani mstaafu ikitokea akatoboa hiyo miaka 12, na makato nayo yanakomea hapo. Baada ya kuvuka miaka 72, mstaafu atalazimika kuishi kwa jasho lake!

Na ikitokea akafariki kabla ya hiyo miaka 12, fedha zake zinakuwa mali ya serikali. Watoto wake hawapewi chochote! Huu siyo wizi wa mchana huu! Na TUCTA eti walibariki!!!
 
Unaonaje ukiuweka ukweli Mkuu..
Formula

[1/580]×N×APE×12.5×33%

Where:
1/580 = accrual factor
APE = The best three years avarage salary
12.5 =Avarage life expectancy after retirement
33% = pension lumpsum at retirement
N = Number of months contributed
 
Uandike huo ukweli basi ili uongo wangu uonekane hadharani. Kinyume na hapo, basi nitaamini na wewe ni wale wale tu mnaowasababishia wastaafu maumivu, kwa sababu tu ya ubinafsi wenu.
Formula

[1/580]×N×APE×12.5×33%

Where:
1/580 = accrual factor
APE = The best three years avarage salary
12.5 =Avarage life expectancy after retirement
33% = pension lumpsum at retirement
N = Number of months contributed
 
Siyo wizi, pamoja na uchawa wangu wa kumtetea mwenyekiti wangu wa chama ila ukweli kikokotoo ni kizuri. Huyo mpumbavu kapiga mahesabu ya kijinga sana. Aacha kupotosha
Sasa mbona unanishambulia tu huku ukishindwa kuwashawishi wadau kuhusu uzuri wa hicho kikokotoo chenu? Na kwa nini wastaafu wengi wanakilalamikia?
 
Ndiyo maana hilo jamaa nimelitukana halina akili kabisa yaani anapotosha
Leo nitakusamehe kwa sababu tu ni muanzishaji wa huu mjadala. Kwa hiyo matarajio yangu ni kupata majibu sahihi ya kwa nini wastaafu wengi wanakilalamikia hiki kikokotoo chenu cha ujanja ujanja.
 
Inasikitisha hata hiyo 33% wanaipata kwa mbinde inachukua hata zaidi mwaka mzima . Wengi wanastaafu wakiwa hawana cha kuwaingizia kioato zaidi ya mshahara inawafanya waishi maisha ya dhiki sana wengine wanafariki bila hata kuonja jasho lao.
 
hivi ukifa kabla ya hiyo miaka 12 baada ya kustafu ,hela zilizobaki inakuwaje?

na kama wanasema wanataka kumsaidi mtu wa umma asitumie hela zake vibaya, na mfanyabiasha ,mkulima,mfugaji naye huwa wanamsaidiaje asitumie hela zake vibaya?
Ukifa kabla ya hiyo miaka hela zinakua zimekwenda na maji
 
Mkuu,
Jitahidi uwe unapata taarifa toka chanzo rasmi.

Hesabu za kikokotoo hazifanywi hivyo kama ulivyoandika wewe!
Naomba ufafanuzi basi! Je, wastaafu hawapewi 33% ya mafao yao wakati wa kustaafu?

Je, kiasi kinachobakia hawalipwi kila mwezi ndani ya miaka 12 pekee baada ya kustaafu? Na ikitokea mstaafu akafariki kabla ya hiyo miaka 12, je fedha zake zinabakia zinakwenda wapi?

Je, hiki kikokotoo kinawahusu pia Wabunge? Au wenyewe siyo watumishi wa umma? Je, hiki kikokotoo kinamhusu Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika mstaafu, pamoja na wale wajane wa wastaafu?

Na kama hakiwahusu, kwa nini kuwe na ubaguzi na wakati na hawa nao ni watumishi wa umma kama ilivyo kwa walimu na kada nyingine?

Naomba majibu tafadhali.
 
Huu wema wa kupangia matumizi ya fedha za mtu mnautoa wapi? Nyinyi fedha zenu anawapangia nani kama siyo muendelezo tu wa wizi wenu wa mchana!
 
Hawezi Kukujibu Lolote Huyo Ni Mtu Aliyekunywa Kangara Sasa Jambo Lipo Bayana Analeta Porojo. Ukiwa CCM Unatetea Kila Jambo Hata Linaloumiza Watu
 
Huu utaratibu ni mzuri sana. Nimeupenda na hongera kwa aliyeuweka. Kusema ukweli kumpa mfanyakazi eg sh milioni 100 zote kwa mkupuo ni hatari sana. Sh milioni 100 ni fedha nyingi sana kwa mlalahoi na anaweza kuzimia mara anapokabidhiwa kwa sababu alizoea kushika elfu laki mbili. Pia ni kuhatarisha afya ya watanzania na kuwafanya kunenepa kwa kula sana. Viongozi wakubwa ndiyo wanatakiwa kupewa fedha nyingi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…