Tujionee kwanza haya maajabu ya Kikokotoo kwa Watumishi wa Umma

Tujionee kwanza haya maajabu ya Kikokotoo kwa Watumishi wa Umma

wakati huo mama anaupiga mwingi kwa safari zake zisizoisha
laiti hii kazi ninayoifanya sasa ingekuwaga kuna mtu alinishauri,
ningelimtafuta na kumpiga shaba.
ni kwamba tu ni kiherehere changu kusomea hii kazi kwa kuvutiwa na mavazi
Nimecheka sanaaa hhhhhhhhhh

Jipige shaba mwenyewe sasa
 
Huu ni uonevu wa wazi kabisa kwa serikali kuwapangia wastaafu matumizi ya pesa zao.
Halafu cha kushangaza mtumishi huyo huyo akiamua kugombea na akawa mbunge anakuwa na matumizi mazuri..
Ila akiendelea kuwa mtumishi wa umma anakuwa na matumizi mabaya...

Afu Jana wanasema Ndege Mbili za Viomgozi hazitoshi kwahyo wameafkiakiana kuongeza ya Tatu 🤣🤣
 
Hayo ndio mambo ya ccm na bunge lao,Sheria ni lazima iwe na usawa Hela kama nimechangia mimi mwenyewe Kwa Nini unipangie matumizi,?Kwa Nini huyo mtumishi alifa hiyo Hela iliyobakia wategemezi hawapewi?hapa Kuna dhuluma ya wazi nyuma ya pazia na wanafahamu fika kuwa hakuna mstaafu ataishi miaka 20baada ya kustaafu ,ni ngumu ukijaribu kuangalia life expectancy yetu,kama ukibahatika kustaafu ukitoboa miaka kumivp na tano ujue wewe ni chuma .Kama Kuna haki tunaomba mstaafu achague kumchukua jumla au kidogo kidogo.Hata wastaafu wa nyuma bado wanaenda kupokea kidogo kidogo
 
Nimecheka sanaaa hhhhhhhhhh

Jipige shaba mwenyewe sasa
hizi kazi za kitumwa zinakera sana kiongozi
mengi tuliyohadithiwa kabla ya kusomea kozi hizo yalikuwa ya kufurahisha mno
kimbembe umepewa hadi mavyeti afu unakutana na uboya mwingi kazini
kumbe uzeeni unapangiwa hadi namna ya kupewa marupurupu.........alooo
 
Kwa kweli ni dhuruma!
Ingawavyo wanadai pension kwa mwezi angalau inakuwa kubwa lakini siyo fair kabisa!
Hiyo siyo Pensheni. Ni Ile uliyostahili ya Mkupuo wakaibakiza wanakulipa kidogo kidogo Hadi miaka 12.5. Pension haipo kama wale wa kabla ya July 2022. Mfano ulistahili 140m ya Mkupuo, wanakupa 40m, hiyo 100 ndiyo inalipwa monthly kidogo kidogo. Ukiimaliza maybe umejaliwa kuishi Hadi 80yrs utajiju
 
Kama Hiko kikokotoo ni kizuri kama wamavyosema basi waoneshe mfano,kianzie kwao wabunge na viongozi wakuu wa nchi,Kisha kishuke huku chini,sheria ni Msumeno,Isichague katika Hilo.
Kwa mara ya kwanza leo Sheikh wangu THE BIG SHOW tumekuwa na mawazo yanayofanana hata kama tuna tofauti zetu kubwa za kiimani. 👍
 
Ukija kwa Vigogo wa ngazi za juu, mfano Wabunge; eti wenyewe hawahusiki na hiki kikokotoo! (Ona ubaguzi na upendeleo wa wazi huu 🤭) Ingawa na wenyewe eti ni watumishi wa umma!! Yaani wenyewe kila baada ya miaka 5 ya Ubunge wao, wanapatiwa mafao yao yote yanayokadiriwa kuwa kiasi cha shilingi milioni 250 za Kitanzania!
Ufisadi huu unaofanywa na serikali ya CCM kwa wafanyakazi wengine wakati wao wakijilipa kwa upendeleo wa hali ya juu ni laana kubwa sana kwao na familia zao!
 
Acha uongo, mfano ma prof vyuoni walipata mpaka mil 30 tu. Kwa ufupi kila mfuko ulikuwa na fomula yake, ila kwa sasa inatoa fursa sawa. Nimemtukana kwa sababu ni mjinga anapotosha watu. Kikokotoo cha sasa kinamuwezesha mstaafu kuishi bila wasiwasi kwa sababu monthly pension ni kubwa na mstaafu akiiwekeza vizuri lumpsum kwenye miradi mbali mbali inamlipa vizuri hata kama ikitokea lumpsum imeisha anaweza kuishi vizuri. Mleta maada aacha uzuzu
Mpuuzi mkubwa wewe! ungenyamaza kwani hujui ulichoandika na uhalisia ulivyo!
Sidhani hata kama umesoma kilichoandikwa! Wala maisha ya mwajiriwa wa kawaida hujui!
Kaa kimya kuficha upumbavu!
 
Mbona kelele zimekuwa nyingi sasa ili hali hapo nyuma kidogo watu walitulia, nimekaa pale naangalia gemu
 
Nimepiga kijembe ndugu yangu. Unadhani yametoka moyoni? Anyways, mimi msimamo wangu ni kuwa CCM inachezea na kudarau watazania kiasi ambacho inaweza kufanya vitu vya kufikirika. Hebu fikiria wana mpango wa kununua tena eti ndege ya viongozi? Kwa upande mwingine ni vizuri wanavyofanya ili wananchi waamke na kujitetea. Tumekuwa kama makondoo.
Watanzania ni wajinga chochote tunachoambiwa ni ndio tu. Upuuzi sana.
 
Hayati ndio alileta huu upuuzi.
Nakazia huu ni upuuzi wa Hayati.
Upuuzi huu aliuleta Hayati ni upuuzi wake.
Upuuzi huu ni upuuzi kama ulivyo upuuzi wake mwingine aliuleta hayati.
Hapana,hayati aliukataa huu upuuzi..tena aliwaambia wasipitishe huu utaratibu mpaka hii formula ibadilishwe.
Nakumbuka alimtumbua hadi Kiongozi katika ishu hii.
Ila baada ya kutangulia mbele (hapa katikati) wezi wakaipitisha juu kwa juu.
 
Hapana,hayati aliukataa huu upuuzi..tena aliwaambia wasipitishe huu utaratibu mpaka hii formula ibadilishwe.
Nakumbuka alimtumbua hadi Kiongozi katika ishu hii.
Ila baada ya kutangulia mbele (hapa katikati) wezi wakaipitisha juu kwa juu.
Hata mimi pia nakumbuka Magufuli hakupendezwa na huu ujinga. Ni wahuni hawa waliopo madarakani wamefanya haya yote. Wanawaibia hadi wastaafu!
 
Naomba ufafanuzi basi! Je, wastaafu hawapewi 33% ya mafao yao wakati wa kustaafu?

Je, kiasi kinachobakia hawalipwi kila mwezi ndani ya miaka 12 pekee baada ya kustaafu? Na ikitokea mstaafu akafariki kabla ya hiyo miaka 12, je fedha zake zinabakia zinakwenda wapi?

Je, hiki kikokotoo kinawahusu pia Wabunge? Au wenyewe siyo watumishi wa umma? Je, hiki kikokotoo kinamhusu Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika mstaafu, pamoja na wale wajane wa wastaafu?

Na kama hakiwahusu, kwa nini kuwe na ubaguzi na wakati na hawa nao ni watumishi wa umma kama ilivyo kwa walimu na kada nyingine?

Naomba majibu tafadhali.
Mkuu, nahisi unapata taabu kunielewa. Sipingani ma hoja zako, isipokuwa napingana na namna hiyo 33% ulivyoielezea as if ni stand alone formula.

Na ndo maana nikakwambia jitahidi upate taarifa kamili za namna ya kikokotoo kinavyofanya kazi.

Mengine yote ni ukweli, isipokuwa formula ya 33% sio stand alone formula
 
Back
Top Bottom