mbenge
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 4,864
- 10,483
Serikali ya CCM imeshazoea kufanya dhuluma kwa wastaafu. Ilianza kwa watumishi wa iliyokuwa EAC ya awali, wakati wazee wa Kenya na Uganda wakilipwa stahiki zao, kwa upande wa Tanzania "blah blah" zikawa nyingi kisha Kambarage akawapiga na kitu kizito kichwani "story" ikaishia hapo.
Hivi sasa serikali ya CCM ina zigo kubwa la madeni kutoka katika mifuko ya hifadhi na kushindwa kuilipa. Kitu pekee ambacho wameona kinafaa kukifanya, ni kuweka kikokotoo kwa wastaafu, ili ipate unafuu katika kulipa kwa mkupuo mmoja.
Tuliwahi kumpata mtu mwenye uthubutu wa kukemea hadharani na kuchukua hatua, Marehemu Mtikila, pale alipoona haki za msingi za raia zikikandamizwa kwa makusudi na serikali. Tuna chama cha wanasheria, yaani TLS, na pia makundi ya wanaharakati, sijui hili la kikokotoo wanalionaje ama wamewahi kulitolea kauli yoyote ile iliyo rasmi!