Ryzen
JF-Expert Member
- Dec 6, 2012
- 7,301
- 8,706
Leo hebu tuzungumze jambo moja ambalo tunaliona la kawaida lakini lina nafasi kubwa katika maisha yetu, Jambo ambalo huakisi muonekano wetu katika Jamii!
Jambo lenyewe ni “ustaarabu”
Ustaarabu ni kitu cha bure kabisa kama ilivyo heshima, ustaarabu na heshima ni vitu viwili ambavyo haviachani!
Nimeona hili leo mahali, lilinikwaza, naamini hata wenzangu liliwakwaza japo hawakusema.. kwa mfano ukikuta mahali huduma inatolewa kwa foleni kwanini usipange foleni? Kuna gharama gani kupanga foleni uoneshe tu ustaarabu wako?
Hata mwl. Nyerere alikuwa akipanga Foleni achilia mbali nafasi kubwa aliyokuwa nayo katika jamii!
Upo kwenye daladala wewe ni mheshimiwa flani unaona gharama gani kufata maelekezo ya kondakta?
Wewe ni Mkristu unafika kwenye Jamii ya waislamu unaona gharama gani kuishi kama wao?
Wazungu wana msemo wao unasema “When in Rome, Live as Romans Live” yaani “ukiwa Roma ishi kama wanavyoishi Waroma”
Umefika kwenye jamii yenye tamaduni tofauti basi jaribu kuishi kama jamii hiyo inavyoishi.. usioneshe umwamba wako utaonekana si mtaarabu!
Tujaribu kuheshimu na kufata taratibu na mamlaka zilizopo hata vitabu vitakatifu vinatusihi hivyo!
Kuna watu wanasema heshimu kila mtu, ila mimi nakuambia “Heshimu Mtu anayejiheshimu!”
I stand to be Corrected!
“I did nothing wrong but somehow I lost”