Tujitahidi kuwa wastaarabu, Hii ni Reflection yetu katika jamii!

Ryzen

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2012
Posts
7,301
Reaction score
8,706
Leo hebu tuzungumze jambo moja ambalo tunaliona la kawaida lakini lina nafasi kubwa katika maisha yetu, Jambo ambalo huakisi muonekano wetu katika Jamii!

Jambo lenyewe ni “ustaarabu”

Ustaarabu ni kitu cha bure kabisa kama ilivyo heshima, ustaarabu na heshima ni vitu viwili ambavyo haviachani!

Nimeona hili leo mahali, lilinikwaza, naamini hata wenzangu liliwakwaza japo hawakusema.. kwa mfano ukikuta mahali huduma inatolewa kwa foleni kwanini usipange foleni? Kuna gharama gani kupanga foleni uoneshe tu ustaarabu wako?
Hata mwl. Nyerere alikuwa akipanga Foleni achilia mbali nafasi kubwa aliyokuwa nayo katika jamii!

Upo kwenye daladala wewe ni mheshimiwa flani unaona gharama gani kufata maelekezo ya kondakta?

Wewe ni Mkristu unafika kwenye Jamii ya waislamu unaona gharama gani kuishi kama wao?

Wazungu wana msemo wao unasema “When in Rome, Live as Romans Live” yaani “ukiwa Roma ishi kama wanavyoishi Waroma”

Umefika kwenye jamii yenye tamaduni tofauti basi jaribu kuishi kama jamii hiyo inavyoishi.. usioneshe umwamba wako utaonekana si mtaarabu!

Tujaribu kuheshimu na kufata taratibu na mamlaka zilizopo hata vitabu vitakatifu vinatusihi hivyo!

Kuna watu wanasema heshimu kila mtu, ila mimi nakuambia “Heshimu Mtu anayejiheshimu!”

I stand to be Corrected!

“I did nothing wrong but somehow I lost”
 
Ndivyo ilivyo ila kuna jamii moja haiwez kubali kuishi kama jamii nyingine huwa wabishi hao
 
Kimusingi ustaarabu unatokana na tabia ya mtu binafsi. Mfano ni vigumu kumubadilisha mtu kitabia ambaae ameshazoea kuishi katika aina au misingi fulani ya maisha.

kwa mfano ukikuta mahali huduma inatolewa kwa foleni kwanini usipange foleni? Kuna gharama gani kupanga foleni uoneshe tu ustaarabu wako?
 
Kimusingi ustaarabu unatokana na tabia ya mtu binafsi. Mfano ni vigumu kumubadilisha mtu kitabia ambaae ameshazoea kuishi katika aina au misingi fulani ya maisha.
Kabisa
 
Asante kwa ushauri mwanana!
Juzi (alhamis) tulikuwa tumepanga foleni watu 3 mi nikiwa katikati, baada ya mtu wa kwanza kusogea kwa teller (bank frani mji mdogo) yule mtu wa nyuma akani overtake na kusimama mbele yangu, yule mwingine alivyomaliza kuhudumiwa yule mama aliyeni overtake akasogea kwa teller kuhudumiwa sikumsemesha nikamuacha tu, alivyomaliza kuhudumiwa nahisi nafsi ilimsuta akanisogelea kama anataka kuniongelesha, kwa kweli, nilimu ignore nikasogea kwa teller nikamuacha amesimama kwenye mstari. Watu wengine ustarabu ni zero kabisa na utu uzima wao.
 
Leo hebu tuzungumze jambo moja ambalo tunaliona la kawaida lakini lina nafasi kubwa katika maisha yetu, Jambo ambalo huakisi muonekano wetu katika Jamii!
Jambo lenyewe ni “ustaarabu”
Ustaarabu ni kitu cha bure kabisa kama ilivyo heshima, ustaarabu na heshima ni vitu viwili ambavyo haviachani!
Nimeona hili leo mahali, lilinikwaza, naamini hata wenzangu liliwakwaza japo hawakusema.. kwa mfano ukikuta mahali huduma inatolewa kwa foleni kwanini usipange foleni? Kuna gharama gani kupanga foleni uoneshe tu ustaarabu wako? Hata mwl. Nyerere alikuwa akipanga Foleni achilia mbali nafasi kubwa aliyokuwa nayo katika jamii!
Upo kwenye daladala wewe ni mheshimiwa flani unaona gharama gani kufata maelekezo ya kondakta?
Wewe ni Mkristu unafika kwenye Jamii ya waislamu unaona gharama gani kuishi kama wao?
Wazungu wana msemo wao unasema “When in Rome, Live as Romans Live” yaani “ukiwa Roma ishi kama wanavyoishi Waroma”
Umefika kwenye jamii yenye tamaduni tofauti basi jaribu kuishi kama jamii hiyo inavyoishi.. usioneshe umwamba wako utaonekana si mtaarabu!
Tujaribu kuheshimu na kufata taratibu na mamlaka zilizopo hata vitabu vitakatifu vinatusihi hivyo!
Kuna watu wanasema heshimu kila mtu, ila mimi nakuambia “Heshimu Mtu anayejiheshimu!”
I stand to be Corrected!
“I did nothing wrong but somehow I lost” ~Khan

Mkuu kuna mtu kakupita ni kwenye foleni ya maanjumati kwenye sherehe
 
Juzi (alhamis) tulikuwa tumepanga foleni watu 3 mi nikiwa katikati, baada ya mtu wa kwanza kusogea kwa teller (bank frani mji mdogo) yule mtu wa nyuma akani overtake na kusimama mbele yangu, yule mwingine alivyomaliza kuhudumiwa yule mama aliyeni overtake akasogea kwa teller kuhudumiwa sikumsemesha nikamuacha tu, alivyomaliza kuhudumiwa nahisi nafsi ilimsuta akanisogelea kama anataka kuniongelesha, kwa kweli, nilimu ignore nikasogea kwa teller nikamuacha amesimama kwenye mstari. Watu wengine ustarabu ni zero kabisa na utu uzima wao.
Aisee hii ya Bank inakera hatari.. inanikuta mara nyingi sana!
 
Hatuwezi kufanana na dunia ikaenda sawa lasivyo uwe mwishi wa dunia..lazima tutofautiane ili tuheshimiane..
Unaweza kwenda kwa sehemu ukakutana na jamii ya wala mbwa,màshoga,
 
Ni kweli kabisa usemayo...

Tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...

Mfano mpo kwenye foleni mnasubiria taa ziruhusu, mara msafara wa kiongozi huo unapita na taa nyekundu, sasa huo ni ustaarabu gani...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom