Tujuane wana JF wa Mwanza

Tujuane wana JF wa Mwanza

Nina kitambo sijaja mwanza mjini eti yale majengo ya big mall huko furahisha yameshaanza tumika?
 
Pasiansi nzengo gani? Maana sie twajuana kwa nzengo bana, weekend uje hapa kijiwe maarufu cha kahawa idara ya maji pasiansi, unapajua?

Mkuu unanikumbusha jamaa mmoja alipigwa na nzengo nzima na hakufa wala kupata madhara makubwa...kila mtu akawa anamgwaya jamaa kwenye mapambano na mkwara wake ilikuwa anakwambia " wewe mi nilishapigwa na nzengo nzima na wakakimbia wote dogo" ah aha ha aha...utaratibu wa nzengo raha saana.
 
Huyo atakuwa ni chacha wa pasiansi polisi ha ha haaa
 
Hahahaaa, Mkuu nimekukubali unasafiri na ungo?! Kumbe upo ilemela, mimi nimejichimbia Igogo hapa, gari acha voil kabisa ndiyo upande huku kwa mguu, kona mbili tatu huwezi kupotea, ila usisahau mwavuli na gambuti, ikifika saa kumi na mbili usije maana utapigwa ngeta!

Mkuu ingawa sipo kitambo ila hiyo ndio mitaa yangu typical nayajua hadi mashimo ya barabarani.
Igogo huko tena, igogo ipi sasa Morafu, Pepsi, au mlimani?
 
Nami ndo mlezi wa JF ROCK CITY WING.

Heshima kwenu wote.
 
  • Thanks
Reactions: ram
Back
Top Bottom