Poleni kwa majukumu ya kulijenga taifa. Ninaomba msaada wenu wa mawazo kama kichwa cha habari hapo juu kinavyojieleza.
Moja: napenda kufahamu kwanza tofauti kati ya BODY SPRAY, PERFUME, DEODORAT.
Kwa mkutadha huo napenda mnifahamishe nitumie kipi kati ya kimojawapo hapo juu.
Tatu: Ili ujue namna gani ya kunisaidaia hapo juu labda niwaelezee kidogo matamanio yangu, binafsi napenda kunukia ila sio kwa kumkela mtu, napenda nikipishana na mtu aisikie harusu nzuri kutoka kwangu, iwe ya body spary au perfume au hata hio deodorat.
Basi kulingana na maelezo hayo nimeona niombe msaada kwenu kwa yeyeto anafahamu vizuri kuhusu hivyo vitu na ningependa sana kama ningepata msaada wa.
1. Aina gani nitumie(body spray, perfume au deodoart)
2. Kati ya hizo tatu hapo juu category ipi ni nzuri, na aina ipi ni nzuri. Mfano perfume lets say blue for men,
3. Je, naweza kuipata wapi? Muuzaji anaeaminika. Hli hasa ndo lengo halis lililonifanya nilete hii mada kwenu, siku hizi wauzaji wa perfume wamekuwa wengi mno kiasi kwamba nimejikuta nanunua perfume lkn haidumu 72hrs kama wanavyokuwa wanapromote kwenye matangazo yao, wameshindwa kuwa wawazi kwenye biashara zao, nimeona nije humu naamini nitapata maaada zaidi. Bajeti yangu mwisho ni Tsh 40,000/= [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]