Tujuzane!! Benki ikifilisika au kuungua moto wateja waliohifadhi hela zao inakuwaje??

Tujuzane!! Benki ikifilisika au kuungua moto wateja waliohifadhi hela zao inakuwaje??

Asante mkuu, mwenyewe hapa on lipoliuona juu Uzi nikachukua seat,,, nimeelimika sana kupitia huu Uzi. Asante kwa wachangiaji wote
 
Mkuu nimepata concern yako;katika mabenki asilimia kubwa vitu viko structured.Kwa kuanzia,kwenye benki kuna kitu kinaitwa SMR,STATUTORY MINIMUM RESERVE,hii huongezeka kadiri BOT wanavyoona.Kwa mfano BOT waliongeza SMR ya bank kwenye government deposits mpaka 30% of the deposits.(Hii ina maana kama benki wanazo government deposits za 10 Mil,wanalazimika kupeleka BOT 3M kama Statutory Minimum Reserve)...Hili ni la kwanza.
Pili,Kuna kitu kinaitwa DEPOSITORS INSURANCE BOARD,hii iko chini ya Mr.Marisa wa pale BOT,lakini so far,Hii insurance board inao uwezo wa ku'refund 1,500,000 flat kwa wahanga wa benki iliyofilisika.The rationale beyond this ni kwamba wanaamini depositors wengi ni wadogo wadogo,na resarch iliyofanyika inadai kwamba ukilipa maximum ya 1,500,000 utaweza kulipa more than 85% ya depositors wote in full....Una swali??
Mkuu nisaidie hapa.
Kama kuna 10,000,000 na mwenye 500,000 wote watalipwa 1,500,000?
 
Mkuu majany umejibu vizuri sana, sema umetumia maneno ya kitaalam zaidi. Hoja ya mwanawao inamaana japo wengi wetu huwa hatupendi kuuliza vitu hata kama hatujui kwa kuona aibu.

Kwa uelewa wangu ni kwamba, benki inapopewa kibali cha kuendesha biashara huduma za kibenki nchini na BoT, huwa wanatakiwa kuweka kiwango fulani cha fedha BoT, hii ni pesa ambayo hawawezi kuichukua. Na BoT hufuatilia mwenendo wa benki husika na kuitaka iongeze kiwango hicho kutokana na fedha za wateja wake.

Kwa mantiki hiyo kiwango cha hiyo akiba hutofautiana kutoka benki moja hadi nyingine kutokana na kiwango cha fedha walizonazo na ukubwa wa benki.

Na jambo la pili, benki zinakua insured, na hawatakiwi kuwa na kiwango zaidi ya kile ambacho wamekubaliana na kampuni ya insurance na vilevile BoT wanakagua kuona hivyo viwango vinazingatiwa. Ndio maana kila mara utakuta mabenki yanaenda kuweka na kutoa hela BoT. Ni kosa benki kuhifadhi fedha zaidi ya kile ilichopangiwa au kukiwekea insurance.

Hadi hapo nadhani kama benki itapatwa na majanga, wateja wao wanakuwa na uhakika wakupata fedha zao.

Nadhani imeeleweka hata kama sio kwa kiwango ambacho muuliza swali alikitarajia, nadhani wadau wengine wataongezea.

Be blessed
Inamaana unataka kusema kwamba kama MTU atakuwa na kiwango zaidi ya 5 million hatoipata iyo Pesa kulingana na Bank kufilisika
 
Wenye Amana zaidi ya 1.5 mil watalipwa 1.5mil
Chini ya hapo watapata hela zote
 
Inamaana unataka kusema kwamba kama MTU atakuwa na kiwango zaidi ya 5 million hatoipata iyo Pesa kulingana na Bank kufilisika
Scenario ya depositors insurance board ni kulipwa maximum ya 1,500,000 kama ulikua na kiasi zaidi ya hicho kwenye akaunti...ila kama ulikua na pesa chini ya 1,500,000,basi utalipwa kiasi chote.......
Baada ya hapo,taratibu za kawaida za liquidation zinaendelea...tukumbuke benki kama kamouni nyingine ina creditors(suppliers n.k) ambao pia watalipwa....hapa utafuatwa ule mtiririko wa malipo as per sheria inavyosema...huanza na secured creditors......mpaka wa mwisho.Na hapa kama baada ya kuliquidate benki na kukawa na salio,basi wale wenye balance kubwa zaidi ya 1,500,000 huweza kumaliziwa kiasi chao..
 
Samahani kidogo wandugu kama nimeubaka huu uzi....ila na mimi ningependa kuondolewa huu ujinga.........

Ningependa kujua kuwa inakuwaje mpaka benki inafirisika....yaani ni mechanism hipi hutokea hapo......!!?
Mkuu naomba nikujibu kwa ufupi sana.....benki karibia zote hufa kwa kukosa ukwasi..ak.a liquidity...na sio kukosa mtaji!!!
 
Umesoma hadi darasa la ngapi? kwa faida yako - Bank huweka dhamana BOT(BANK KUU YA TANZANIA) - Hawaruhusiwi kua na hela inayozidi kiwango hicho cha dhamana Tofauti kati ya bank zawa na ya kigeni ni gharama unazotozwa za kuhudumiwa bank Mfano: Eco-Bank wameingia na wamecut market price kwa huduma mbali mbali wanazotoa ili wateja kama ww mkimbilie huko -
Bora ungekaa kimya
 
Back
Top Bottom