Tujuzane kuhusu minada mbalimbali ya machinga nchini Tanzania

Tujuzane kuhusu minada mbalimbali ya machinga nchini Tanzania

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
Habari zenu wakuu.

Hakuna sehemu zinaweza kuwa nzuri kwa wajasiriamali wanaoanza kujitafuta kama minada.

Andika hapo jina la mkoa/ wilaya uliopo na siku ya mnada (minada ya wamachinga)
Kama hautojali elezea kwa ufupi pia kuhusu movement na ukubwa wa mnada husika.

# kwa jijini Dar es salaam naomba kujua siku ya mnada kata ya mbande.
 
Nitaomba kusahihishwa kama sitakuwa sawa. Jumanne boko kalfonia, alhamisi Bunju B Sokoni, pia kuna mnada wa zinga bagamoyo, kuna salasala ama mbuyuni Dar.
 
Tulizoea kuona minda mikoani na sio Dar. Maisha yana speed ya upepo sana.
 
Kwa misheni zako inabidi pia uwe unavizia mikesha ya mwenge
 
Yes mkuu taja .
Mbali, umeshacalculate gharama za usafiri? Minada ni kama bilishi, kabila zote zipo mkoa wa simiyu. Kipindi hiki cha mavuno watu wengi huuza mazao yao ya kilimo ili waweze kupata hela ya mahitaji mengine kama vile nguo na vitu vingine. Ni minada mikubwa tu, changamoto kwako itakuwa gharama za usafiri kufika huku.
 
Siku ya Jumanne UNGINDONI kigamboni, mazagazaga kama yote na watoto wazuri wakali kwa sana.
 
Nitaomba kusahihishwa kama sitakuwa sawa. Jumanne boko kalfonia, alhamisi Bunju B Sokoni, pia kuna mnada wa zinga bagamoyo, kuna salasala ama mbuyuni Dar.
Umepatia mkuu salasala ni jumapili na bagamoyo ni jumatatu alafu ijumaa kunduchi mtongani na jumatano ni tabata alafu jumamosi tegeta kibaoni (mcanada)
 
Mkoa wa pwani: jumapili kuna mnada mlandizi alafu alhamisi kuna mnada vigwaza. wengine wataendelea...
 
Back
Top Bottom