Tujuzane madhaifu ya MO SIMBA AWARDS

Tujuzane madhaifu ya MO SIMBA AWARDS

Mo anasema haamini kama Simba imekuwa na mashabiki wa kumwaga kila kona. Lakini hajawa na tuzo kwa watoa hamasa,vikundi na matawi ya Simba. Mashabiki lialia kama yule jamaa bonge na yule mfupi analiaga Simba ikifungwa walitakiwa wapewe tuzo
 
Sikatai hili, nakubaliana nawe mshambuliaji sio kufunga tu, ila sema wewe kwa kipi bocco alimzidi kagere kwa msimu huu, hiyo moja.
Pili! Hushangai mchezaji bora wa klabu, ambae nae ni mshambuliaji, awe mchezaji bora wa klabu ila si mshambuliaji bora, km bocco kamzidi kagere na kuwa mshambuliaji inakuwaje azidiwe na kagere kuwa mchezaji bora kwa ujumla.

Ushawahi kuona wapi T.O anakuwa kaongoza kitaifa ila kwenye shule yake yeye asiwe wa kwanza.
Kweli kabisa mkuu
 
Swala la categories bado lina changamoto. Next time wajaribu kiwashirikisha wadau wengi wa mpira kuhusu nan aingie kwenye category na nan asiingie...
Swala la kapombe kuwepo kwenge category akat zimbe hayupo doesn't make sense.
Swala la chama kutokuwepo kwenye category ya kiungo bora doesn't make sense too...
 
Kwangu mimi nimeona, Mo awards zimezidi kujiongezea thamani, na kuifanya club ya simba izidi kupaa zaidi. Set up ya mandhari ilikuwa poa sana, waandaji walikuwa well organized.

Mapungufu niliyoyaona mimi.
1.MC's , nafikiri Mc Luvanda hakuitendea haki kabisa nafasi yake kama Mc wa Lugha ya kingereza, alishindwa kutoa maelezo mara kwa mara kwa audience yake. Pale kulikuwa na wageni waalikwa waliokuwa wakuongea lugha tofauti na kiswahili, na ndy mana wakawekwa ma Mc wawili lkn matokeo yake Luvanda amekuwa akivizia maneno na matukio ya kuongea. Ilifaa wamuite Jokate pale.

2. Suit, nimependa sana idea ya suit, ni nzr mno, lkn suit za jana hazikuwa na viwango vya kuridhisha. Pengine kitambaa alichotumia sy kizuri au designer mwenyewe kaboronga. Viatu havikuwa classic kbs, Spesho kwa suit za jana, kazingua.....next time watafute au kujaribu mastylist na madesigner wengine waone.

3. Rangi ya suit, jana wachezaji walivaa suit zenye rangi kama yenye uwekundu kwa mbali, nafikiri idea ilikuwa iendane na theme ya simba, lkn kwa maoni yangu, wangevaa rangi ya dark blue, charcoal au grey wangependeza sana. Hakuna tena sababu ya kuweka kile kiua pembeni, just iwe classy suit.
 
Habari za wakati huu wana jamvi

Jana kulikua na tukio kubwa sana la ugawaji wa tuzo za wachezaji waliofanya vizuri katika timu ya Simba Sports Club
Ikumbukwe tuzo hizi zinafanyika kwa mara ya pili kwa maboresho makubwa tofauti na za mwaka jana ambazo zilikua ndo za kwanza

Kwanza nichukue nafasi hii kuupongeza uongozi wa Simba na wale wote waliohusika na kuandaa tuzo hizi ili kutambua mchango wa wachezaji katika timu ya Simba SC

Lakini kama kawaida kila tuzo hazikosi kasoro isipokuwa kwenye tuzo zenyewe basi zitakua kwenye uandaaji wa tukio lenyewe

Binafsi kwenye tuzo naona waliopata walistahili lakini kwenye suala la aundaaji wa tukio ndo nimeona kasoro kidogo

1:Tuzo ya aina moja kwenye vipengere vyote.
Binafsi kwa ufuatiliaji wangu kwenye masuala ya tuzo sijawahi ona kila kipengere kina aina moja ya tuzo yaani tuzo ya mchezaji bora inafanana na goli bora na ya tuzo ya heshima?
Nadhani haya mambo yapo kwenye miziki na filamu.Nategemea msimu ujao tuzo kama ya mchezaji bora iwe hata na kisanamu cha mtu anapiga mpira kama Ulaya na kwingineko wafanyavyo hata kwenye vipengele vingine kuwe na utofauti wa aina ya tuzo.

2:Tatizo la Kiteknolojia
Hili nadhani ni tatizo ambalo kila mtu angeweza kuling'amua kwa jana maana kuna wakati utakuta ma MC wanaongea huku tunawekewa video ya goli la chama yaani ilikua vurugu,pia suala zima la picha za wachezaji wanaowania tuzo zilikua na ubora mbovu najiuliza walishindwa kuwaandaa wachezaji walioingia kwenye categories wakawapiga picha za HD ili wawe wanazidisplay pale kwenye screen?

Hayo ni miongoni mwa mapungufu niliyoyaona mimi jana kwenye tuzo za Mo Simba Award,Mbali na mapungufu hayo lakini lazima tukiri tuzo zile zilifana sana watu walipendeza,vituko vya hapa na pale.kila kitu kilikaa mahala pake mbali na mapungufu ya hapo juu ambayo najua wahusika watayafanyia kazi kwa msimu ujayo

Mwisho niwatakie kila la kheri Simba sasa natumani mnaelekea kweny suala la usajili na sherehe za siku ya Simba (Simba day)

Nawaamini mtafanya vizuri kuliko mwaka jana .
Acha Wivu mkuu ndio maana mnajiita Mabingwa sijui Mabingwa wa nini wakati Bingwa ni mmoja tu.Simba sports club.
 
Wakuu website iliwekwa na mashabiki walihimizwa wapigie wachezaji kura kwa kila category iliyowekwa.Mi binafsi nilipiga kura,kwenye kiungo bora chama pia alikwepo,tatizo mnalalamika wakati hata hamkuwapigia kura mliowaona wanafaa
Kwanye washiriki wa tuzo ya beki Bora Kapombe hayuko uwanjani muda mrefu ...badala yake angekuwa mohamedi Hussein.
Kabisa mkuu... hapa captain msaidizi hakutendewa haki
Mo anasema haamini kama Simba imekuwa na mashabiki wa kumwaga kila kona. Lakini hajawa na tuzo kwa watoa hamasa,vikundi na matawi ya Simba. Mashabiki lialia kama yule jamaa bonge na yule mfupi analiaga Simba ikifungwa walitakiwa wapewe tuzo
Hizi tuzo walikuwa wanapewa tu au kutokana na kura za mashabiki?
 
Nimeongea kama shabiki wa mpira. Tuache kushabikia personality cults. Tusiabudu watu awe Mo au Manji.
Nafikiri wameziita MO kwa sababu yeye ndo mdhamini. MO ni "brand name" na sio jina la MTU. Akitokea mdhamini mwingine zinaweza kuitwa jina lake
 
Hivi MANARA ANAKOSAJE TUZO...???? Yani wangeweka hata kipengele cha mhamasishaji boraa wampe molarii jamaa
 
Halafu Mpoki asiwekwe tena hachekeshi anakera na kutia aibu
 
Back
Top Bottom