Sema wazanzibari wana kiswahili cha tofauti kidogo ukikaa kule unaweza hisi huku bara hatuongei kiswahili, halafu baadhi ya maneno ya kule ni yale ambayo kwa huku kwetu tunayachukulia kama matusi, kwahiyo kama akili yako mbovu wakiongea unaweza jikuta unacheka mwanzo mwisho na unaweza hisi wanafanya makusudi
Hiyo ni kawaida sana katika lugha ambazo huzungumzwa na watu wengi waliotawanyika kwenye eneo kubwa kimakazi.
Hiyo hali inaitwa lahaja.
Hata Kiswahili cha Mombasa kina tofauti na Kiswahili cha Nairobi na sehemu zingine za Kenya.
Hata Kisukuma nacho kina lahaja zake.
Kinyantuzu [Kisukuma cha Bariadi/ Simiyu] kina utofauti na Kisukuma cha Mwanza na Shinyanga. Hata Kisukuma cha Shinyanga kina tofauti zake na Kisukuma cha Mwanza.
Ila vyote ni Visukuma!
Kiingereza nacho ni hivyo hivyo.
Kiingereza cha Uingereza kina tofauti zake na Viingereza vya Marekani, Kanada, Australia, na New Zealand.
Pia, hata Marekani kwenyewe kuna lahaja tofauti tofauti za Kiingereza chao.
Wazawa wa kusini mwa Marekani wana lahaja zao zilizo tofauti na za wazawa wa sehemu zingine za Marekani.
Tofauti hizo za lahaja huwa zipo kwenye tahajia, lafudhi, matamshi, na misamiati.
Zanzibar ‘biringanya’ huitwa ‘biringani’.
Kama hujui na kama mtu unayezungumza naye hajui, nyote mnaweza kudhani ‘yeye’ ndo anakosea, kumbe wote mko sawa ila hamjui tu uwepo wa hizo tofauti ndogo ndogo zilizopo chini na ndani ya lahaja.