Tujuze umeanza kutumia JamiiForums tangu lini? Ni kipi kilichofanya ukavutiwa na JF?

Tujuze umeanza kutumia JamiiForums tangu lini? Ni kipi kilichofanya ukavutiwa na JF?

DR SANTOS

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2019
Posts
12,846
Reaction score
28,106
Habari wana jamvi,

Moja kwa moja kwenye mada, binafsi nilianza kuisikia JamiiForums 2012 na kipindi hicho simu zililokua zinasapoti internet nyingi ni OS, na JAVA phones japo android zilikuepo ila too expensive by that time.

Ni mpenzi wa riwaya nakumbuka rafiki yangu aliniambia riwaya zinatumwa JF nikashawishika kufungua ID lakini nikasahau password nikafungua id tena ikapotea, na kwa sasa ninayo hii kiukweli JF inanifaa sana nimejifunza mengi kupitia JF nimegundua JF ina vitu vingi zaidi ya riwaya experts wa kutosha. JF is the great place to learn.

Wewe je tujuze ulianza lini kutumia JF? Kipi kilichokuvutia.

images.jpg
 
Mpaka sasa mimi ni expert member😀😀
 
Niliisikia kupitia kwa huyu boss mwenyewe alikuwa anaisema na classmate wake. Nilikuwa standard 7 nikajua litakuwa ni jarida kama Mnara wa Mlinzi.

Siku chache baadae nikakutana na kipeperushi kimebandikwa duka flani kimeandikwa www.jamiiforums.com nikakumbuka si ndio hii nyumbani walikuwa wanaisema. Sikuwa na simu nikapuuzia.

Siku moja nikaingia Google kutafuta kitu nikapewa machaguo kutoka JF nikaingia. Tokea hapo nikawa nikibahatisha simu naingia uku, kuanzia form 2 nikapata simu ya Java nikawa naingia kupitia Opera Mini natafuta mada yoyote.

ID yangu ya kwanza nilifungua nikiwa form 4 nikakaa miezi mingi si-log in kwa vile sichangii nasoma tu nikapoteza password, nikaja na ID hii after form 4.
 
Back
Top Bottom