Tukiacha ushabiki wa kivyama na Unafiki, Hoja ya Spika haijajibiwa

Zenue ndio kitu gani mkuu? Huenda hata kiswahili kinakushinda, ndio maana umekomaa na kujadiri watu badala ya issues
Umerudia kosa tena:

Hakuna "kujadiri" kwenye Kiswahili, bali kuna "kujadili"


Wahi QT au madarasa ya MEMKWA
 
Huyu yericho kama kawaida ni mpotoshaji wa ukweli. Inaelekea ndio biashara yake kuna watu wanamlipa.
Kwanza hakuna kundi lililoaminishwa magufuli hakopi. Magufuli alikua na miradi ya kimkakati ambayo wakopeshaji hawako tayari kukukopesha wanaona ni ya kujikomboa kiuchumi. Walipoona tunaanza na hela zetu wenyewe ndio yakajitokeza mabenki tukakopa kwao.
Tofauti na magufuli samia anakopa ovyo bila mkakati. Anakopa ovyo hadi hela za kujenga madarasa kitu wakati wa magufuli tunafanya wenyewe. Chini ya magufuli alijenga moyo wa kujitegemea kwa kuhakikisha anakata unyonyaji wa wawekezaji na kuhakikisha kodi inalipwa. Chini ya samia ni kurukia mikopo yoyote akioneshwa na mabeberu.
Muelekeo tutakopa hadi hela ya kula sikukuu na kushona nguo za sikukuu toka ubeberuni chini ya samia😂
 
SIYO KWELI KWAMBA RAIS SAMIA ANAKOPA BILA MIKAKATI. Tujaribu kuwa waungwana kidogo hata kama hatumpendi kiongozi wetu au chama chake. Kwa mfano, mkopo wa UVIKO-19 fedha zimepelekwa kwenye Halmashauri kujenga madarasa (nani alipendezwa kuona watoto wetu walivyojazana madarasani achia mbali kukaa chini, upungufu wa vyoo n.k.), vituo vya afya, barabara vijijini. Kuboresha elimu, afya na miundombinu ya vijijini siyo mkakati kweli, labda mimi nina uelewa mdogo kwenye dhana nzima ya mikakati ya maendeleo. Tutafakari tafadhali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…