Tukiachana na Masuala ya kutekana , hali ya kiusalama mitaani sio nzuri, Serikali iingilie kati .

Tukiachana na Masuala ya kutekana , hali ya kiusalama mitaani sio nzuri, Serikali iingilie kati .

1. Ukiona mkuu wa mkoa anasema msiwape polisi lawama na mtafute njia mbadala za kujilinda
2. Ukisikia malalamiko ya upinzani juu ya vyombo vya usalama na hakuna uwajibikaji
3. Ukisikia polisi wanashiriki kufanya ukatili wa kijinsia na hakuna maamuzi ya kisheria
4. Ukisikia polisi wanatumika kisiasa

elewa kwamba haya yanatokea kwa sababu na wakati sahihi
Tuna polisi ya hovyo sn
 
Ngoja nikukumbushe visa 2
unamkumbuka yule jamaa aliitwa Hamza alichofanya kwa polisi walipo mdhulumu madini$ yake alichokifanya?

unakumbuka wale askari wa mtwara waliomfanyia tukio muuza madini alafu wakawekwa selo asbh wakakuta mwenzao mmoja amekufa kizembe bila hatia?

dhuruma, utekaji, uuaji sio jambo jema ni hatari sana
Rip Hamza
 
Kutokana na hali ya kudorora kwa usalama wa Wananchi hapa nchini, kuna ulazima wa kutembea au kumiliki silaha muda wote kwa ajili ya ulinzi binafsi au kwa ajili ya kujihami dhidi ya hatari ya vitendo vya utekaji.

Aidha, kuna ULAZIMA wa kubadilisha Sheria zetu na Katiba iliyopo ili suala la Kumiliki Silaha za Moto Kama vile Bunduki au Bastola iwe ni haki ya kila raia wa nchi ambaye mwenye umri wa utu uzima na mwenye akili timamu sawa sawa.
Hii itasaidia Sana kupunguza au kukomesha kabisa matukio ya watu kutekwa kiholela.
sio kwa waTz. Hawa walevi watatumia ovyo hizo bunduki.
 
Wanasiasa bwana.

Watu wanavunja mpaka sanamu la Nyerere??
 
Matukio ya uhalifu ni mengi sana ,mengine yanaripotiwa na vyombo vya habari , mengine tunakutana nayo kwenye mitandao ya kijamii lakini kuna mengine hayaonekani popote .

Tunakoelekea watu wataogopa kufanya biashara na shughuli zao

Watu wanaofanya shughuli zao usiku wataogopa kuendelea nazo

Serikali na vyombo vya usalama vifanye jambo .
Safi kwa kuleta hoja yenye manufaa..... Pia Ifahamike kuwa utekaji nalo ni mojawapo ya doa kwa usalama wa wananchi. Hivyo basi rai kwa vyombo vya ulinzi na usalama kushughulika na vimemelea vyote vinavyoleta uvunjifu wa usalama. Kinyume chake matokeo hasi yatajitokeza.
 
Matukio ya uhalifu ni mengi sana ,mengine yanaripotiwa na vyombo vya habari , mengine tunakutana nayo kwenye mitandao ya kijamii lakini kuna mengine hayaonekani popote .

Tunakoelekea watu wataogopa kufanya biashara na shughuli zao

Watu wanaofanya shughuli zao usiku wataogopa kuendelea nazo

Serikali na vyombo vya usalama vifanye jambo .
Mitano tena. Jeshi lipo imara, wewe upo nchi gani?
 
Back
Top Bottom