Tukianza utaratibu wa kulipa wafanya kazi kwa masaa inawezekana?

Tukianza utaratibu wa kulipa wafanya kazi kwa masaa inawezekana?

mara nyingi hii ni kwa ajira zinazozalisha,ndio maana kuna overtime.

sasa sijajua wewe hao wafanyakazi wako,akifanya kazi mpaka masaa ya ziada unampa nini,ndio kinachoongeza ufanisi,carrots&sticks.
 
Utaratibu wa kulipana kwa masaa mfano kwenye mgahawa wangu, wasaidizi ninawalipa sh 500 kwa saa. Wanatakiwa kufanya kazi kwa masaa kumi. Saa moja la mapumziko halipwi lakini chakula ni bure. Asipokuja kazini halipwi na kila shift anayofanya kazi ana lisaa limoja la mapumziko ya kulipia. Inamaana baada ya siku 30 za kazi atakuwa na likizo yenye thamani ya sh 15,000.

Wafanya kazi wengi wanafanya kazi kwa mazoea, asubuhi anakupigia simu kuwa jirani yake amefariki atakuwa msibani. Anajua mwisho wa mwezi mshahara wake upi kamili.

Hii itakuwa njia ya kuacha kutega kazi. Tumezoea malezi ya kijamaa kuwa faida inagawanywa kwa wote, waliofanya kazi na wavivu.
Hata serikali ingefanya hivi kuleta ufanisi..wabongo excuses nyingi sana ,yaani ndani ya mwezi mmoja sababu hazikosekani za kutokufika job.Uliza kampuni za kigeni ,wanatujua sana
 
Utaraibu huu lazima uendane na kiwango cha mshahara,hauwezi kumlipa mtu mshahara wa shilingi 4000 kwa siku halafu bado ukataka umlipe kwa saa kwa sababu tu ya kumpatia chakula,ukipiga mahesabu hapo muhimu kama nauli ili afike eneo lake la kazi unaweza kuta akafika nyumbani na shilingi elfu moja kama hajaweka vocha wala kununua mahitaji yoyote ya nyumabni kwa siku,ni mpango ambao unafanyika katika baadhi ya nchi ila siyo nchi zenye kuwalipa watu chenji,bali ni nchi zenye kulipa watu hela.
 
Nchi za dunia ya 3 huu utaratibu hawauwezi, maana wafanyakazi wao wanafanya kazi masaa mengi lkn malipo kiduchu.
Unforgetable

[emoji2021]Manners Maketh Man[emoji2021]
 
Back
Top Bottom