Tukibaki Hai, Tutasimulia

Tukibaki Hai, Tutasimulia

TUKIBAKI HAI, TUTASIMULIA - 17

Na Steve B.S.M

Brookhaven, New York.

Saa nne asubuhi

Bwana Lambert aliingia ndani ya ofisi akiwa analegeza tai shingoni.

Mkononi alikuwa ameshikilia mkoba mweusi wa ngozi.

Mkoba huo ulikuwa na kifungo cha chuma.

Aliushikilia mkoba huo vema, upo kifuani kwake ameukumbatia na mkono wake wa kuume.

Alipoingia tu ndani akaurejeshea mlango upesi na kwenda moja kwa moja kwenye kiti chake.

Akaketi na kuuweka mkoba wake ndani ya droo ya meza yake.

Kisha akatulia akiskizia.

Moyo wake ulikuwa unapiga kwa kasi.

Aliukua anausikia kabisa kwenye masikio yake makubwa.

Na pumzi yake haikuwa ya kawaida.

Alikuwa anahema kwa kasi japo si kwanguvu.

Alitulia hapo akifikiria.

Akifiria namna alivyotenda mpaka kufika hapo.

Alikumbuka nyendo zake zote alizopitia mpaka kufikia hapo alipoketi.

Akaona kila kitu kipo sawa.

Akashusha pumzi fupi kisha akatua koti lake sasa.

Koti kubwa jeupe

Akalipachika kwenye kiti kisha akawasha tarakilishi yake kwaajili ya kuandika baadhi ya taarifa ambazo zilipaswa kunakiliwa kwenye mafaili.

Akiwa anafanya hivyo, mara mlango ukafunguliwa.

Akarusha macho yake kutazama.

Mlangoni akawaona wanaume wawili waliovalia sare rangi ya bluu iliyokoza

Wamefunika vichwa vyao na kofia aina ya bareti zenye chapa ya ulinzi.

Wanaume hao, mmoja mweupe na mwingine mweusi, walikuwa wamebebelea bunduki mikononi mwao.

Bunduki kubwa mithili ya majangili wanaolenga kuangusha tembo nyikani.

Nyuso zao hazikuwa rafiki.

Macho yao makali yalimtazama Dr. Lambert kana kwamba mwalifu aliyetoka kufanya mauaji.

Naye Dr. Lambert akawatazama kwa kustaajabu.

Aliwatazama kwa macho yasiyoelewa chochote kinachoendelea hapa.

Aliwafahamu mabwana hawa kama wafanyakazi wa ulinzi wa kampuni mpya iliyopata tenda ya kuimarisha ulinzi eneo hili la maabara ya taifa.

Lakini pia aliwafahamu kama wana-ulinzi wa gredi ya pili, juu yao wakiwepo wanausalama.

Mabwana wale wanaovalia suti nyeusi.

Lakini kwanini hawa wako hapa wakiwa wamebebelea silaha?

Alikuwa anaenda kulijua hilo muda si mrefu.

Bwana mmoja kati ya hao walinzi wawili, yule mwanaume mweusi, akamfuata wakati mwingine akiwa amebakia pale mlangoni.

Akamwambia dokta,

"Tunataka kuona ulichokichukua kule maabara."

Dokta akastaajabu.

Alisema,

"Nini hiko? Sijachukua chochote mimi."

Bwana huyo mlinzi akamtazama kwa macho ya kina kirefu cha maji.

Hakuwa na masikhara.

Alitulia kwa kama sekunde tatu akimtazama dokta pasipo kutia neno.

Uso wake uliongea kila kitu.

Dokta akajifaragua akijitetea,

"Sijabeba kitu mimi. Naamini mtakuwa mmekosea au mmenifananisha."

Bwana yule mlinzi, akanyanyua silaha yake na kumwonyeshea.

Dokta akaogopa sana.

Kuona mdomo wa bunduki ukitazama uso wake kulimfanya atetemeke kwa hofu.

Bwana yule akasema,

"Sitarudia tena. Weka mezani kile ulichokichukua maabara."

Kisha akapayuka,

"Upesi!"

Dokta akaruka kwa woga.

Haraka, kwa mikono yake inayotetemeka, akafungua droo na kutoa mkoba mweusi.

Akauweka mezani.

Ulikuwa ni mkoba mweusi wa ngozi wenye kifundo cha chuma.

Punde tu alipouweka mezani, akanyoosha mikono yake juu na kusema huo ndo' mzigo wake alotoka nao maabara.

Wakati huo wenzake wawili walikuwa wameshafika katika eneo la tukio.

Walisimama kule mlangoni wakitazama kwa kurusha macho yao ndani wapate kuona yanayoendelea humo.

Walizuiliwa kuingia ndani na yule mlinzi aloiyesimama hapo.

Mmoja wao alikuwa ni yule bwana mfupi kuliko wote, na mwingine ni yule kijana mwenye umri mdogo kuliko wote humu ofisini.

Mlinzi yule aliyesimama mkabala na dokta, akauchukua huo mkoba mweusi na kuufungua.

Akaupekua.

Kwa kama sekunde kumi hivi alifanya zoezi lake kisha akaurejesha mkoba huo mezani.

Akamtazama mwenzie aliyekuwepo mlangoni na kumpa ishara ya kutikisa kichwa.

Hamna alichopata.

Kumbe ndani ya mkoba kulikuwa na kiasi kidogo cha chakula kwenye kontena na matunda mawili, ndizi mbivu.

Dokta akauliza,

"Ni nini mmeona humo cha ajabu?"

Mabwana wale hawakujibu. Hapa akapata nguvu zaidi ya kuongea.

Aliunyakua mkoba wake akiwatuhumu walinzi wale kwa kuenenda kama wanyama wasiokuwa na akili.

Alisema ya kwamba yeye hubeba chakula chake hata anapokuwa akifanya kazi maabara kwasababu ya matatizo yake ya vidonda vya tumbo.

Hawezi kungoja mpaka muda wa chakula cha mchana ufike.

Anapaswa kufanya hivyo kwani hapa karibuni hali yake ilikuwa mbaya zaidi kiasi cha kutapika damu.

Aliposema hayo, walinzi wakamwomba radhi wakisema walikuwa katika majukumu yao.

Kisha wakaondoka zao na hali ya hapa ikapoa.

Mabwana wale wawili, wenza na dokta, wakaingia na kumpa pole mwenzao huku wakiwarushia tuhuma wanaulinzi hao kwa kutokuwa makini na kusababisha taharuki kali.

Bwana yule kijana alisema,

"Sasa kazi yetu imekuwa kama gereza. Bunduki na risasi zimegeuka kuwa sehemu ya maabara."

Baada ya muda kidogo, hali ikarudi kuwa shwari na shughuli zingine zikaendelea kama kawaida.

Dokta Lambert, akiwa amehakikisha kuwa kila mtu hapa anashughulika na yake, akafungua droo ya pili ya meza yake.

Macho yake yalikuwa na wangalifu mkubwa.

Alifungua droo hiyo kwa utaratibu mno kiasi kwamba hakutengeneza sauti yoyote.

Kisha akaitazama kwa kuibia.

Mkoba wake ulikuwa umekaa kwa kutulia.

Mkoba mweusi wenye fundo la chuma.

Mkoba huu ulikuwa ni wa pili wakati wa kwanza ukiwa kwenye ile droo ya kwanza ya meza..

Droo ambayo aliutoa mkoba ule aliowapatia walinzi kwaajili ya kuukagua.

Akatabasamu kwa mbali.

Mchezo wake ulienda vile alivyokuwa anatarajia.

Mikoba miwili inayofanana kwa kila kitu ilitosha kabisa kumvusha mto yordani.

Akahisi moyo wake umekuwa wa baridi na adhma yake inaenda kutimia.

Akatabasamu tena.

Baadae jioni, majira ya saa kumi, akiwa ameshamaliza kila jambo hapa kazini akaliendea gari lake akiwa na mkoba wake mkononi.

Alilenga kwenda nyumbani moja kwa moja.

Akauweka mkoba wake mahali salama ndani ya gari kisha akatekenya funguo kuwasha chombo.

Kabla hajaondoka, akasikia ngo-ngo-ngo.

Kuna mtu aligonga kioo cha dirisha la upande wake wa kulia.

Moyo ukamlipuka mithili ya guruneti.

Alishtuka kwa hofu kubwa aliyojitahidi kuizuia isionakane lakini uso wake ukafeli.

Macho yake yalijawa na woga.

Alitazama upesi akamwona mwanaume, kwa nje, akiwa anampungia kwa furaha.

Alikuwa ni bwana yule mfupi anayefanya naye kazi katika ofisi moja.

Bwana huyo alikuwa anatabasamu kwa upana akipeperusha kiganja chake.

Akashusha kioo apate kumsikia.

Bwana yule akasema,

"Samahani sana, bwana. Nadhani unaelekea nyumbani. Unaweza ukaniacha hapo mbele kidogo?"

Bwana huyo alitaja mahali aelekeapo lakini Dr. Lambert akamruka kiunzi.

Alimwambia hapiti huko.

Hata na hivyo, bwana huyo akaendelea kusisitiza apewe lifti, atafahamu yeye mwenyewe pa kushukia huko mbele ya safari.

Dr. Lambert akafikiri kidogo.

Alikosa namna ya kumwepuka bwana huyu, hivyo basi, japo kishingo upande, akaridhia kwenda naye.

Akafungua mlango na kuingia ndani kwa furaha.

Akamweleza dokta namna gani anavyopata shida kwenye usafiri baada ya gari lake kupata hitilafu zinazochukua muda kuzitibu huko karakana.

Lakini maelezo yake, dokta hakuyajali. Badala yake alikuwa anawaza kero ya kumpakia bwana huyu kwenye gari yake akifahamu fika ni mtu wa maneno mengi.

Zaidi bwana huyo alikuwa akimpotezea mahesabu yake ya muda kwani alipanga kuongea na Mitchelle punde tu atakaposhika barabara akitoka maabara.

Aongee naye kuhusu mzigo wao kwasababu leo mwanamke huyo alikuwa akiungoja kwa hamu sana ikiwa ndo' siku ya mwisho kati ya zile alizompatia.

Basi aliendesha akiwa ametulia, mawazo mepesi yamemkaa kichwani.

Kuna muda alisahau kama ana mtu pembeni kwa namna alivyokuwa anafikiria mambo yake.

Muda aliomkumbuka akawa haachi kujiuliza bwana huyo atashukia wapi ili apate kuwa huru na shughuli zake.

Kuna muda alitamani kumshusha kwanguvu lakini ndo' hivyo, aliishia tu kutamani kwani asingeweza.

Jambo hilo lisingemjengea picha nzuri.

Gari likazidi kwenda huku mgeni wake haonyeshi dalili yoyote ya kushuka.

Hata alipobadili barabara akitegemea ataambiwa niache hapo, bado hakufanikiwa.

Mgeni alitulia tuli kana kwamba wanaelekea nyumba moja.

Swala hili likaanza kumjengea hofu taratibu.

Alijiuliza bwana huyu anataka nini?

Alianza kufikiria mienendo yake na hapa ndipo akakumbuka sakata lile la chooni.

Alikumbuka siku ile namna alivyotoka chooni kuongea na Mitchelle kisha akakuta mlango upo wazi.

Alipoenda kutazama ofisini hakumkuta bwana huyu mpaka kitambo kidogo aliporejea kutokea kusikojulikana.

Hapa hofu yake ikaongezeka zaidi.

Hajakaa vizuri, simu ikaita.

Hakuelewa ilikuaje, lakini alijikuta anatazamana uso kwa uso na bwana yule.

Akatoa simu mfukoni mwake na kutazama.

Ilikuwa ni namba isiyokuwa na jina lakini moja kwa moja aliishaitambua.

Alikuwa ni Mitchelle.

Akazima sauti kisha akaiweka simu juu ya dashboard ikiwa inatazama chini.

Kukawa na utulivu kidogo.

Lakini haikuchukua muda, simu ikaita tena.

Dokta akaitazama akiwaza. Mwendo wa gari kaupunguza.

Yule bwana wa pembeni akamwambia,

"Si upokee?"

Akamtazama.

Badala yake akaiminya tena simu hiyo na kuendelea na safari kidogo kabla hajaegesha gari pembeni na kumtama bwana yule ashuke.

Alimwambia,

"Nadhani hapa panakutosha. Naomba ushuke, nina safari zangu zingine."

Bwana yule akatabasamu.

Alikuwa ametulia kwenye siti yake kama mtu anayewaza jambo.

Kabla hajafanya kitu, simu ya dokta ikaita tena. Akamtazama dokta na kumwambia,

"Ni yule uliyekuwa unaongea naye chooni, sivyo? Sasa kwanini haupokei?"

Hapo dokta akayakodoa macho.

Akapokea simu ile iliyoita, akasema maneno machache,

"Tafadhali, nakupigia si muda mrefu."

Aliongea akiwa anamtazama mgeni wake. Alipokata, akiwa anatazama kwa walakini, akamuuliza bwana yule,

"Maongezi gani chooni?"

Bwana yule hakujibu. Aliendelea kutabasamu kwa mbali akitazamana na dokta.

Macho yake yalikuwa yanaongea.

Dokta aliyatazama kwa umakini akauona ujumbe wake humo.

Bwana huyo alikuwa anajua JAMBO.

Kumbe siku ile hakukosea kabisa kuwa na mashaka naye pale alipotoka chooni.

Alimuuliza,

"Dr. Jean, niambie ni nini unafahamu?"

Bwana yule akatabasamu sasa akionyesha meno.

Kisha akamwambia Dokta kuwa aliskia kila jambo aliloliongea akiwa chooni.

Lakini pia kama haitoshi, alikuwa anajua kilichotokea leo hii kuhusu mkoba ule mweusi wa ngozi.

Alimwona Dokta akiwa maabara na kupakia baadhi ya vitu kwa siri. Na hata alitambua kuwa mkoba ule aliompa mlinzi kuukagua haukuwa wenyewe.

Mkoba halisi ulikuwepo kwenye droo ya pili. Na huo ndo' mkoba ambao anao hivi sasa kwenye gari.

Alisema,

"Kabla ya walinzi kuja, mimi nilishaona ulichokifanya nikiwa nimesimama dirishani punde baada ya wewe kuingia ofisini.

Niliujua mchezo wote uliokuwa umeupanga, Lambert."

Dokta akakosa cha kusema.

Kwa muda akatulia kitini akijaribu 'kurewind' mambo yote kichwani.

Mbona kila kitu alikiona kipo sawa?

Akajiuliza

Ilikuaje akawa mzembe kiasi hiko?

Maswali hayo yakamnyima fursa ya kumzingatia mgeni wake kwa muda.

Alikuja kurudishwa mchezoni na sauti ya dokta Jean ikisema,

"Sasa naweza nikashuka nikaondoka."

Upesi akamwahi bwana huyo kwa kumshika mkono.

Akamwambia,

"Ngoja kwanza."

Kisha akamuuliza,

"Kuna yeyote umemwambia haya?"

Dokta Jean akajibu,

"Kwa sasa hapana. Sijajua hapo mbeleni."

***
 
TUKIBAKI HAI, TUTASIMULIA -18

Na Steve B.S.M

Katikati ya jiji la New York.

Saa tano usiku

Kulikuwa na gari nyeusi iliyojiegesha pembezoni mwa barabara.

Mbali na gari hilo, shughuli zingine katika heneo hili zilikuwa zinaendelea kama kawaida.

Magari yalikuwa yanaenda na kurudi. Watu wanapandisha na kushusha.

Kila mtu alikuwa anashughulika na yake. Hakuna aliyejichosha na gari hilo.

Baada ya muda kidogo, mwanamke aliyevalia taiti nyeusi, blauzi nyeusi na raba nyeupe chini, huku kichwa chake kimefunikwa na kapelo nyeusi pia, alilifuata gari hilo akalifungua na kuingia ndani.

Mkononi alikuwa amebebelea kijimfuko kidogo kilichosheheni.

Kimejaa kwa bidhaa.

Alikiweka kijimfuko hiko kwenye kiti pacha na cha dereva kisha akavua kofia yake.

Alikuwa ni Mitchelle.

Alitikisa kichwa kutengenezea nywele zake vema kisha akashusha pumzi fupi ya uchovu.

Katika mfuko ule wa bidhaa alotoka nao dukani, akatoa humo kijikasha fulani chenye umbo la bomba.

Kijikasha hiko kilikuwa na rangi ya machungwa na maandishi mazuri ya nakshi na rangi za kuvutia.

Akakifungua kwa kubandua kijimdomo chake kisha akaingiza mkono wake humo.

Akawa anakula taratibu akiwa anatazama njia.

Vilikuwa ni vipande vidogovidogo vya viazi.

Akivitafuna vinalia kakara-kakara.

Akiwa anaendelea kutafuna, mara akaona gari alilolitambua.

Huenda gari alilokuwa analingoja.

Gari hilo lilisonga likasimama mbele ya gari lake, mita chache tu zikiwatenganisha.

Akaacha kutafuna 'bites' zake akiongeza umakini kwenye gari hilo.

Kuna kitu alikiona humo ... alijitilia shaka lakini alipoendelea kutazama aliamini ameona kitu sahihi.

Si kwamba alikiumba yeye mwenyewe kichwani.

Hapana. Ni kitu sahihi.

Na kitu hicho ndo' kilimfanya aweke mazingatio yake makubwa hapo.

Alijisemea mwenyewe,

"Ni nani yule ameongozana naye?"

Macho yake yakimtazama Dr. Lambert na mwanaume ambaye alikuwa mgeni machoni pake.

Kila alipomfikiria bwana huyo hakupata taarifa yoyote kichwani, haijalishi alifikiri kwa kina kiasi gani.

Aliamini ndo' kwanza anamwonea hapa.

Sasa yanini Dr. Lambert kuongozana naye?

Akafungua droo ya gari na kutoa bunduki ndogo humo.

Alipoona ya kwamba kila kitu kipo vema, akajiweka tayari kwa hatari yoyote inayoweza kutokea mbele yake.

Ndani ya gari lile, akamwona Dr. Lambert akiwa anaongea na mwanaume yule mgeni.

Ni kana kwamba walikuwa wanajadiliana cha kufanya.

Dr. Lambert aliongea kwa kutumia mikono yake mara nyingi wakati yule mwingine akiongea mara chache, mara nyingi akiitikia kwa kutikisa kichwa.

Kidogo, Dr. Lambert akashuka akiwa na kijimkoba cheusi mkono wake wa kuume.

Alitembea akifuata gari la Mitchelle kwa mwendo wake wa miadi.

Wakati huo, yule mwenzake katika gari, yaani Dr. Jean, akiwa anamtazama kwa kila hatua.

Bwana huyo alikuwa anatazama mithili ya muuza genge anayemngojea mwizi adokoe mali yake.

Dr. Lambert akafungua mlango wa gari la Mitchelle na kuketi.

Alifanya hivyo baada ya kuhamisha mfuko wa bidhaa wa Mitchelle.

Alipoketi, kukawa kimya kidogo.

Alimtazama Mitchelle akamwona mwanamke huyo akiwa bado anatazama gari lake.

Akasema,

"Nitakuelezea, Mitchelle."

Mitchelle hakusema jambo. Bado macho yake yaliendelea kutazama gari lile.

Dr. Lambert akafungua mkoba wake akisema,

"Kila kitu kipo tayari. Mazingira yangu yalikuwa magumu lakini nashukuru nimefanikisha."

Alitoa 'tube' moja yenye mfuniko kutoka kwenye mkoba wake.

Tube hiyo ilikuwa na kimiminika rangi nyekundu.

Akaifyonza na bomba la sindano kisha akaifanyia majaribio.

Akaona kila kitu kipo vema.

Akamwambia Mitchelle,

"Ni muda sasa."

Mitchelle akamtazama na kuitazama sindano aliyoishikilia mkononi.

Akaona jambo geni.

Akauliza,

"Mbona rangi nyekundu?"

Dokta akatabasamu kidogo kisha akamtoa hofu.

Alimwambia ni rangi tu lakini hakuna component yoyote iliyobadilika ndani ya kemikali hiyo zaidi ya maboresho makubwa alofanya.

Alimweleza kuanzia sasa na kuendelea, side effects za dawa zitakuwa ndogo mno kulinganisha na ile ya mara ya kwanza.

Mitchelle akautoa mkono wake kumkabidhi dokta.

Huenda hakuwa na imani lakini hakuwa na chaguzi nyingine hapa.

Muda ulikuwa unaenda kuitafuta saa sita ya usiku ili ianze siku mpya.

Dokta akamdunga dawa.

Punde akahisi mwili wake wake unasisimka ajabu!

Vinyweleo vyote vimesimama akihisi baridi kali linapita toka miguuni mpaka kichwani.

Hakuwahi kuhisi hivi hapo kabla.

Lakini baada ya dakika tatu, hali yake ikaanza kurejea katika kawaida.

Alihema akiwa anasikilizia kwa umakini yale yanayoendelea ndani ya mwili wake.

Kitambo hiko kidogo mambo yakawa shwari.

Hakusikia kitu.

Ni kana kwamba hakuna lililotokea.

Dokta akatabasamu.

Alimwangalia kwa macho ya matumaini akamuuliza,

"Unajiskiaje?"

Akajijibu mwenyewe,

"Vizuri enh?"

Kisha akatabasamu. Alifurahishwa na kazi yake japo hakuambiwa.

Mitchelle, akiwa na uso wa uchovu, akamtazama na macho yanayorembua. Kwa udogo wa macho hayo, nusura kidogo yafumbe asione.

Akasema,

"Ni nani yule?"

Dokta akatazama gari lake.

Kule akamwona dokta Jean akiwa ametulia kama maji mtungini. Bila shaka anamngoja yeye.

Akauminya mdomo wake na kuanza kusema.

Kusema yale yaliyotokea.

Moja baada ya jingine.

Alipomaliza, akamwambia Mitchelle,

"Anataka kuonana na wewe, na hiyo ndo' sababu ya yeye kuja hapa."

Mitchelle akamtazama dokta kwa kuyatumbua macho.

Dokta akamuwahi,

"Tafadhali, onana naye hayo mengin--"

Mitchelle akamkatisha,

"Una akili timamu?"

Dokta akajitahid kumweleza namna gani jambo hilo ni salama.

Alimweleza Mitchelle kuwa bwana yule hana madhara yoyote yale kwani hamna anachojua.

Kitendo cha kutaka kukutana naye ni sababu tu ya kusikia habari zake kama vile alivyomweleza hapo mwanzo.

Alimalizia kwa kusema,

"Hayo mengine niachie mimi. Nitajua namna gani ya kuyamaliza."

Mitchelle alikuwa anamtazama bwana huyu kama mtu aliyerukwa na akili.

Alijiuliza kama ni mzima au lah.

Akahitimisha si mzima.

Aliuliza,

"Hivi haya unayoyaongea yanatokea kwenye kichwa chako au kuna mahali pengine unapopatumia kufikiri?"

Dokta akazamisha kichwa kwenye viganja vyake.

Alifikiri asijue namna ya kufanya.

Alimtazana dokta Jean katika gari lake akamrudia tena Mitchelle.

Akamsihi amwamini katika hili. Hawezi fanya jambo la kipumbavu ingali maisha yake pia yapo rehani.

Alimwambia, kama hatokutana na bwana huyo basi itakuwa hatari kwao kwani anajua kila jambo.

Hapo Mitchelle akamwambia,

"Basi atakufa."

Dokta akashika kichwa chake chenye mvi.

Akasema kwa msisitizo,

"Hatuwezi kumuua! Mitchelle, Mungu wangu, ebu niskize.

Kila mtu ameona nimetoka naye kazini alafu kesho habari zije kuwa kafa. Huoni ni kuniweka matatani?

Kwa mara moja duniani, naomba uniskilize."

Mitchelle akaridhia.

Japo kishingo upande.

Alimwonya dokta kuwa lolote lile litakalotokea nje ya makubaliano haya, basi atachukua hatua mkononi mwenyewe.

Hatua ambayo huenda ikapelekea dokta kulazwa futi sita ardhini.

Dokta akaridhia.

Akashuka, maramoja, toka kwenye gari na kumwendea dokta Jean.

Aliongea naye kidogo kisha kwa pamoja wakaongozana kwenda kwa Mitchelle.

Bwana huyo, akiwa anamtazama Mitchelle kwa macho ya butwaa, alimsalimu mwanamke huyo na kujitambulisha.

Taaluma yake ilikuwa inaendana sawia na ile alokuwa nayo dokta Lambert.

Mitchelle akamwambia,

"Nashukuru kukufahamu, Jean."

Akiwa anatabasamu la bandia usoni.

Kisha akauliza,

"Ulitaka kuonana na mimi ... vipi, ulikuwa na shida gani?"

Dokta Jean akamweleza kuwa ni udadisi wake ndo' ulomsukuma.

Baada ya kupata maelezo kutoka kwa dokta Lambert alijikuta anapata hamu ya kushuhudia maajabu kwa macho yake mwenyewe.

Maajabu aliyoyaita ya Milenia.

Alisema,

"Nilishiriki katika kazi ile lakini hatukupata nafasi ya kuona matokeo ya mwisho ya kazi ile.

Ni wachache tu waliobahatika, nami sikuwa mmoja wao."

Baada ya hapo akasema naye anatamani kuwa mmoja wa mradi huu kama ilivyo kwa dokta Lambert.

Lakini hapa kabla hajaendelea kuyasema mengi, akaomba faragha.

Alitaka kuzungumza na Mitchelle wakiwa wawili pekee.

Swala hilo likamshtua Dokta Lambert aliyekuwa ameketi kwenye viti vya nyuma.

Aliyatoa macho yake akiangazia watu hawa wawili walioketi mbele yake.

Jambo walilozungumza halikuwamo ndani ya makubaliano yake na dokta Jean.

Ndiyo kwanza alilisikia hapa.

Akauliza,

"Nini?"

Mitchelle na dokta Jean wakamtazama. Mitchelle akasema,

"Naomba utupatie faragha."

Dokta akayatumbua macho.

Akamtazama Dr. Jean.

Mitchelle akarudia,

"Naomba utupatie faragha."

Akataka kusema jambo,

"Laki--"

Mitchelle akamkatisha kwa kurudia ombi lake. Alikuwa anahitaji faragha.

Alimwambia Dr. Lambert,

"Ni wewe ulisema Dr. Jean anataka kuongea na mimi, sivyo?"

Dr. Lambert akanywea kama unyoya ulonyeshewa.

Hakuwa na namna.

Akashuka na kuendea gari lake.

Alipoketi akawatazama watu wale kwa umakini. Alitumai anaweza kupata kitu kwa kutazama vinywa na sura zao lakini alijidanganya.

Hakuelewa kitu.

Alijiuliza ni nini Dr. Jean anataka kumwambia Mitchelle pasipo uwepo wake? Kwanini kitu hiko kinahitaji faragha?

Kwanini Dr. Jean hakumweleza hapo awalo kuwa ana ujumbe wa kumfikishia Mitchelle?

Alihisi kichwa kinakuwa cha moto kwa mawazo haya ya sasa.

Kila alipomwona Dr. Jean anaongea huku Mitchelle anamsikiza, alihisi tumbo lake linavuruga.

Anahitaji kujisaidia.

Alijisemea,

"Huyu mshenzi ana mpango gani?"

Baada ya muda kidogo, akamwona Dr. jean na Mitchelle wakipeana mikono kisha Dr. Jean akashuka toka kwenye gari.

Waliyamaliza maongezi yao.

Dr. Lambert akashuka aende kuonana na Mitchelle lakini asifike mbali, gari la Mitchelle likatimka.

Mitchelle aliondoka bila kuagana naye.

Alilitazama gari hilo akihisi huenda likasimama lakini haikuwa hivyo.

Na mwendo wake, likatokomea mbele ya macho yake kufumba na kufumbua mara mbili.

Akamtazama Dr. Jean.

Dokta huyo alikuwa anatembea taratibu akilifuata gari la Lambert.

Akamwendea upesi.

Akamkwida kola la shati yake akifoka,

"Umemwambia nini? ... Kwanini ulitaka kuongea naye kwa siri?"

Wakati huo Dr. Jean alikuwa anatabasamu kwa mbali.

Anamtazama kwa macho ya kutojali, asiogope kufura kwa mwenziwe hata kidogo.

Alisema,

"Unaweza kuniacha tafadhali?"

Dr. Lambert, akiwa anatafuna meno yake, akamwachia kwa kumsukuma.

Alimwonyeshea kidole akamwambia,

"Nilifanya kosa kukukutanisha naye, sio?

Utalipia hili!"

***

Brooklyn, New York.

Saa mbili Asubuhi

Jamal alitazama saa yake ya mkononi kisha akaunyoosha mkono wake wa kuume kumpungia mhudumu.

Hapa alipokaa palikuwa pamejificha kidogo. Hakuwa anaonekana kwa urahisi.

Kidogo muhudumu akaja na kumsikiza.

Akaagiza kahawa nyeusi.

Bwana huyu alikuwa amevalia shati la mikono mirefu la rangirangi, ambalo ameliacha vifungo wazi kuonyesha tisheti yake nyeusi ndani.

Suruali ya jeans na raba chapa ya AirMax chini.

Aliegesha mguu wake juu ya mwingine, akafungua simu yake na kuikodolea.

Kwenye kioo hiki kikubwa cha simu yake, kulikuwa na picha ya jengo kubwa la chuo kikuu cha Columbia.

Moja ya chuo kikubwa kinachopatikana katika jiji la New York.

Mbali na picha hiyo kulikuwa na maelezo kadhaa kuhusu chuo hiko na anwani yake.

Kwa chini ya maelezo hayo kulikuwa na taarifa binafsi kumhusu mwanafunzi Jamal.

Hapo palikuwa na jina lake kamili, namba yake ya usajili na pia picha yake.

Katika uwanja huo, Jamal akabofya sehemu ya rekodi za kifedha ya mwanafunzi.

Hapo akaona mwenendo wake wote wa malipo ya ada tangu alipoanza chuo.

Katika rekodi hiyo, muhula wa sasa aliomo (First Year first Semister) palionekana ni patupu.

Kulikuwa na alama ya kimstari hapo ikionyesha haijalipiwa.

Akaminya lips zake na kusema,

"Muda si mrefu, sitakuwa nadaiwa.

Sasa nitakuwa huru na masomo yangu."

Alipoyasema hayo, akatazama mkoba wake mdogo aliouweka mezani.

Mkoba huo ulikuwa umebeba matumaini yake makubwa

Aliporudisha macho kwenye simu, akasikia sauti aloyoitambua.

"Naona umeshafika!"

Alipogeuza shingo, akakutana na Richie.

Mwanaume huyo alikuwa anatabasamu. Amevalia shati jeupe na kizibao cha sweta, rangi ya kijani.

Suruali ya kijivu. Kiatu kikubwa cha ngozi, rangi ya kahawia.

Alimradi kufunika mwili tu.

Bega lake la kushoto, alikuwa amening'iniza begi jeusi.

Aliketi mkabala na Jamal, na baada tu ya salamu, akamuuliza kuhusu kazi yake.

Alisema,

"Umekamilisha, sio?"

Jamal akatikisa kichwa.

"Ndio, kila kitu kipo tayari. Vipi kuhusu pesa yangu?"

Richie akamtoa shaka, pesa amekuja nazo.

Alimwambia,

"Kila kitu kipo ndani ya hili begi."

Akinyooshea begi alilokuja nalo.

Hapo Jamal akatabasamu.

Akavuta begi lake na kulifungua.

Aliuliza,

"Richie, ulitoa wapi hii data uliyonipa?"

Richie hakuwa tayari kusema.

Akaendelea na begi lake.

Humo akatoa faili la rangi ya njano na kumkabidhi Richie.

Richie alipoona faili hilo akasema na nafsi yake,

"Hatimaye. Ukweli ninao mkononi mwangu."

Asante sn ngoja nisonge nayo[emoji123]
 
TUKIBAKI HAI, TUTASIMULIA - 19

Na Steve B.S.M

Jamal akampatia Richie muhtasari wa data ile aliyompatia akaifanyie kazi.

Akamweleza ya kuwa yale yote yaliyomo katika taarifa hiyo yanamhusu binadamu na vijenzi vyake.

Data za muunganiko wa damu ya binadamu, mate ya binadamu na karibia kila kitu kuhusu kemikali zote zilizomo katika mwili hai wa binadamu.

'Chemical composition' za vyakula karibia vyote ambavyo hutumika na binadamu, na pia composition ya karibia kemikali zote ambazo ni sumu kwa matumizi ya binadamu..

'Chemical reactions' karibia zote zinazofanya mwili wa binadamu kufanya kazi kwa ufanisi wake, na athari ya kukosekana kwa kila kemikali ndani ya mwili huo.

Kemikali ambazo zipo tumboni. Kwenye mifupa. Kwenye ubongo.

Kemikali zote zinazozalishwa na ini la binadamu na kazi takribani mia tano za kikemikali zinazofanywa na 'organ' hiyo ndani ya mwili.

Alimwambia Richie,

"Kwa mujibu wa tafiti ya wanasayansi wa chuo cha California waliyoifanya katika mwili wa mwanamke mjamzito, walibaini kuna kemikali takribani mia moja na tisa katika mwili wa binadamu.

Ikiwemo kemikali hamsini na tano ambazo hazikuwahi kuripotiwa popote pale hapo nyuma.

Pia kemikali arobaini na mbili ambazo vyanzo vyake na matumizi yake katika mwili wa binadamu hayafahamiki mpaka leo hii kwa wanasayansi.

Kemikali hizo huitwa 'mystery chemicals'.

Huenda kila mmoja anazo.

Kazi yake mwilini, hakuna anayejua. Chanzo chake mwilini, hakuna anayejua pia.

Lakini ajabu ni kwamba, katika chapisho ulilonipa, zimeanishwa kemikali mia mbili ambazo ni 'mystery'.

Kemikali mpya kabisa, sijapata kuziona wala kujifunza popote pale. Haswa katika mwili wa binadamu.

Kemikali hizo sijajua kazi yake ni nini katika mwili uliotajwa. Na nilishindwa kutafuta majibu zaidi sababu ya masharti uliyonipatia."

Richie akasafisha koo lake kisha akayabandua macho yake kwenye karatasi alilokuwa anasoma.

Akamtazama Jamal usoni.

Mwanaume huyo mweusi alikuwa na macho mekundu. Ni wazi hakupata wasaa wa kutosha wa kulala usiku wa kuamkia siku hii.

Kazi hii ilikuwa kubwa mno.

Wingi wa makaratasi aliyoyashika Richie, ulithibitisha hilo.

Richie akauliza,

"Una uhakika hakuna mtu anayejua kuhusu taarifa hii?"

Jamal akaapa.

Alisema hata mwenzake anayelala naye hakupata kujua ni nini anafanya, hivyo kila kitu kipo salama.

Lakini akamwambia Richie kwamba kemikali hizo ambazo bado hawajazifahamu, huenda angepata taarifa zake kama angemshirikisha profesa wa chuoni kwao.

Alisema,

"Pengine hiko ndo' kinafanya taarifa hii kuwa siri. Huoni hilo?"

Richie akatikisa kichwa.

"Hapana, Jamal. Ni hatari. Naamini kuna taarifa nyingi zijazo, tutakapozipata kwa ukamilifu wake basi tutajua mengi. Acha kwanza nikapitie hizi."

Simu ya Jamal ikaita.

Aliichomoa mfukoni akaitazama. Jina Huncho.

Akaminya sauti kisha akaendelea na maongezi.

Alimtaka Richie ampate pesa yake aondoke kwani yuko nyuma ya muda.

Lakini akasihi chapisho lingine litakapopatikana basi apatiwe maramoja kwani kuna jambo amelihisi na nafsi yake.

Alisema,

"Yawezekana huu ukawa ni mradi wa kutengeneza watu. Sina uhakika lakini ... Sijui ... Nahisi tu."

Richie akamuuliza akiwa ameyakodoa macho yake,

"Kwanini unahisi hivyo?"

Akapandisha mabega yake na kuupinda mdomo.

Akasema,

"Kwa namna taarifa zilivyopangiliwa humo. Taarifa zenyewe zilizowasilishwa. Na usiri wake. Auhisi jambo? ... Ni hisia tu, nilishawahi kusikiasikia haya mambo ... kama nilivyosema hapo mwanzo ... Nahisi tu. Kama si hivyo basi yawezekana ni kuhusu Pharmaceuticals.

Tutapata dira baada ya kupitia kazi zijazo.

Lakini ..."

Hapa akarudi kwenye swali lake la kwanza kabisa alilouliza

"Richie, umetoa wapi hizi data?"

Richie hakuwa tayari na swali hilo. Akasema hayo ni yake na aachiwe mwenyewe.

Kama ilivyo ahadi, akatoa pesa ndani ya begi na kumpatia Jamal.

Jamal akahesabu na kuona ni timilifu. Akashukuru na kuaga.

Muda wote huo simu ya Jamal ilikuwa inaita kwa kutetemeka mfukoni.

Richie akamtazama mwanaume huyo akienda zake.

Alipotoka tu mgahawani, akatoa simu yake na kumpigia Hilda.

Akamweleza yale yote aliyopata kuambiwa na Jamal.

Alisema,

"Kama utapata muda, naomba tuonane."

Hilda akamjibu,

"Sidhani kama itawezekana leo. Kuna kazi kubwa ya boss Bryson nafanya hapa."

Richie akahamaki,

"Kazi nyingine?"

Hilda akamweleza ya kazi hiyo kuwa amepatiwa asubuhi ya siku hii pale alipokutana na Bryson mahali fulani.

Richie akapendekeza wakutane sehemu ili amsaidie kuifanya.

Pendekezo hilo likamfurahisha Hilda.

Alicheka mtu wa pembeni angesikia.

Kwa upande wa Jamal, bwana yule, kijana barobaro, aliyetoka kuongea na Richie muda si mrefu ulopita, aliingia ndani ya basi akaketi pembeni ya dirisha.

Alipoketi tu, akatoa simu yake iliyokuwa inaita mfukoni na kuipokea.

Alikunja sura akisema,

"Huncho, ukipiga mara mbili inatosha kwani nyumba inaungua moto?"

Sauti ya upande wa pili ikazozana naye. Ilikuwa ni sauti ya mwanaume ikikwaruza.

Sauti hiyo ilisema,

"Jamal, ulisema mpaka muda huu utakuwa ushantumia pesa yangu. Naona kimya, vipi?"

Jamal akamwambia yu kwenye basi. Pesa anayo mfukoni.

Punde atakaposhuka basi atamrushia kwenye simu.

Swala hilo likawa gumu kwa Huncho. Hakupenda wazo hilo.

Alitaka pesa yake cash.

Akamwelekeza Jamal mahali alipo kisha akasema anangoja hapo.

Jamal akakata simu.

Akairudisha mfukoni huku akiongea mwenyewe kwa kulalama.

Alisema,

"Madawa yatakuja kumuua huyu mjinga. Yeye anawaza unga tu, hamna kingine."

Baada ya robo saa akashuka toka kwenye basi.

Akaitoa pesa yake na kuitenganisha mfuko kisha akaendelea na safari.

Muda kidogo akawa amekutana na Huncho mahali palipojificha kiasi.

Mwanaume huyo alikuwa mrefu, mweusi, mwenye kuvalia nguo za rangi rangi nyingi.

Nywele zake amezisokota rasta zilizofika mabegani.

Usoni amevalia miwani nyeusi ya jua.

Jamal alimpatia pesa akazihesabu na kukiri zipo sawa kisha akasema,

"Tuonane tena siku nyingine."

Akaondoka zake akimwacha Jamal hapo.

***

New York Police Department, New York.

Saa sita mchana

Mpelelezi alitoka kwenye ofisi ya mkuu wake wa kazi akiwa ameshika kiuno.

Alikuwa amevalia shati jeupe na 'suspender' nyeusi. Suruali ya kitambaa na kiatu kinachong'aa.

Macho yake yalikuwa yamelegea kama mtu aliye na usingizi, kuchoka au vyote kwa pamoja.

Sauti kali iliyotoka kwenye ofisi ya mkuu wake ilifoka,

"Nakwambia unacheza na sharubu za simba. Sitakustahimili tena, afisa. Sitakustahimili tena!"

Mpelelezi akaufunga mlango na kwenda zake.

Uso wake umeparara.

Akiwa anajongea, akasikia mtu anamwita.

Aligeuka akamwona Babyface kwa mbali.

Bwana huyo alikuwa amevalia suti nyeusi nadhifu.

Nywele zake zinang'aa na kulala kama zimelambwa na paka.

Usoni mwake amevaa tabasamu pana linaloonyesha meno yake yote.

Alimpungia mpelelezi mkono, akamwonyesha ishara kuwa anakuja kisha akaenda zake mwelekeo wa ofisi ya mkuu wa upelelezi.

Mpelelezi akamtazama bwana huyo akiwa anatafakari yake kichwani.

Hakukaa hapo, akaelekea kwenye ofisi yake alipojibwaga katika kiti na kushusha pumzi ndefu puani.

Taratibu akiwa anazungusha kiti chake kwenda huku na kule, akawa anatafakari.

Alikuwa na mambo mengi kichwani.

Ni kama vile ujenzi wa ghorofa ulikuwa unaendelea katika ubongo wake.

Alitafakari mambo yanavyokwenda.

Moja baada ya jingine.

Akili yake ikampeleka mbali ...

Siku za nyuma: Majira ya saa nne asubuhi.

Kule San Fransisco, California. Majira ya saa nne asubuhi.

Aliamka kichwa kikiwa kinamuuma.

Alihisi mtu yumo ndani ya fuvu lake akibondabonda na nyundo.

Akiwa ameshika kichwa chake kuugulia maumivu, akakagua mazingira ya hapa alipo.

Palikuwa ni pageni machoni mwake.

Hayakuwa mazingira ya 'lodge' ile aloilipia.

Akaketi kitako akiwaza na kuwazua.

Palikuwa kimya sana hapa.

Hakujua amefikaje.

Aliwaza kama ni hoteli ama nyumbani mwa mtu.

Akatoka kitandani na kuufuata mlango.

Kifua chake kilikuwa wazi, akiwa amevalia suruali pekee.

Chini yuko peku, anauhisi ubaridi wa sakafu.

Kabla hajaufungua mlango, akasikia sauti ya mwanamke ikiwa inaongea huko upande wa pili.

Akatulia tuli, asikie mwanamke huyo anaongea nini.

Kwa dakika moja za kuskiliza, hakuambulia kitu.

Sauti haikusikika vema.

Ni kana kwamba mtu alikuwa anaongea akiwa ndani ya chungu.

Akaufungua mlango na kushika korido.

Alinyookea sebuleni akamkuta mwanamke akiwa ameketi kwenye kochi kubwa, mezani kuna sahani nyeupe yenye bites.

Sebule hii ilikuwa pana lakini yenye uhaba wa samani.

Makochi mawili tu yalikuwapo hapa pamoja na meza ndogo.

Ni bayana mkazi wa hapa alikuwa akipendelea zaidi nafasi kuliko mrundikano wa vitu.

Mwanamke huyo alikuwa anaongea na simu, na punde alipomwona Mpelelezi akakatisha maongezi yake ili apate kumlaki.

Alikuwa ni mwanamke yule wa Casino.

Alikuwa amevalia blauzi fupi rangi ya pink iliyoacha tumbo lake bapa kuwa wazi.

Chini amevalia kibukta kifupi rangi nyeusi chenye michirizi meupe pembeni.

Nywele zake amezibana kwa ustadi mkubwa usidhanie kabisa kama ni ndefu kiasi tunachojua.

Alitabasamu akasema,

"Karibu sana bwana. Naona umeamka."

Mpelelezi akamuuliza imekuaje akafika hapo. Alitaka kujua ni nini kilitokea jana yake usiku.

Mwanamke yule akampoza.

Akamsihi atulie kwanza, atafahamu kila kitu.

Alimuuliza,

"Unajiskiaje?"

Mpelelezi akajibu yuko sawa, lakini mwonekano wake ukiwa kinyume na anachosema.

Kila saa alikuwa anakunja uso wake kwa maumivu ya kichwa na mwenyeji wake akalibaini hilo.

Akamwambia,

"Nilikuandalia supu kwaajili ya hangover. Ni vema ukaipata sasa."

Mwanamke huyo akaenda jikoni na punde akaja na bakuli zuri lenye supu ndani yake.

Akampatia Mpelelezi akimkaribisha.

Lakini kabla Mpelelezi hajatia kitu mdomoni, akauliza,

"Nini kilitokea jana? ... Nataka kujua."

Mwanamke yule akamjibu,

"Nadhani ulikunywa kupita kiasi."

Mpelelezi akapata mashaka.

Hakuwahi kunywa kiasi cha kupoteza kabisa fahamu zake.

Hiyo jana kulitokea nini kiasi cha kushindwa kujimudu?

Ghafla akajipapasa mfukoni mwake.

Hakuhisi kitu.

Mwanamke yule akamwambia,

"Simu zako nilizihifadhi kwaajili ya usalama. Ngoja nikupatie."

Akaenda zake chumbani.

Mpelelezi akiwa hapo sebuleni peke yake, akarusha macho yake huku na kule kufanya ukaguzi wa mazingira ya hapa.

Kichwa bado kilikuwa kinamgonga.

Kuna muda alishindwa kuhimili akakishika kwanguvu.

Punde Mwanamke yule akarejea akiwa na simu mbili mkononi pamoja pia na dawa ya kutuliza maumivu.

Akampatia Mpelelezi.

Mpelelezi akanywa dawa hizo maramoja akisindikizia na maji mengi alopewa.

Akiwa anafanya hivyo, mwanamke yule akawa anamtazama kwa udadisi.

Alimwambia,

"Kunywa sasa supu yako kabla haijapoa."

Mpelelezi akafanya vivyo, lakini kiu yake ya kutaka kujua yanayoendelea hapa ikambana.

Alitaka kuuliza.

Upesi mwanamke yule akamsihi,

"Kula kwanza. Najua una maswali mengi. Nami ninayo pia."

Kisha akatabasamu.

Mpelelezi akazidi kuamini.

Mwanamke huyu alikuwa ni wa ajabu.

***
 
Back
Top Bottom