leadermoe
JF-Expert Member
- Feb 15, 2017
- 1,392
- 4,588
Umekuja speed mwenyewe ukajua tayariNaam Kaka[emoji91]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Umekuja speed mwenyewe ukajua tayariNaam Kaka[emoji91]
Ume like alichosema[emoji38]sijatia neno mimi
Hahaaa Nilimaanisha uvosema utaniuliza maswali kujiridhisha nahilo nikama ulijua bado sijafika huko episode ya 18 nilosema nilisema tu kukuridhisha hahaa sema nimesoma naendelea ila kuna sehemu Sijaelewa watoto wa Bryson hao mapacha Celina na mwenzie wanaumwa nini mpaka wanatakiwa kupewa dawa kila Siku?? Na mama yao pia naona anamatatizo hashiriki tendo na mumewe Bryson kisa ninini??? nimerudia kutafuta sehemu ya hayo maelezo sijaona au labda ni mawenge yangu ndio sijapaona labda!!@moneytalk unamsapoti Antonnia kuniita mie mchawi[emoji22][emoji22]
[emoji16][emoji16][emoji16]Maelezo ya familia ya Brayson yako sehemu ya 2. Tendo wanashiriki ila mke hana uwezo wa kuzaa tena.Hahaaa Nilimaanisha uvosema utaniuliza maswali kujiridhisha nahilo nikama ulijua bado sijafika huko episode ya 18 nilosema nilisema tu kukuridhisha hahaa sema nimesoma naendelea ila kuna sehemu Sijaelewa watoto wa Bryson hao mapacha Celina na mwenzie wanaumwa nini mpaka wanatakiwa kupewa dawa kila Siku?? Na mama yao pia naona anamatatizo hashiriki tendo na mumewe Bryson kisa ninini??? nimerudia kutafuta sehemu ya hayo maelezo sijaona au labda ni mawenge yangu ndio sijapaona labda!!
Naendelea kusoma sema ina matukio mengi ila jinsi navoendelea kusoma napata picha!!
Kuna Kuna Bryson Mitchelle kutumika kwenye mission ya kudungwa sindano ya madawa Dr Lambert Richie Hilda yule mwanamke aliepeleka bahasha yenye dollar kwa Bry Kampuni ya Bry kuzorota madeni aliyonayo mission ya kuuza ungaa etc so tupo pamoja
amenifurahisha tuUme like alichosema
uko vizuri lovHahaaa Nilimaanisha uvosema utaniuliza maswali kujiridhisha nahilo nikama ulijua bado sijafika huko episode ya 18 nilosema nilisema tu kukuridhisha hahaa sema nimesoma naendelea ila kuna sehemu Sijaelewa watoto wa Bryson hao mapacha Celina na mwenzie wanaumwa nini mpaka wanatakiwa kupewa dawa kila Siku?? Na mama yao pia naona anamatatizo hashiriki tendo na mumewe Bryson kisa ninini??? nimerudia kutafuta sehemu ya hayo maelezo sijaona au labda ni mawenge yangu ndio sijapaona labda!!
Naendelea kusoma sema ina matukio mengi ila jinsi navoendelea kusoma napata picha!!
Kuna Kuna Bryson Mitchelle kutumika kwenye mission ya kudungwa sindano ya madawa Dr Lambert Richie Hilda yule mwanamke aliepeleka bahasha yenye dollar kwa Bry Kampuni ya Bry kuzorota madeni aliyonayo mission ya kuuza ungaa etc so tupo pamoja
Ahaaa hapo sawa nahisi sikupaona! Naendelea kusoma asante sana[emoji16][emoji16][emoji16]Maelezo ya familia ya Brayson yako sehemu ya 2. Tendo wanashiriki ila mke hana uwezo wa kuzaa tena.
Poa poaAhaaa hapo sawa nahisi sikupaona! Naendelea kusoma asante sana
Endelea mkuuTUKIBAKI HAI, TUTASIMULIA -- 37
Na Steve B.S.M
Pennyslavia, Marekani. Majira ya saa nane mchana.
AFISA Michael Summer alivua miwani yake ya jua akaiweka juu ya ‘dashboard’, alifanya hivyo baada ya kuzima gari lake kwani sasa hakuhitaji miwani hiyo maana ameshatoka juani na safari yake imekomea hapo, akafungua mlango na kutoka ndani kisha akaunyoosha mgongo wake, mgongo ukalia ka-ka-kaa! Akashusha pumzi ndefu ya uchovu kisha akalijongea jengo moja lililopo mbele yake, jengo lenye bango kubwa linalosomeka: THE SMITHS. Jengo hilo lilikuwa linahusika na mauzo ya vipuri vya magari, mlango na kuta ya jengo hilo kwa mbele ilikuwa ni ya kioo kitupu.
Akiwa anasogelea mlango, amebakiza kama hatua nne hivi, mara bwana mmoja aliyevalia ‘overall’ ya bluu na kapelo nyeusi alitoka ndani ya jengo hilo akiwa anatembea kwa upesi. Bwana huyo alikuwa anatazama chini akitembea, kidogo akampisha bwana Michael lakini kabla hajaenda popote alihamaki mkono wake wa kushoto umedakwa, kutazama akaona uso wa Michael ukimwangazia na kwenye mkono wa kushoto bwana huyo ameshikilia ‘beji’ ya polisi aliyokuwa anamwonyeshea.
Michael akasema, “bila shaka wewe ni Anthony Sandlers,” kabla bwana yule hajajibu, akaongezea: “mimi ni mpelelezi, nina maongezi kidogo na wewe.”
Maneno hayo yakamshtua bwana yule ndani ya overall. Alimtazama afisa Michael kwa macho ya shaka kisha akatikisa kichwa kuridhia alichoambiwa lakini ajabu ni kwamba punde mkono wa bwana huyo ulipoachiwa, alitimka mbio kama mwendawazimu!
Alitupa miguu yake kadiri alivyoweza akielekea mashariki mwa jengo lile, bwana Michael naye asiwe nyuma, akatimka kumfukuzia. Mbio mbio mbio! Bwana yule alivuka barabara akiyakwepa magari, naye Michael akafanya hivyo! Bwana yule aliwavuka watu na kuwasukuma huku na kule, naye Michael akafanya hivyo! Walikimbizana kwa kama dakika tano pasipo yoyote kufanikiwa.
Ni kama bahati, pikipiki moja ilitokea kusikojulikana ikamsukumia mbali bwana yule mwenye overall. Aliruka juu kiasi chake kisha akabamiza kwenye moja ya kuta ya duka, alipoanguka hapo akawa hana tena jipya, alitulia chini kuugulia maumivu. Bwana Michael Summer, akiwa anahema juu juu, akamsogelea bwana huyo huku akiwa ameshikilia kiuno chake. Alipomfikia akachuchumaa na kumtazama bwana huyo na mbio zake za sakafuni, akamwambia:
“Sasa naona tunaweza kuongea.”
Baada ya muda mchache watu hao wawili wakawa wamo ndani ya gari la Afisa Michael Summer, bwana yule wa overall, Anthony Sandlers kwa jina, akiwa yu kifungoni kwa pingu mikono yake ipo nyuma ya mgongo.
“Kama haufahamu kitu kwanini ulikuwa unakimbia?” Michael alifoka akimtazama Anthony. Macho yake yalikuwa makali, uso wake haukuwa na lepe la utani. “Nakuuliza wewe. Kwanini ulinikimbia?”
“Kwasababu niliogopa!” Anthony akafoka kwa ‘panick’. “Nilikimbia kwasababu niliogopa!” akarudia tena jibu lake. Afisa Michael akaingia mfukoni mwake na kutoa simu, aliifungua akamwonyesha bwana Anthony. Katika simu hiyo kulikuwa na picha kadhaa zinazoonyesha tukio la mauaji ya Travis. Picha ya mwisho ilikuwa ni ile iloandikwa kwa maandishi ya damu ya Travis ‘SUITS AND TIE’.
Anthony akasema kwa mkazo, “van uliyoitoa yard siku hiyo, ndo’ limehusika na mauaji ya afisa huyu wa polisi. Wewe ulikuwa zamu, nataka kujua nani alichukua usafiri huo.”
Kabla Anthony hajajibu, Michael akamwonyesha picha ya van hiyo, picha ambazo zilidakwa na CCTV camera, akasema: “Bila shaka sio gari ngeni machoni pako. Sasa naomba kujua, gari lilitokaje yard ukiwa unalinda na ni nani aliyelichukua.”
Anthony akamtazama Michael usoni, macho yake yalikuwa yanasema jambo lakini hakufungua mdomo kutamka, Michael akamsihi kama hatoonesha ushirikiano basi na yeye atajumuishwa kama mshirika wa mauaji, ‘an accomplice in murder’, kusikia hivyo bwana Anthony akashuku na kujitetea:
“Sijui nani alichukua hilo gari. Lilibiwa tu! … liliibiwa na mtu ambaye sikumwona.”
“Liliibiwa?” Michael akauliza kwa kejeli. “na ulinzi wote ule niliouona pale kwenye yard, gari liliibiwa vipi? Liliwezaje kupita kwenye mageti matatu mpaka nje pasipo kugundulika wakati wewe ndo’ mtu pekee unayetoa ruhusa ya kitu chochote kukatiza getini? Ina maana hukuliona au ulishiriki katika wizi huo?”
Anthony akashusha pumzi, hakuwa na cha kujibu. Alifikiria njia ya kujinasua na kikombe hiki lakini hakupata cha maana kichwani mwake. Michael aliendelea kumhimiza aseme ukweli ili ajiepushe na kesi ya mauaji, alimuahidi bwana huyo kuwa atamlinda na kumsaidia endapo tu akitoa ushirikiano kamili.
“Naamini kuna mtu nyuma ya maamuzi yako, Anthony. Niambie. Unaweza kuniamini.”
Anthony alifikiri. Akakumbuka familia yake nyumbani, mke na mtoto, chozi likamshuka. Aliisikia sauti ikisema kichwani mwake kumkumbusha maagano yake yake ya kazi ya kuwa uhai wa familia yake utakuwa rehani kama akienenda kinyume, akajikuta anatoa chozi zaidi.
Kabla hajasema kitu kingine, risasi ilipasua kioo cha nyuma ya gari kisha ikatua kichwani mwake na kumfumua ubongo! Yani ndani ya sekunde tu, bwana huyo akawa maiti ndani ya gari akimwaga damu pomoni. Afisa Michael akabaki ameduwaa. Hakukaa vema, mdunguaji aliyetoka kufanya tukio la mauaji, akamweka afisa huyo katika ‘target’ yake.
Kisha akavuta pumzi moja ndefu.
******
Kwenye Majira ya Saa tano usiku:
Hilda alijigeuza kitandani akalala chali, mikononi mwake ameshikilia tablet anatazama filamu humo ndani. Mwanamke huyo aliyekuwa amevalia nguo nyepesi ya kulalia, macho yake yalikuwa yamepwaya kwa uchovu wa usingizi lakini hakutaka kusalimu amri, alichokuwa anakifanya ni kubadilisha tu mapozi lakini tablet haiachii mkononi.
Katika chumba hiki hakukuwa na mwanga mwingine isipokuwa mwanga wa tablet pekee. Vitu vingine humu ndani havikuwa vinaonekana vema isipokuwa uso wa Hilda tu ambao ulikuwa unaangazwa na mwanga wa chombo hicho.
Mwanamke huyo akitazama filamu yake, alijisemea: “Nikifika katikati nalala. Nimechoka sasa.” Kisha akapiga mihayo miwili kwa mkupuo. Anapambana na macho asilale.
Katika dirisha la chumba hiko, kwa chini kabisa kuna gari lilionekana likisogea karibu na maeneo haya. Gari hilo lilikuwa ni van nyeusi isiyokuwa na maandishi, vioo vyake vyote ni tinted kiasi cha kutokuona aliyekuwemo ndani ama dereva anayeendesha.
Gari hilo lilisonga na lilipofika karibu na malango ambayo yanatumika kuingilia ndani ya makazi ambamo Hilda yumo, lilijiegesha na kuzima taa, kisha kidogo likazima na injini, kukawa kimya kama vile hakuna kitu.
Hilda alijitahidi kutazama filamu yake lakini kadiri alivyokuwa anasonga mbele akawa anazidiwa, usingizi ulimzidi nguvu mno, ilifikia kipindi aliachia tablet yake ikamwangukia usoni akashtuka kama mbwa aliyetupiwa jiwe, hapo ndo’ akakata shauri, acha tu alale.
Alizima kifaa chake akajilaza lakini kabla hajapotelea usingizini, alisikia mlango wake ukiita kengele keng-keng-keng-keng-keng! Akashtuka, akajiuliza ni kweli amesikia kengele ama ni mang’amung’amu yake ya usingizi, basi akakaa kusikiliza kwa umakini, kidogo kengele ikaita tena, kumbe si mang’amung’amu bali ni uhalisia, mlangoni pake kulikuwa na mgeni. Mgeni katika majira haya ya usiku.
“Nani huyu saa hii?” alilalamika akinyanyuka kitandani, akauendea mlango wake wa sebuleni na kabla hajafungua akachungulia nje kwa kupitia kitundu kilichopo mlangoni hapo, nje akaona sura ya mtu, mtu anayemjua, lakini hakujua kwanini mtu huyo yupo hapo muda kama huo, alitafakari upesi kama kuna jambo lililoenda kombo lakini hakulipata. Alifungua mlango wake akisema, “Karibu.”
Lakini uso wake, dhahiri shahiri, haukuonyesha kumaanisha kile alichokitamka ila hilo halimkuzuia mgeni wake kuingia ndani, aliingia na mlango ukafungwa. Korido ikabakia tupu na kimya.
****
East Hampton, New York. Saa saba usiku.
Bryson alizima gari lake kisha akatulia humo ndani kwa dakika kadhaa. Kuna jambo alikuwa analiwaza. Aliegemea kiti akitafakari, kidogo akashusha pumzi ndefu kisha akaufungua mlango wa gari na kwenda nje. Alihakikisha ame-lock gari yake kwanza ndipo akaelekea ndani. Alipofika mlangoni, alitaka kuweka ‘codes’ za kufungua mlango wake lakini akabaini kuna kitu hakipo sawa.
Taa ya sebuleni ilikuwa inawaka.
Akajiuliza kifuani mwake ni nani aliyekuwapo hapo, basi upesi akaweka codes na alipoingia alitembea upesi mpaka sebuleni, hapo akastaajabu kumwona mke wake amejilaza kwenye kochi. Mwanamke huyo amejikunyata akijifunika shuka.
Kabla hajasema jambo, mwanamke huyo alifungua macho yake na katikati ya giza jepesi la sebuleni akamwona mume wake amesimama kama mnara, akamuuliza: “Umetoka wapi muda huu, Bryson?”
Bryson akaketi, naye mke wake akanyanyuka na kukaa kitako.
“Umerudi saa ngapi kutoka hospitali?” Bryson aliuliza na kuongezea, “mbona hukuniambia kama unarudi nyumbani? Mtoto vipi?”
Mke wake aliguna kwanza alafu akamtaka mumewe atazame simu yake, Bryson akaitoa na kutazama, kwenye kioo kulikuwa na ‘missed calls’ takribani kumi toka kwa mkewe, tena na ‘messages’ kadhaa.
“Ulitaka nikuambiaje, Bryson kama hupokei simu zangu wala kujibu messages zangu?” mke akauliza. “nimejaribu sana kukutafuta, napiga na natuma ujumbe lakini kimya, ulitegemea ningefanya nini kama sio kuja nyumbani? Ajabu nakuja nyumbani haupo na unarejea majira haya? Ina maana huu ndo’ muda wako unaorudi nyumbani mimi nikiwa hospitali kumuuguza mtoto? Bryson!”
Bryson alikaa kimya, mke akaendelea kuongea akilalamika ya kwamba amemkuta mtoto aliyebakia nyumbani akiwa na njaa na amelala peke yake majira hayo ya usiku, alipomaliza kulalamika hayo akarejea kwenye swali lake, Bryson alikuwa ametokea wapi muda huo? Na akaongezea, kwanini hakuwa hapokei simu yake wala kujibu messages zake?
Bryson alikosa cha kujibu kwa muda huo, aliona kama kichwa chake kinafanya ziiiiii – ziiiiii- ziiiiii asielewe hata cha kufanya, upesi mke wake akanyanyuka kama radi na kumwendea kwenye kochi alilokaa, akampokonya simu na kuifungua, moja kwa moja akaenda kwenye ‘call logs’, huko akakuta mtu wa mwisho mwanaume huyo kuwasiliana naye alikuwa ni Hilda!
Mwanamke huyo akaanza kudondosha machozi kama mito ya baraka. Aliitupa simu ya mume wake kwenye kochi kisha akaenda zake chumbani. Korido nzima anavuta makamasi ya kilio. Aliamini kabisa kuwa Hilda ashamchukulia mwanaume wake. Moyo wake ulisinyaa kwa maumivu.
Bryson aliketi pale sebuleni kwa muda kidogo akiwaza mambo haya yanayojiri mbele ya macho yake. Alitaka kusimama kumwendea mke wake lakini akienda huko atamwambia nini akamwelewa? Hakuona jibu. Alikaa hapohapo sebuleni na nguo alizotoka nazo kazini mpaka usingizi ukamsomba, akakoroma kama nguruwe mdomo akiuacha wazi.
Jua linapokucha, aliamka akijikuta hapohapo kwenye kochi, akakurupuka kana kwamba amemwona mwizi. Alipotazama saa yake akashangaa kuona ni saa mbili kasoro asubuhi, upesi akanyanyuka kwenda kumtazama mke wake chumbani, hakumkuta! Akaenda pia kwenye chumba cha mtoto wake lakini pia vilevile hakumkuta, nyumba nzima alikuwa mwenyewe, mke hayupo na pia mtoto aliyekuwa amebakia naye hapa nyumbani hayupo. Akahisi kuchanganyikiwa.
Alipiga simu ya mkewe ikaita lakini haikupokelewa, akawaza kwenda hospitali lakini akienda huko itakuwa nini? Baada ya kufikiria kwa kina akaona ni stara kwenda kazini kuendelea na majukumu yake alafu akitoka huko, majira ya jioni, apitie hospitali kuungana na familia yake, pengine mke wake atakuwa amepunguza jazba. Akajiandaa na muda si mrefu, kama dakika arobaini na tano, akawa amefika kazini.
Huko akakutana na Richie. Alikaa hapo ofisini kwa kama dakika kumi na tano pasipo Hilda kutokea, akamuuliza Richie kama ana habari yoyote kumhusu mwanamke huyo, Richie akasema aliwasiliana naye mara ya mwisho jana mapema, hakupata kuwasiliana naye tena hivyo hajui kinachoendelea, siku ikazidi kusonga, wanaume hawa wawili, wote, wakiwa katika maswali na mashaka. Kila mmoja katika muda wake alimtafuta Hilda pasipo mafanikio, simu ilikuwa inaita lakini haipokelewi.
Yalipofika majira ya mchana, wakati wa mapumziko ya kupata chakula cha mchana, Richie akautumia muda huo kwenda nyumbani kwa Hilda kumjulia hali. Hakuweza kuvumilia mpaka jioni wakati wa kutoka kazini. Kila dakika iliposogea alijikuta anazidiwa na hofu na anapaliwa na woga. Alipofika huko, akaukuta mlango wa Hilda ukiwa wazi pasipo kufungwa na funguo, alitegua kitasa akaingia ndani na punde kidogo akabaini jambo ambalo hakulitegemea.
Jambo la kutisha.
Aliukuta mwili wa Hilda ukiwa kitandani, hauna uhai, damu zimetapakaa kwenye godoro na shuka. Maiti ya mwanamke huyo imeachama mdomo na macho wazi!
***