Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 154,929
- 459,607
Mwenyewe nimeshasahau yaani sijaelewa chochote hata kutag watu naona haina maana nitawasumbua tu masikini kwa hii story iliyosahaulikanimesoma hata sikumbuki yupi ni yupi sababu unaikawiza mno
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mwenyewe nimeshasahau yaani sijaelewa chochote hata kutag watu naona haina maana nitawasumbua tu masikini kwa hii story iliyosahaulikanimesoma hata sikumbuki yupi ni yupi sababu unaikawiza mno
🤣🤣🤣twend hivohivo tutaelewa mbeleMwenyewe nimeshasahau yaani sijaelewa chochote hata kutag watu naona haina maana nitawasumbua tu masikini kwa hii story iliyosahaulika
Kumbe iliendelea hii uwiiii Ndio naiona leo aiseee Bantu Lady Tayukwa baby zu Lovelovie Kalpana leadermoe Gily Santos06 hii kumbe iliendelea bana!TUKIBAKI HAI, TUTASIMULIA - 39
New York, majira ya saa mbili asubuhi.
Makaburi ya Mount Carmel. Hapo palikuwa na watu wachache wasiozidi kumi na mbili, watu hao wamevalia nguo nyeusi za kuhani msiba. Watu kadhaa, haswa wanawake, walikuwa wamevalia miwani nyeusi kufichama macho yao, sio kwa kupambana na jua, la hasha, bali kuficha malenga ya machozi yao.
Miongoni mwa watu hao, alikuwamo Richie. Bwana huyo alikuwa amevalia suti nyeusi, haikumkaa vema, suti ilikuwa pana kuliko mwili wake, kando yake alikuwa amesimama Jamal, mwanaume huyo alikuwa amevalia tisheti nyeusi na suruali nyeusi ya jeans, shingoni mwake amevalia mkufu mwepesi ulobeba nembo ya msalaba. Kwa muda wote huo alikuwa kimya, kimya akimtazama Richie kwa kuibiaibia. Alikuwa anawaza namna gani ya kumchokonoa bwana huyo kwa maongezi. Kila alipomwangalia aliona hayuko tayari, akasema acha ningoje.
Jeneza lilishuka chini ya ardhi, likamezwa na dunia, baada ya hapo watu wakaanza kuondoka kuendelea na shughuli zao, kuondoka wakimwacha mfu mpweke kama ilivyo ada. Waliondoka mmoja mmoja, wakabaki watu wanne, wawili miongoni mwao ni Richie na Jamal.
Jamal hakupenda kuwepo hapa, lakini ilimbidi. Alikuwa anamtazama Richie kila muda kama atakata shauri waondoke lakini kimya, mwishowe akamgusa begani akimwambia waende, msiba ushakwisha, Richie akamtaka atangulie yeye yuko nyuma anakuja, Jamal akaona acha tu angoje.
Baada ya muda, Richie akiwa na macho mekundu yalokaukiwa na machozi, akasema akiwa ameng'ata meno: "damu ya Hilda haitaenda bure." Akarudia tena, damu ya Hilda haitaenda bure.
Hamaki alisema bila kigugumizi.
Lakini, nini kilimkuta Hilda siku ile? Ni nani aliyemfungulia mlango kuja kuitoa roho yake?
***
Brooklyn, New York. Majira ya saa tatu usiku.
Gari jeusi aina ya 'saloon' ilijiegesha pembezoni mwa barabara ya Fifth Avenue ...
Likazima taa,
Kisha na injini.
Kidogo mlango ukafunguka akatoka bwana mmoja mrefu aliyevalia suti, bwana mwenye asili ya Asia, mwendo wake kamilifu akiendea duka kubwa lililokuwa linatazamana naye. Alivuka barabara upesi na si punde akawa mlangoni mwa duka hilo.
Ndani ya duka, mwanaume mmoja mzee wa makamo ya sitini na kitu, alikuwa akitazama 'shelf' ya bidhaa kutafuta kifaa cha kunyolea nywele, mwanaume huyo mzee alikuwa amevalia koti kubwa, kofia aina ya 'newsboy', macho yake yametwaliwa na uzee lakini bado ni angavu.
Akiwa anatazama, akili yake yote ipo hapo, mara akasikia mtu akimtaja jina lake; "Rodney", alipogeuka akamkuta mwanaume yule mwenye asili ya Asia akiwa amesimama kando yake, mikono kaitia mfukoni. Akamuuliza,
"Tunafahamiana?"
Bwana yule naye akamrudishia swali, "unamjua Dr. Lambert?"
Rodney hakujibu, badala yake alimkagua bwana yule anayemuuliza kuanzia juu mpaka chini, macho yake yalisema anawaza kitu kichwani, na ni kweli, alipomaliza kukagua akasema; "hapana, simfahamu," kisha akageukia 'shelf' ya bidhaa kana kwamba hamna kitu kilichotokea.
Alifanya hivyo kwa sekunde kadhaa, akageuka kutazama tena. Hakumwona bwana yule. Alitazama huku na kule lakini hakuwapo kabisa. Hakujua kaelekea wapi, lakini zaidi hakujua bwana yule alikuwa anataka nini, kwanini alikuwa anamuulizia Dr. Lambert?
Alichukua bidhaa yake akailipia kisha akaelekea nje, huko alitazama kushoto na kulia alafu akaelekea gari lake, aliingia ndani na punde alipo-lock mlango, sauti ilitoka kwenye viti vya nyuma ikisema,
"Nadhani hapa tunaweza kuongea vema."
Sauti hiyo haikuwa ngeni. Alitoka kuisikia muda si mrefu. Wapi? Kule dukani, ni yule mwanaume! Akaogopa sana. Alitaka kupiga kelele lakini hakufanikiwa. Alizibwa mdomo wake na kitambaa, si punde macho yake yakalegea kama mtu anayetekenywa na unyoya sikioni, kisha akalala usingizi wa kukosa fahamu.
Bwana yule aliyekuwa kwenye gari akatoa simu yake na kupiga, alafu akasema: "tayari ninae."
Sauti ikamuuliza: "umemdhuru?"
Akajibu: "Hapana, nimemtuliza tu."
"Sawa. Sasa fanya kama tulivyokubaliana." Akapewa hilo agizo kisha simu ikakata. Bwana huyo alimpekua Rodney, mifukoni na pia kwenye gari yake, alipopata anachokitaka aliondoka akamwacha mhanga wake katika gari, bado hajielewi, mdomo ameachama.
Aliendea gari alokuja nayo hapo, akayoyoma. Baada ya kama nusu saa, bwana Rodney ndo' akaamka na kujipata ndani ya gari yake asijue amefikaje humo. Kidogo, akapapasa mifuko yake, sijui alikumbuka nini, alipapapasa kwa haraka na pupa, hakuhisi kitu. Alipoona hivyo akaingiza kabisa mikono yake humo, akapekua na kupekua, hamna kitu! ....ngoja, simu ilikuwepo, pia pesa zilikuwepo, sasa alikuwa anatafuta nini?
Alitazama kioo cha simu yake, pana 'missed calls' tatu, akapiga simu kidogo ikapokelewa, cha kwanza kuuliza ni nini kinaendelea? Hakumaliza maongezi yake, akawasha gari yake na kutimka mbio-mbio!
Akiwa anaendesha aliendelea kuongea na simu, alipokata akapiga namba nyingine, namba aliyoitunza kwa jina la Dr. Lambert, namba hiyo ikaita pasipo kupokelewa. Hakukoma. Akapiga tena. Simu ikaita, bado mtu hakupokea. Basi akawa anaitazama kioo cha simu kila sekunde.
"Pokea simu!" Aliongea mwenyewe. "Pokea simu wewe mpuuzi!"
Alitazama simu mara kadhaa, mwendo wake akikimbiza upepo.
Mara yake ya mwisho alipoitazama simu, alinyanyanyua uso akakutana na gari kubwa likiwa mbele yake. Huo ndo' ukawa mwisho wake. Hakupata hata kuomba maji. Hakupata hata kutumia mashine yake ya kunyolea aloinunua.
Ndani ya sekunde, kichwa chake kikawa kinavuja damu, macho yake yako wazi, usukani umembana na kumpasua kifua chake. Simu yake imerukia huko nyuma ya gari. Inaita. Kwenye kioo ni jina la Dr. Lambert linaonekana. Si muda mrefu simu hiyo ikakata. Mara ikapiga tena. Iliita ikakata. Kidogo, wakati watu wameanza kusogea kutoa msaada na ving'ora vya polisi ama gari la wagonjwa vinaita huko mbali, ujumbe ukaingia kwenye simu. Ujumbe ulisomeka pale kwenye kioo;
"Rodney, usifanye kitu chochote kile cha kijinga. Fanya tuonane haraka iwezekanavyo!"
***
Manhattan, New York. Si muda mrefu tangu ajali ya Rodney ijiri.
Dr. Lambert aliweka simu mezani. Ameukunja uso wake. Alishusha pumzi ndefu, kidogo mlango ukafunguliwa akiingia bwana yule alokuwa na Rodney kule barabara ya Fifth Avenue kabla ya kumkumba kifo chake. Bwana huyo alikuwa ameshikilia mkoba mweusi. Aliuweka mezani kisha akamwambia Dr. Lambert kuwa kazi imekamilika, lakini Dr. Lambert akamdaka mkono na kumuuliza:
"Rodney?"
Bwana yule akauchoropoa mkono wake kwanguvu kisha akasema hajui kitu zaidi ya kumwacha bwana huyo akiwa na uhai wake ndani ya gari yake, baada ya hapo akasisitiza hapo New York wana muda mchache, siku nne tu, hivyo afanye upesi kumpatia maelekezo mengine kabla muda haujawaishia.
Dr. Lambert akagoma. Hakutaka kushiriki kazi nyingine isipokuwa kwa mikono yake mwenyewe. Hakutaka kuharibu zaidi. Hakutaka kutumia nguvu bali akili. Aliamini kama angepewa nafasi ya kuonana na Rodney basi angeimaliza kazi hiyo bila kutumia msuli wowote wa nguvu. Bila kuacha alama wala nyayo kwa wanausalama.
"Lakini nilimuuliza kama anakujua, akasema hakufahamu!" Bwana yule akajitetea. "Sasa ningefanyaje?"
Dr. Lambert akamwambia, "unadhani angesemaje mbele ya mtu aliyemwona kwa mara ya kwanza tena akiwa amevalia hivi?" Akaongezea kwa mkazo, "kama tukifanya hivi kwa kila mmoja ambaye tunakutana naye, tunampoteza fahamu na kumpekua mifuko, tutabaki salama?"
Bwana yule akaukunja uso wake alafu akauliza: "kazi imefanyika au haijafanyika?" Alafu akamkumbusha Dokta nafasi yake, ya kwamba yeye ni mtu wa kuhusika na maabara tu, mambo mengine nje ya hapo ayawache, hayamhusu, sio fani yake, baada ya maelezo hayo, bwana huyo akaenda zake. Lakini baadae ambayo haikupita muda mrefu, wote walikuja kugundua kuwa hali ilikuwa 'serious' ya vile walivyodhania.
Simu ya Dr. Lambert iliita, alipopokea, akasikia sauti iliyojitambulisha kuwa afisa wa polisi, afisa huyo akamuuliza Lambert kama anamjua Rodney kwa namna yoyote ile, Lambert akajibu anamfahamu mwanaume huyo, afisa wa polisi akamalizia kwa kumpatia wito wa kufika kituo cha polisi haraka iwezekanavyo.
Wito ambao ulimfanya Dr. Lambert arukwe na pigo moja la moyo. Akili yake ikawaza kila ovu alilowahi kufanya, lakini zaidi alikumbuka kifo cha yule dokta mwenzake.
Dr. Jean.
"Afisa, kuna nini kimetokea?" Lambert aliuliza. Macho yake ameyatoa kana kwamba madungu. Afisa wa polisi akamwambia kuna ajali mbaya imetokea, na mtu wa mwisho mhanga yule kuwasiliana naye alikuwa ni yeye! Mhanga gani? Akauliza upesi. Afisa wa polisi akamwambia ni bwana Rodney Woods.
Lambert akajikuta anahisi joto.
Joto kali.
Alipoikata simu alimweleza yule bwana alofanya oparesheni ya Rodney juu ya yale yote yalotokea, tena kwa kumfokea na kumnanga. Alipomaliza akamwambia ampeleke kituo cha polisi, huko Dr. Lambert hakupata kutoka, aliambiwa abakie hapo kwaajili ya upelelezi zaidi. Achilia mbali upelelezi wa ajali ya Rodney, bali upelelezi wa kile kilichotokea katika mazingira ya kazi ya marehemu huyo, na zaidi upelelezi kuhusu kifo cha Dr. Jean.
Kwanini bwana huyo alisafiri ingali upelelezi wa kifo cha bwana yule haukuwa umekamilika ukizingatia nafasi yake ya ushahidi ni muhimu? Alijiuliza mwenyewe kichwani akiwa njiani kuelekea kituoni. Ni nini atajibu endapo afisa wa upelelezi akimuuliza?
Lakini hamna ushahidi wa kuonekana. Alijipa moyo mwenyewe. Ni nini cha kumuunganisha na matukio hayo kiasi cha kuaminika? Hamna. Ndio, hamna. Alisema na nafsi yake. Basi akatabasamu. Akatabasamu mwenyewe akiwa katika chumba cha mahojiano.
Akatabasamu akiwa katika chumba hicho mwenyewe, mbele yake kiti cha mpelelezi kilichokuwa kitupu.
***
Simu iliita, Bryson akaitazama. Ni majira ya saa nne ya usiku sasa na bwana huyu alikuwa yu njiani, kwenye gari lake, kurejea nyumbani. Mkono wake mmoja ulikuwa katika usukani wa gari, hata mawazo yake yalikuwa barabarani ila ndo' yalitibuliwa na kuita kwa simu hiyo, akayahamishia kwenye kioo cha simu.
Kutazama ni mkewe. Kidogo simu ikakata.
"Anataka nini huyu?" Alijisemea mwenyewe kifuani.
Aliinyaka simu yake akapiga, kidogo simu ikapokelewa na sauti ya mkewe. Baada ya kujuliana hali, mkewe alimuuliza mahali alipo naye akamwambia yu njiani anakaribia, baada ya hapo, mwanamke huyo akamuuliza;
"Umenionea kibanio changu kikubwa cha nywele?"
Alimuelezea kibanio hicho kilivyo, mumewe akakielewa lakini hakuwa anajua kilipo, hakukumbuka hata mara yake ya mwisho kukitia machoni ni lini. Alipomalizana na simu hiyo aliitupia kwenye kiti cha pembeni kisha akaongea mwenyewe, ndo' nini sasa? Yani kupigiana simu kisa vibanio vya nywele? Wanawake bwana!
Akaendelea na kuendesha gari.
Lakini si mbali ... si mbali ....
Akakumbuka jambo.
Jambo la kumtisha.
Alinyakua simu yake kama mwewe akampigia mkewe, simu ilipopokelewa akauliza upesi, "umepata?"
Mkewe akamjibu hapana, bado anatafuta. Upesi akamuuliza tena, "unatafutia wapi?" Akamjibu chumbani mwa watoto. Hapo moyo wake ukapasuka.
"Chumbani kwa ...?"
Akakata simu kisha akakanyaga pedeli ya mafuta kwelikweli, gari likakimbia almanusura kupaa. Kufika nyumbani, alishuka upesi akaelekea ndani, huko akanyookea mpaka chumba cha watoto, akamkuta mkewe akiwa ameketi kitandani, mkononi mwake ameshikilia nguo ... nguo yenye mabaki ya damu.
Mkewe akamuuliza; "Bryson, ni nini hiki?"
Bryson akiwa ameyatoa macho, hakuwa anajua nini cha kusema. Alihisi kichwa chake kimekuwa cheupe kama theluji. Mdomo wake mzito kama zege.
***
Ilivo ndefuu weeee!! Mi nilichokua Nakumbuka tu ni majina Mitchelle Dr Lambart Dr. Jean Bryson mkewe Hilfa Jennifer mapacha sikumbuki nani alikufa nani yupo hai🤣🤣🤣Asante mamii, hata nilipofika sipakumbuki 🤔🤔🤔 nitaanza upya 😀😀😀😀😀
Mambo mengine yanaudhi,Kama vp wawe wanakaa nazo.maana wao ndo wanaoanzisha kuzileta huku.
Ni nzuri sana ila ndefu balaaa na haijaaisha hapo!Mh sikuisoma ila naona nikiisoma kwa sasa itanishughulisha nikitulia ntaisoma
Ipo njema sana ilaaa uwe na muda hapo mwanzo unaeza usielewe ila unavoendelea kuisoma unapata picha ni nzuri sana ukitulia isome sis!Asante ccy ngoja niisome pia
Sawa ccy asante sanaIpo njema sana ilaaa uwe na muda hapo mwanzo unaeza usielewe ila unavoendelea kuisoma unapata picha ni nzuri sana ukitulia isome sis!
Mi mwenyewe leo nimeshtukajee kukuta muendelezo nilishaisahaugi hata!UWii twafwaa maana hata content yote ilishapotea ngoja tuanze upyaaaaa
Thanx sisy
KItambo sana tupo busy na Mage..na AmirMi mwenyewe leo nimeshtukajee kukuta muendelezo nilishaisahaugi hata!
Kabisa akina Mage wamejua kutushikaKItambo sana tupo busy na Mage..na Amir
Taabu tupu.nimesoma hata sikumbuki yupi ni yupi sababu unaikawiza mno