Tukidhani ni Binadamu wenzetu, kumbe ni mashetani! Mtu unaombeaje mwenzako afe kwa Corona? Can't believe this wickedness! Huu sio utu, ni ushetani!

UKIONA HIVYO JUA KUNA CHANZO.
Bashite na pole pole walitoa matamko yasiyostahili kutolewa na kiongozi wa ngazi zao.Hukukemea wala kulalamika!

Wamesemwa hao "viongozi" tegemewa(kwa mtazamo wako) unaona tatizo. Hao si Mungu na hata wakiondoka (kwa corona au vifo vingine) maisha yataendelea na watasahaulika kama binadamu wengine! Hakuna mwenye roho ya thamani mara 2 au zaidi ya mwingine. Kila mmoja ashinde mechi zake.
 
Mkuu umesema yote yaliyo moyoni mwako wala hukutaka kuwa mnafiki!!!!
 

Naona juhudi za kujiwekea nafasi nzuri ya kugombea nafasi bungeni
 
Pia humu kuna uzi ulodai kuwa lisu kaugua corona huko alipo watu wakashangilia pia hadi kusema afe kabisa, mzee mayala hakulalamika wala.
 

Kaka yangu Paskali, naelewa uchungu wako. Lakini jiulize kama hiki unachokiona leo (and you have absolutely rightly spoken against it) kingetokea wakati wa miaka 5 ya mwanzo ya utawala wa Kikwete (let alone waliotangulia)?

Who are the culprits? Ilianzishwa wakati wa Kikwete wakati kina Mwigulu wanalipua mabomu na kuua watu wasio na hatia viwanja vya Soweto kwa ajili tu ya kuzuia CHADEMA wasishinde uchaguzi wa marudio wa udiwani.

Magufuli alichokifanya ni kuongezea intensity ya tatizo ambalo ni mkakati wa kishetani wa ccm kubaki madarakani (na kumbuka kuwa Kikwete alituambia hadharani kuwa hata ccm kukubaliana na mbinyo wa kuruhusu vyama vingi "ulikuwa ni mkakati wa kuzuia watu wengi zaidi kuichukia ccm kwa kigezo cha kudai vyama vingi maana angalau kipindi hicho ccm ilikuwa inaungwa mkono na 80% ya Watanzania").

Unfortunately kwa ccm, muda huu Watanzania wengi ni waelewa na ccm wanajua kuwa kwenye uchaguzi huru na wa haki ccm LAZIMA itashindwa TU. Ndio maana bingwa wa kuogopa ushindani (Magufuli) anaogopa na kufanya ayafanyayo.

Paskali, naomba nenda ukawaambie watoto wa Azory, ndugu zake Ben Saanane, mke na watoto wa Tundu Lissu (na wengine wote walioumizwa) haya maneno uliyoyaandika leo halafu urudi kutupa feedback.

Sikubaliani na mtu anaemtakia mwenzake kifo, kiwe cha corona au ugonjwa wowote ule, ajali, kurogwa, kupigwa ngumi au risasi. Ila pamoja na hayo, anza kuwaambia watawala watubu kwanza. You can't keep on killing people and expect the victims' relatives to wish you well. Namuomba BWANA YESU WA NAZARETH ANISAMEHE na kutupa wote moyo wa kusamehe.
 
Boss Pascal Mayalla Post na Mada yako ni ya Kinafiki sana na mno, Wewe ni Gwiji wa Tasinia hii ya Habari, Tumia Kalamu yako Kuponya, Kuleta Umoja wa Kitaifa, Tumia Kalamu yako Kujenga.

Kuanza kulaumu wanoombea mabaya wenzao bila kuainisha sababu zao za kuombea mabaya wenzao ni kujishushia Heshima yako. Ulitakiwa ulete Uzi na Mada zinazo balance Mada yako au zinazobalance Issue.

Ukiangalia kwa mapana, na kitaalamu, watu wa aina uliyosema, hawasukumwi na wao wenyewe, lazima kuna kitu kinachowasukuma mpaka kufikia hatua ya kuombea mabaya wengine, ungepata muda wa kukaa nao chini na kuwauliza sababu, lazima utapata sababu ya maumivu, au wao wameumizwa yao au jirani zao au mtu wao au watu wao wa karibu

Sasa mada yako ingeshauri nini kifanyike ili hali hii isitokee tena, Kuwa Kiongozi si jambo dogo, Ukishajua Uongozi ni Dhamana basi mambo mengine yatakwenda vizuri. Kumbuka kwenye Jamii lazima utakutana na Watu wenye Mitazamo tofauti.

Unaweza kumlazimisha Punda kwenda Kisimani, lakini hauwezi kumlazimisha Punda kunywa Maji.



 
Mayala, waswahili wanamsemo usemao mazoea ubadirika kuwa tabia, watanzania tulikuwa na kuzoezwa upendo undugu na hata ungetoka mwanza ukaenda mbeya unajiona wewe ni mtanzania na huko Tanzania. Utukujibagua kwa ukabila wetu, rangi , dini hata siasa. Kila mtu alikuwa na haki ya kuuliza, kuhoji na hata kusema kile ambacho yeye alikiamini hata kama si kizuri kwa watawala ila asivunje sheria.

Lakini cha ajabu watawala ambao mungu kawapa dhamana ya nchi hii wakaanza kutugawa, nenda visiwani zanzibar kunawatu wanaitwa mazombe. Wanao uwezo wa kuua, kutesa lakini hawakamatwi. Bara wasiojulikana japo jamii inawajua.

Wanao uwezo wa kuua, kuteka na kutesa lakini watawala wanaangalia tu. Kwa ubinadamu ukisikia aliyekutesa jana kafa ama kaugua nadhani utafurahi. Mfano kunaviongozi wamewataja wagonjwa kuwa na korona waziwazi hakuna aliyejaribu kukemea hata walio juu yao. Lakini leo hii kunawatu wana kesi za kutoa taarifa na wengine wamefungiwa hata kuandika. Chuki ni zao la dhuruma na haki ni zao la upendo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…