Donnie Charlie
JF-Expert Member
- Sep 16, 2009
- 16,908
- 19,123
We si muumini wa 'karma'? Nadhani uzi wako upo indirectly..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nyuzi nyingi zinazohusu siasa mara nyingi umekuwa upande wa kutetea serikali na ni jambo zuri. Lakini mazuri kwa unayempenda ni kumuweka kwenye mstari wa sawa ikiwa kama anakosea. Mifumo inaongozwa na watu na asili ya sisi watu ni mapungufu.Mimi siombei mtu kifo, ila namkumbusha tu huyo bwana kuwa kuna watu walisimama mstari wa mbele kuitetea Tanzania walirudi wakiwa vipofu wengine,
Ndiyo unafiki wenyewe Mkuu. Wanafikiri matatizo wameumbiwa wengine. Sasa kwanini watu wasifurahi pale Mungu wao anapowaadhibu maadui zao??Vipi kuhusu yule aliyewafananisha watanzania wenzake na corona, yeye mbona ulikaa kimya
Kama zilikua ni za kupikwa jamii forums ni jukwaa huru na hata majina tunayotumia humu ni BANDIA hebu tupe takwimu za kweli zinasemaje?Ukweli ni kwamba taarifa zilizokuwa zinztolewa hazikuwa sahihi, (Ummy Mwalimu anajua), kwa hiyo kusema eti kuna award tunataraji ni uzwazwa wako tu, ilibashiriwa kwamba walikuwa wanajaribu kuficha ukweli ili kujidanganya kwamba maambukizi yako chini tanzania, ni ujinga kuficha jambo ambalo liko wazi, tunapima kizembe, tunaficha taarifa halafu watu wakisema wana hofu na taarifa hizo za kupikwa wanakamatwa na jeshi la polisi, endelea kuwapumbaza hao viongozi wenu uchwara muone mwisho wake
Unataka kusema nini ndugu? Tuliza akili ndio uandike ujumbe wakoWengine Hawa apa wamepewa kazi ya kuzka watu wanao kufa kwa Corona kina MBOWE utasema wanawazia matako Yan mtu et serekal inaficha ila wao wanajua sababu wao ndio wanazika IV mbowe mtaacha siasa Lin na kudanganya watu ao watanzania wanao kufa kwa ma mia wako wap? Na mliwazikia wap
Sent using Jamii Forums mobile app
Haya endelea kudhani...Sidhani kama unanizidi kipato mzee...BTW hata chama sina,mimi ni mdau wa serikali tu.
Hiyo rushwa nimeanza kula lini,...Mimi bado kijana rika la kawaida tu..,sifanyi kazi hata huko serikalini...ni mdau wa serikali;namaanisha nina sapoti serikali iliyo madarakani,si chama..,ni tabia yangu toka utotoni...serikali yoyote ile hata chama gani kikiingia madarakani ntasapoti tu,japo maovu ntayakemea.Ukiona hivyo utajiri wako ni wa mashaka na ni mla rushwa mkubwa hakuna mwenye kipato kizuri akalipa kodi ya halali na kujikomba kunifanya mdau wa serikali
Sent using Jamii Forums mobile app
Unaweza ukawa umenizidi pia... Ila mimi sio wa kupewa sijui 7000 au 7800...Hiyo hata kwa chakula cha siku hainitoshi na usingle wangu huu,lol.Haya endelea kudhani...
Hata Levy Mwanawasa alikufa akiwa madarakani na Zambia ipo inaendelea. Wao sio Mungu kwamba wakifa na nchi inakufa.UKIONA HIVYO JUA KUNA CHANZO.
Bashite na pole pole walitoa matamko yasiyostahili kutolewa na kiongozi wa ngazi zao.Hukukemea wala kulalamika!
Wamesemwa hao "viongozi" tegemewa(kwa mtazamo wako) unaona tatizo. Hao si Mungu na hata wakiondoka (kwa corona au vifo vingine) maisha yataendelea na watasahaulika kama binadamu wengine! Hakuna mwenye roho ya thamani mara 2 au zaidi ya mwingine. Kila mmoja ashinde mechi zake.
Jiulize nini kimetufikisha hapo?? Kwakweli hata mimi natamani watu fulani ianze nao kwanza. Sema ni vile tu haichagui.Wanabodi,
Mtu unachokiandika, ndicho unacho kiwaza!, kuna watu, tunaishi nao, tunakula nao, tunalala nao, tukidhani ni binaadamu wenzetu, kumbe ni machoni tuu ndio kama watu, lakini mioyoni ni mashetani wakubwa!. Mtu unaombeaje binaadamu mwenzako afe kwa Corona?!. Can't believe this wickedness imewakuta Watanzania wenzetu!. Huu sio utu, sio ubinaadamu, ni ushetani!
Unaweza usiamini hili ninaloandika hapa lakini ni kweli kabisa, wakati dunia ikihangaika na janga la ugonjwa wa Corona linaliitesa dunia nzima tukiwepo sisi Tanzania, kuna baadhi ya wenzetu humu mitandaoni utu na ubinaadamu umewatoka wamekuwa sio watu tena, sio binaadam bali ni mashetani kwa kuombea wenzao sio tuu wapate Corona, bali wapate Corona na wafe kwa vifo vya Corona!.
Hili nimelishuhudia humu jf na mitandao mingine baadhi ya wenzetu waki andika ku wish wenzao wapate Corona na wafe kwa Corona kwa wengine kuwataja kabisa kwa majina mimi nikiwa ni mmoja wao na wengine kuwataja kwa majina ya utani au hata bila kutaji jina ula unajua ni nani!.
Lengo la bandiko hili sio mimi kulalamika kuwa kuna watu wananitaka nipate Corona, kwasababu mimi ni nobody, hata nikichomoka na Corona, it's only my wife, my kids na my family ndio wata suffer, bali kuna watu very wicked wana wish viongozi wetu fulani fulani wafe kwa Corona, kutokana na positions za hao viongozi, ikitokea kweli wakachomoka kwa Corona, taifa tuta suffer kwa kupigwa na double tragedy!.
Mimi ni miongoni mwa Watanzania wenye uwezo wa kitu kinachoitwa graphology ni uwezo wa kusoma maandishi ya watu, kisha ukabaini mwandishi alimdhamiria nini, hata akiandika neno "bora tuu afe kwa Corona ", bila kumtaja ni nani, kupitia graphology unajua ni nani alidhamiriwa afe!, japo huyo mwandishi anaweza kuwa hakuandika kwa kumtaja jina expressly kuwa nataka fulani afe kwa Corona, lakini kupitia uwezo huo wa graphology, then unatambua impliedly aliyedhamiriwa ni nani!.
To wish someone specific afe kwa Corona ni highest stages of wickedness, Watanzania siku zote ni watu wenye upendo, tunapendana na tunawapenda viongozi wetu, na hata chama chetu japo tunakilalamikia sana humu mitandaoni kuwa ndicho chanzo cha umasikini na madhila yote yanayolikuta taifa letu, lakini in reality, tunakipenda sana na kila mwaka huwa tunakichagua tena na tena mwaka hadi mwaka, na kama janga la Corona halitadumu muda mrefu na kuleta madhara makubwa, then mwezi October, 2020, tunakichagua tena, sasa iweje binadamu wenzetu, Watanzania wenzetu kuingiwa na roho ya ushetani wa ajabu kwa kuwa na wishful thinking ya kuombea viongozi wetu fulani fulani tegemewa, wafe kwa Corona?!.
Ajabu kubwa zaidi ni idadi ya members watakao toa likes kwa huyo mtu, inaonyesha jinsi tulivyo na kundi kubwa Watanzania wenzetu ambao ni wicked kwa kusupport hizo wicked ideas!, na kipimo rahisi kwa mashetani hawa, utakiona kwenye uchangiaji kwenye hili bandiko.
Swali la kujiuliza hivi ni kweli Watanzania watu tuliiokuwa na upendo wa ajabu zaidi hata ya upendo wa mshumaa, wa kumulikia wengine huku kwako unateketea, sasa tumefika hapa kuombeana vifo vya Corona?. Huu ni utu, ni Ubinaadamu au ni ushetani wa ajabu?.
Hivi kweli sisi Watanzania tumefikia stage ya kuishi na binadamu wenzetu wenye mawazo ya kishetani kama haya halafu tunaishi nao tukiendelea kula nao, kunywa nao na kulala nao na wengine hadi tunawapongeza!, hivi ushetani huu unatofauti yoyote na ule ushetani wa Sodoma na Gomorrah?!.
Ingekuwa kila kitu mtu anachokiwaza kinaandikwa kwenye paji la uso wake, hivyo nikikuambia ufunge macho na kuwish ulitaka mtu gani afe kwa Corona, amini usiamini, watu tungekuwa surprised kukuta mke ana wish mume ndio afe, mume ana wish mke ndio afe na nikiuliza ungewish kiongozi gani afe kwa Corona, majibu yangekuwa yanaandikwa usoni!, watu mngeshanga na ungeweza usiamini!.
Tiba Nambari One Duniani ni Imani, yaani faith, kwa janga kama la Corona ili liishe na lisilete madhara makubwa na maafa kwa Tanzania na duniani kwa ujumla, ni kama Watanzania na watu wote, ikiwa wote tuta wish kwa dhati ya mioyo yetu kumuomba Mungu kwa dhati, alipishie mbali, hili janga la Corona, lakini kitendo cha wengine tunasali, na kumuomba Mungu atuepushe na janga la Corona, huku kuna wenzetu wengine wao waki wish fulani apate Corona afe, kunapunguza nguvu ya sala zetu, huu sio Ubinaadamu, sio utu, ni ushetani!.
Hala hala kwa mashetani hawa, ingekuwa dua ls kuku linampata mwewe, saa hizi siku nyingi kuna watu tungekuwa ni historia, lakini Mungu sio Athumani, kila mtu atakufa siku yake Mungu aliyompangia tena kwa kifo kile kile mtu ulichopangiwa, kama mtu umepangiwa kufa kwa Corona, utakufa tuu kwa Corona and no one can do anything kuzuia, ili kitendo cha mtu kumwish mtu fulani afe kwa Corona, sheria ya karma my act kwa kanuni ya what goes around, comes around, wakati uki wish fulani afe kwa Corona, karma may act upon you na ku reverse your wishes on opposite directions, hiyo wish ikakurudia wewe na familia yako!.
Tupendane wandugu, na tuwishiane mema!.
Mungu Ibariki Tanzania
Mungu wasamehe Watanzania wenzetu waliomkaribisha shetani ndani yao na umtume Roho Mtakatifu wako, awasafishe na kuwatakasa with their evil thoughts and wickedness na kuliepusha taifa letu na janga la Corona.
Amen.
Paskali
Wameumizwa mioyo na kujeruhiwa miili na nafsi ko watesi wao wakitembea mbele kwa covid nao watapumua na kupata ahueni maana haingii akilini mtu anakutesa afu uache kumuombea mabaya ili atoweke na wewe upate nafuuHili jambo nimeliona sana humu...Achana na hilo, kuna wengine hata nyuzi za tanzia wanaonekana kufurahia....limenistaajabisha sana hili.