Tukidhani ni Binadamu wenzetu, kumbe ni mashetani! Mtu unaombeaje mwenzako afe kwa Corona? Can't believe this wickedness! Huu sio utu, ni ushetani!

Mimi siombei mtu kifo, ila namkumbusha tu huyo bwana kuwa kuna watu walisimama mstari wa mbele kuitetea Tanzania walirudi wakiwa vipofu wengine,
Nyuzi nyingi zinazohusu siasa mara nyingi umekuwa upande wa kutetea serikali na ni jambo zuri. Lakini mazuri kwa unayempenda ni kumuweka kwenye mstari wa sawa ikiwa kama anakosea. Mifumo inaongozwa na watu na asili ya sisi watu ni mapungufu.

Serikali yetu kwa miaka imekuwa ikifanya madhaifu mengi tena ya waziwazi ambayo ni yenye madhara kwa raia mmoja mmoja, mengine kwa wote na yana athiri nchi kwa ujumla. Suala la uchama liweke kando kwa sababu binafsi si mfuasi wa chama chochote bali mafungamano yangu ni kujitahidi kuishi kwa kadri niwezavyo kwa kuyaendea yale ambayo Mungu ametutaka tuyatende.

Nakuusia ndugu yangu pamoja na kuiusia nafsi yangu, ukiona heri limefanywa na yoyote lifurahie na lipongeze! Ukiona shari immefanywa na yoyote usione haya kukiri na kutafuta njia bora ya kulitengeneza liwe zuri, imma kwa kumwambia aliyekosea kuwa hapo umekosea! Akilifuata ni yeye na akiliacha ni yeye. Wewe hauna dhima tena kwani umeshfikisha kilichotakikana.

Kumbuka wa-Tanzania tupo takribani millioni 50. Ikiwa kama kiongozi akifanya dhulma kwa wa-Tz asifikiri kwamba amefanya dhulma kwa nchi! Bali amefanya dhulma kwa watu millioni 50. Na yeyote atakayeiunga mkono hiyo dhulma naye yumo kwa kuwadhulumu watu millioni 50. Sasa ndugu unamema kiasi gani cha kufidia idadi ya watu millioni 50? Ikiwa kama wamefanya dhulma x10 na wewe ukai support zidisha mill 50*10... Ila ni vipi hayo ikiwa unayafanya kwa heri? Tumuogope na tumukhofu Mungu! Mungu anatisha jamani! Haya mambo ya kidunia yasitupumbaze!

Mungu atuongoze kwenye kheri.
 
Vipi kuhusu yule aliyewafananisha watanzania wenzake na corona, yeye mbona ulikaa kimya
Ndiyo unafiki wenyewe Mkuu. Wanafikiri matatizo wameumbiwa wengine. Sasa kwanini watu wasifurahi pale Mungu wao anapowaadhibu maadui zao??

Kuna matatizo ya kutengenezwa na binadamu kwa mwenziye. Mf Yaliyomkuta Mh Lissu sote tunafahamu. Sasa inapotokea watesi wake wamepatwa na corona kisha wakadanja unategemea wafuasi wake watasikitika au watashangilia na kumtukuza Mungu wao kwa kujibu maombi yao??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mshahara za dhambi mauti bali karama la Mungu ni uzima wa milele!! Pasco nimewahi kuandika kwenye moja ya mabandiko yako kuwa utawala wa awamu ya tano umejenga chuki ya kiasi kisichomithirika miongoni mwa watanzania! watu wa Mungu tunatakiwa kuwatatkia watu mema hata wanaotuudhi lakini inahitaji moyo wa neema kuishi katika level hiyo!

hawa wanaoombea wengine wafe ni wale ambao wanajihisi kuwa helpless chini ya utawala huu wa mkono wa chuma lakini kwa upande mwingine kuna kundi ambalo kila siku wanasondeka watu ndani kwa kesi za ajabu ajabu, wanawapoteza watanzania wenzao au kuwaiga risasi kwamba yeyote mwenye mtazamo tofauti na wao huyo ni wa kufa kupotea au kuozea jela kwa kifupi chi yetu sasa ina hayo makundi mawili na kama hatutapa kiongozi mfariji wa kuturudisha pamoja kuna suala zima la ukabila pia linakuwa kwa kasi sana!
 
Kama zilikua ni za kupikwa jamii forums ni jukwaa huru na hata majina tunayotumia humu ni BANDIA hebu tupe takwimu za kweli zinasemaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unataka kusema nini ndugu? Tuliza akili ndio uandike ujumbe wako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Paskali navyojua mimi wewe ni mhandishi huru,sio mfanyakazi wa serikali hii ya Magufuli. Kwa hiyo sio msemaji wa serikali hii.Wasemaji wapo.

Wacha serikali ijitetee yenyewe.Kwani ndio inawajibika kwa wananchi.sio wewe. Sana sana wewe ungedai transparency katika hilo swala la Corona.

As pressman ungedai press conference na vigogo wa serikali at least twice a day.
Unaona Free world jinsi press inavyo wahenyesha watawala na mabingwa wa tiba.
Hawa unaowatetea sio masultani,tumewaandika kazi WATUTUMIKIE si vinginevyo.

Wanaposhindwa kulitambua hilo wanapoteza sifa za uongozi.Sijui kwanini wasianzie kusotea uongozi Kivukoni ili wajue majukumu na miiko ya uongozi ni nini?
 
Ukiona hivyo utajiri wako ni wa mashaka na ni mla rushwa mkubwa hakuna mwenye kipato kizuri akalipa kodi ya halali na kujikomba kunifanya mdau wa serikali

Sent using Jamii Forums mobile app
Hiyo rushwa nimeanza kula lini,...Mimi bado kijana rika la kawaida tu..,sifanyi kazi hata huko serikalini...ni mdau wa serikali;namaanisha nina sapoti serikali iliyo madarakani,si chama..,ni tabia yangu toka utotoni...serikali yoyote ile hata chama gani kikiingia madarakani ntasapoti tu,japo maovu ntayakemea.
 
Si afadhali hata hao wanaoombea wengine wapate au wafe kwa covid19. Vipi wale ambao kwa kiburi chao cha madaraka, sasa watu wanapoteza maisha kwa hiyo hiyo corona? Tuwape jina gani?
 
Hata Levy Mwanawasa alikufa akiwa madarakani na Zambia ipo inaendelea. Wao sio Mungu kwamba wakifa na nchi inakufa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jiulize nini kimetufikisha hapo?? Kwakweli hata mimi natamani watu fulani ianze nao kwanza. Sema ni vile tu haichagui.
 
Hili jambo nimeliona sana humu...Achana na hilo, kuna wengine hata nyuzi za tanzia wanaonekana kufurahia....limenistaajabisha sana hili.
Wameumizwa mioyo na kujeruhiwa miili na nafsi ko watesi wao wakitembea mbele kwa covid nao watapumua na kupata ahueni maana haingii akilini mtu anakutesa afu uache kumuombea mabaya ili atoweke na wewe upate nafuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…