Tukiendeleza kutumia nguvu kuwanyamazisha watu wanaohoji juu ya mambo ya kitaifa, tunatengeneza Taifa la hovyo na nchi kutekwa na adui

Tukiendeleza kutumia nguvu kuwanyamazisha watu wanaohoji juu ya mambo ya kitaifa, tunatengeneza Taifa la hovyo na nchi kutekwa na adui

ZALEMDA

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2017
Posts
1,956
Reaction score
2,225
Kipindi cha ukoloni, mkoloni hakupenda kabisa kuona watu wenye akili wakihoji. Kama Afrika isingekuwa na watu wenye kuhoji mpaka leo tusingekuwa tumejipatia uhuru.sehemu nyengine hawakupata uhuru kwa mtutu wa bunduki bali kwa hoja tu. TAIFA lenye watu wa kuhoji mana yake liko hai na linaonyesha kuwa linatoa high quality education siyo taifa mbumbumbu.Taifa la namna hiyo haliwezi kuvamiwa kiurahisi.

Kwa kunyamazisha maoni ya watu mbali mbali tunazamisha elimu yetu na kuhatarisha uhai wa taifa letu kwa sababu watoto wetu mashuleni hawatakuua na uwezo au kuona umuhimu wa kuwaza kwa undani zaidi juu ya maswala muhimu ya darasani hata ya kitaifa.yani no need of critical thinking.

TUNAJIHUJUMU WENYEWE na hatuwezi kuendelea kuiwa na nuchumi wa kati au kupanda zaidi kwenda kuwa nchi tajiri ulimwenguni.Ndiyo maana mimi binafsi nilipoona hayati JPM amejitahidi kuchagua viongozi wasomi niliona ni njia mojawapo ya kuipa value elimu yetu.Na napendekeza hapo badaye kama tukipata katiba mpya,mbunge angalau awe na degree ili akienda bungeni atunge sheria kwa kutumia critical thinking na siyo ndiyo mzee.

Tujenge utamaduni wa kujibu hoja zinapotolewa.iwe mojawapoa ya job decription katika maofisi yetu.ukishamjibu mtoa hoja anayo wajibu wa kukubari majibu au kukataa lakini mwisho wa siku watu wataweza kupima pande zote mbili kuwa huyu kajibu vizuri au huyu anayekataa majibu ni mkolofi tuu.LABDA JESHINI NDIYO TWAWEZA KUITIKA NDIYO AFANDE ,lakini sehemu nyengine tuwaache watu waseme na tuwajibu Kwa ufasaha.

Tuendelee kujenga taifa imara zaidi

Asanteni
 
Kujibu hoja kama zipi ungefafanua
 
Mleta mada pamoja na uandishi wako kuwa wa mashaka sana huku ukitaka mbunge awe na degree na mastaz na Phd au Profesa hiyo ni shida ya utumwa wa akili.

Mleta mada kifupi hujaeleweka hata chembe kwa sababu labda ungesema nani kanyamazishwa leo asiongee, kilamtu amesikika akipongeza uhuru wa vyombo vya habari, na mama amepongezwa mpaka na wapinzani, vyombo vilivyofungiwa vimefunguliwa ebu wewe tufafanunulie. Maana hata wewe umeandika tumekusikia.

Mara unasema watu wajibiwe maswali ofisini yaani hapo ndiyo umetupoteza zaidi kwa sababu ofisi huwa ni sehemu ya kazi sasa kama wewe unaona ofisi kuwa ni sehemu ya kuulizana maswali basi unatatizo.
 
Mleta mada pamoja na uandishi wako kuwa wa mashaka sana huku ukitaka mbunge awe na degree na mastaz na Phd au Profesa hiyo ni shida ya utumwa wa akili...
mbunge kuwa na degree hapo kuna utuma wa akili kiviiipi?kuhusu kujibu hoja maofisini nilikuwa namanisha kuwa kuwepo kitengo cha kujibu hoja au ajibu aliyeulizwa
 
Nimekupata vema!Gwaji boy alitakiwa kujibiwa si kukimbilia kumkamata.
 
Mie nafikiri kwamba, taifa litaweza siku zote kupata maendeleo ya kweli, inabidi liwe na wananchi wanaoweza kuwa na hulka ya ' kuhoji' na na kupewa majibu sahihi kwa masuala muhimu yahusuyo taifa lao, bila ulazima wa labda kujibiwa na vitisho kwa mustakabali endelevu wa taifa hilo......
Nimekupata vema!Gwaji boy alitakiwa kujibiwa si kukimbilia kumkamata.
 
Mbowe amepewa kesi ya ugaidi kwa kushinikizwa mabadiliko ya katiba
 
ati kwamba ukichanja na ukipima voltage kwenye bega ulilochoma inasoma ukigeuza ambalo haujachoma haisomi.
Hahahhahaha daaah akili zingine bana kuna wengine wanasema Chanjo inabadili DNA daah sasa hawa tu utawajibu nini.
 
Back
Top Bottom