NAWAZA kivingine. Haya ni mawazo tu namna tunaweza kutoka hapa tulipo kama nchi na mama hii kitu inamharibia sana wananchi walianza kumpenda sasa wanalia na tozo.
Tanzania Naipenda.
- Boresha Bandari yako, Punguza ushuru wa Magari ya kuanzia mwaka 2013-2018 watu wataagiza wengi na serikali itapata hela nyingi.
- Jenga Viwanda vingi kwa kutafuta wawekezaji wengi kwa sbb tayari raw material nchi hii tunayo ya kutosha utapata kodi nyingi
- Punguza misafara isiyo ya lazima. Ukiwa na ziara nenda na watu wachache tu
- Badilisha mfumo wa kununua magari. Magari kama V8 yawe kwa Waziri Mkuu tu Mawaziri Wakuu wa Mikoa na Viongozi wote Serikalini wanunulie VANGUARD zinawatosha
- Punguza Safari za Nje, Tumia Mabalozi, Safari za nje safiri zile tu mnaenda kuweka Mikataba. Mikutano Mtume Waziri mkuu hana msafara mkubwa
- Punguza Warsha Serikalini ambazo sio za Lazima
- Wekeza kwenye tehama kila kazi serikali ziwe kwenye mfumo
- Punguza baraza la mawaziri liwe dogo. Naibu Waziri na Naibu katibu hawana kazi
- Punguza Idadi ya Wabunge bungeni
- Ongeza UShuru kwenye Bia ni starehe watu hawanywi kila siku
- Safirisha Mizigo kupitia reli badala ya barabara
- Tutengeneze PikPiki na Bajaji tuuze kwa nchi majirani ni technolojia rahisi
- Uza Nyama Nje ya Nchi
- Uza Maziwa Nje ya Nchi
- Ondoa Mikutano ya chama peleke pesa vuta mabomba ya maji kutoka Ziwa Tanganyika kuja miko yenye shida ya maji na ziwa Victoria.
- Jenga Kutumia FORCE ACCOUNT tumia JKT
Tanzania Naipenda.