Tukifanya Hivi, Kina Mwamposa na Manabii kuwa Walipa Kodi Wakubwa

Kwenye jumuiya ROMAN hatupangiwi kiwango kwa kaya?
Njoo Arusha uone
 
Kwenye jumuiya ROMAN hatupangiwi kiwango kwa kaya?
Njoo Arusha uone
Unajaribu kukwepa hoja yako ya mwanzo.Nakukumbusha umesema hivi "Mwamposa anaweza kuwaambia waumini watoe 5000 ili awape maji,mafuta au komuniyo bure" Hoja ipo hapo.Kanisa Katoliki linapangia watu kiasi cha kutoa kwa kila Jumuiya kulingana na ukubwa wa Jumuiya.Kiasi gani kila kaya itatoa itategemea na mgawanyo wa wanajumuiya walioko kwa hiyo Jumuiya.Kiwango kinachopangiwa Jumuiya kutoa siyo sadaka ya jumapili ili wapate komuniyo bali ni michango mbali mbali kulingana na uhitaji wa Kanisa mahalia.Hii ni utaratibu upo pote kwa Majimbo yote yaliyopo chini ya TEC.
 
Unachoita utaratibu wa kaya kupewa kiwango cha iite mchango au sadaka ni hicho hicho kilichopo kwa mwamposa.Kununua ushirika na MUNGU kwa hela.
Mwamposa anasema toeni 5,000 kusaidia kuendesha huduma..atawapa maji
Askofu, Ruwaichi atasema toeni 20,000 kila kaya kuendesha kanisa..atawapa komunyoo.
 
Sio chuki ndugu
Anachokifanya kinaonekana kiko kibiashara....awaambe watu waje na maji yao ayaombee warudi nayo makwao.
Vinginevyo inakuwa biashara alipe kodi ikiwa sheria itamwi giza kwenye wigo.
Mapadre , masister, wachungaji walipe Kodi za PAYE
Hajakataza hilo mbona.......sio kila muumini atakumbuka au atataka kubeba maji kutoka nyumbani hivyo kawasogezea tu huduma.

Alafu hiyo pia ni sehemu ya sadaka ili kuwezesha huduma yake iendeleee kuwepo.
 
Kwa Kanisa Katoliki,je yule ambae hajatoa kabisa atanyimwa komunio? Na kwa Mwamposa yule ambae hajatoa hiyo 5,000 atapewa maji hata kama anayahitaji?
 
Ni vigumu mno na haiwezekani kutoza kodi katika mtindo unaofanywa na akina Mwamposa!

Labda Imani hizo zifungiwe! La sivyo haiwezekani kodi kulipwa ktk mtindo huo!

Akiona mnampelekesha" anaamua kuwagea bule walio toa sadaka! Mtamfanyeje?
 
Na pale posta kuna TRA kuna siku niliagiza USB moja tu ya Elfu 10 wakataka kunitoza kodi
Nikaagiza Dongle ya kuflashia simu kwa 120k wakanipiga kodi 60k

Hili nalo unalizungumziaje???
 
Kwa Kanisa Katoliki,je yule ambae hajatoa kabisa atanyimwa komunio? Na kwa Mwamposa yule ambae hajatoa hiyo 5,000 atapewa maji hata kama anayahitaji?
Yule ambaye hajatoa michango, sadaka ya jumuiya hatanyimwa komunyoo.

Atanyimwa kubatizwa mtoto, komunyoo ya Kwanza na kipaimara kwa mtoto, huduma ya mazishi kwa kufika padri, kufangashiwa ndoa kama hawajafunga.

Kwa mwamposa: Asiyetoa 5000 hatanyimwa maombezi na kusali.
Atanyimwa maji
 
Na pale posta kuna TRA kuna siku niliagiza USB moja tu ya Elfu 10 wakataka kunitoza kodi
Nikaagiza Dongle ya kuflashia simu kwa 120k wakanipiga kodi 60k

Hili nalo unalizungumziaje???
Kodi inatozwa kwa sheria, ikiwa Sheria iliyotumika haikuwa sahihi unakata rufaa huko TRAB/TRA kwa Mwigulu mpaka Court of Appeal.
Kwa hali yako nipe full scenario kabla sijawahukumu maofisa wa TRA waliokutoza hiyo kodi
 
Sijawahi kuona mtoto amenyimwa kubatizwa kisa Mzazi hajatoa michango.Siku ya Boxing day Jimbo letu limebatiza watoto wadogo na haikujalisha umetoa michango ama la.Wewe unachanganya hapa kati ya kuhudhuria kwenye Jumuiya na kutoa michango,ni vitu viwili tofauti kabisa.Kuna waumini ni wahudhuriaji wazuri tu wa Jumuiya lakini hawana uwezo na wanajumuiya wanawafahamu vizuri na hupewa huduma zote za Kikanisa wanapokuwa na uhitaji.
 
Njoo Arusha,
 
Woote mwamposa , Catholics ni wafanya biashara wanaotumia mifumo, call them modalities tofauti.
Nimeeleza hapo juu, na hizi modules zao za biashara ni out of our Tax laws scope
 
Nashukuru kufahamu kuwa naongea na mkatoliki mwenzangu, muundo wa kanisa katoliki ni tofauti na hayo madhehebu mengine ya kiprotestanti.

Upadre ni wito ndio maana siku ya upadrisho wanalala chini pale kanisani wakitafakari juu ya maamuzi yao watakayoyaishi maisha yao yote yanayobakia ni tofauti na hao maaskofu ambao hata elimu zao wamezipatia wapi haijulikani.

Maaskofu hao wanafaidika na jamii iliyo desperate katika kupiga pesa ndefu, wanaambiwa wakung'ute kabisa mifuko yao kabla hawajaondoka.

Kero ni kwamba wao wanaondoka kwa miguu kurudi makwao wakati maaskofu hao wa kisasa wanaondoka na magari yao ya bei mbaya kurudi makwao tena wameyanunua kwa pesa hizo hizo za waumini.

Maisha ya mapadre kwa ujumla wao yanatokana na sadaka zetu hivyo hawana jeuri ya kuishi kifalme wakiwa chini ya umiliki wa parokia wanazofanyia kazi.

Kagame na Ruto wapo very right kutetea mamilioni ya raia wanaofanywa watumwa wa biashara yenye jina la Mungu, wanachofanya ni sawa kabisa wakiwatetea raia wao walio mateka ya wafanyabiashara wa dini wa miaka ya sasa.
 
misikiti hapo haihusiki mjomba umejichanganya.
 
Ulicho kiandika ni upupu hukufanya utafiti au huna uelewa wa Kodi. Mwamposa ana kiwanda chake Cha maji na mafuta ambacho kimesajiliwa na kinalipa Kodi. Ni sawa na wew kutengeneza kiwanda chako Cha mbolea Kisha kuamua Ile mbolea kuipeleka ktk mashamba yako. Serikali haiwez kuja kukudai Kodi tena kwa kuwa mbolea Ile uliyo lipia Kodi umeitumia shambani na mavuno yamestawi vizuri.

Kodi yao wataipata kiwandani ktk uzalishaji Ile Mwamposa anatoa ni huduma ya kiimani pia ujue mashirika ya Dini zote hpa nchini yamepewa msamaha wa Kodi kwa vitu mbalimbali kisheria Wanavyo viagiza nje ya nchi.

Mbona tukipita Misikitini huwa tunaona kanzu, kofia, madawa mbalimbali ya kienyeji amabyo waislamu wanauziwa na hakuna anaye lalamika kwa nini wawauzie hivyo vitu Misikitini na Wala huwa hatuoni mashine za EFD?

Tuache mihemko na wivu wa kimasikini.
 
Woote mwamposa , Catholics ni wafanya biashara wanaotumia mifumo, call them modalities tofauti.
Nimeeleza hapo juu, na hizi modules zao za biashara ni out of our Tax laws scope
Unaweza kulifanyia hesabu kanisa katoliki kila senti ukajua inakwenda wapi na inatumika vipi tofauti na hao kina Mwaposya na wa aina hiyo.

Ipo nidhamu ya uendeshaji wa kanisa katoliki ambayo haipo katika makanisa hayo mengine.
 
Nakuunga mkono!
Ajabu ni pale watu wanamkagua Mwamposa wanasahau mapadre ,Masister hawalipi PAYE wakati sadaka zetu ndio kipato Chao, otherwise watuambie wanaishije ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…