Tukikubaliana na dhana za kuikejeli elimu kisa Profesa Muhongo kakejeliwa tutapotea kama Taifa

Tukikubaliana na dhana za kuikejeli elimu kisa Profesa Muhongo kakejeliwa tutapotea kama Taifa

Sisi ni Taifa ambalo ..Mganga WA kienyeji ambae ana tangaza dawa hadi za kufuta kesi..

Kitu ambacho ni Sawa na kutangaza kulinda wahalifu... Mganga huyo anagombea hadi ubunge na kushinda...

Taifa ambalo waziri wa afya anaunga mkono kuacha kupima corona na kuita media kutangaza chachandu ya ndimu kama dawa ya Corona...

Msukuma ni zao la jamii ambayo tunayo..
Upumbavu wa halaiki
Umenikumbusha Marehemu Profesa Chachage.
 
Alichokisema msukuma yupo sahihi kabisa maana tunao ma professor uchwara..
Imagine mtu kama ndalichako et nae professor
 
Kama professor kazingua acha aambiwe ukweli mda mwingine wasomi tuliowasomesha kwa kodi zetu hutugeuka Watanzania kwa maslahi yao binafsi huku rasilimali zetu zikiporwa na Mabeberu.
Hilo ni jambo tofauti, mheshimiwa. Elewa mada. Musukuma, darasa la 7, ndiye hawezi hata kuelewa jinsi ya kupambana na mabeberu. Rais Magufuli alipounda zile timu 2 za madini hakuweka hata mtu 1 anayefanana na Musukuma au Kibajaji. Wote ni wasomi wanaoelewa madini, uchumi, sheria, negotiation, na mifumo ya kodi. Mada ndiyo hiyo; tunawahitaji akina Muhongo kwa kuielewa dunia ya sasa. Ila mimi nawakubali akina Musukuma kwa kutukumbusha tulikotoka zamani na kutuchekesha
 
kosa ni pale elimu inapochanganywa na siasa, hawa wasomi wamekubali kutumika na hao wanasiasa inafika wakati wanaupindisha ukweli ili kuwafurahisha wasiosoma sasa nyakat zinafika wanarudi ktk uelewa wao hao wanasiasa wanajikuta hawana ufahamu wa kinachozungumzwa na wasomi,waache washambuliane sasa wenyew kwa wenyew
 
Hizi dharau hazijanzia kwa hao darasa la Saba, dharau zimeanzia kwa Wasomi wenyewe kwa kutoheshimiana wao kwa wao..,
Alichokisema Msukuma ni mwendelezo tu..,
Wasomi ndio wanawadharau sana wa darasa la saba- Mh. Musukuma anajikinga tu na kipigo
 
Alichokisema msukuma yupo sahihi kabisa maana tunao ma professor uchwara..
Imagine mtu kama ndalichako et nae professor
Wewe na Musukuma tuonyesheni kuwa katika michango ya uboreshaji wa maendeleo ya kisasa wale sio maprofesa bali ninyi.
 
Bado tuna sisitiza, Wasomi waongee Kama waelevu na waweze kueleweka in simple terms, mfano hapa Tanzania tuna umeme wa Gas, wa Hydropower, wa Solar, Wa upepo na wa mafuta
Ivi katika mazingira ya uwepo wa hizi project ilishindikanaje hoja ya Muhongo kutetewa kwa tafiti ili asionekane muongo?
Wakati mwingine wasomi wanajidhalilisha wenyewe kwa kujipendekeza kwa Wanasiasa ili wapate vyeo na mali. Hapangekuwa na haja ya professor yule kujiita takataka wala kusema marehemu Magufuli alimwokota jalalani. Ni kujidhalilisha na kudhalilisha elimu yake. Wajinga kama Msukuma (ujinga sio tusi! ni mtu asiye na elimu) wanapata uhalali wa kuwatukana. Unaona proffesor yule kwa hofu na kutojiamini akamwita marehemu yule, "Mheshimiwa Mungu.....!) Ngoja wanyanyaswe na wajinga wa darasa la saba.
 
Mheshimiwa Msukuma amepata umaarufu mkubwa siku za karibuni haswa kwa kumkejeli Profesa Muhongo mwenye kuamini kwamba umeme wa gesi ni suluhisho la suala zima la nishati hiyo. Ni mawazo ya Profesa Muhongo na anao uwezo wa kuyatetea kwa hoja kila anaposimama na kuongea bungeni.

Naona kama Msukuma anakwenda mbali sana anapoamua kumkejeli Profesa na akawaweka katika kundi moja maprofesa wote kwa kigezo cha kutokubaliana tu na mitazamo yake. Ujinga ni mzigo mzito sana na upo uhakika hao mabilionea na mamilionea wanaojulikana kila kona wanawategemea wasomi wenye elimu za juu.

Tutakuwa tunapotea kama Taifa tukianza kukubaliana na dhana hizi za darasa la saba kuwa na manufaa na mafanikio kiasi cha wenye elimu kubwa kuanza kuonekana hawana maana. Ni kosa kubwa sana tutakuwa tunalifanya.

Wanaokesha usiku ndani ya maabara kubwa za mataifa yaliyoendelea wakitafuta kila aina ya chanjo dhidi ya Covid19 ni wasomi wa viwango vya juu. Na matokeo ya elimu zao wameanza kuzaa matunda kwani miezi michache ijayo dunia kwa maana ya ile ya watu kuchanganyika wakifanya shughuli mbalimbali itaanza kurudi kama ilivyokuwa zamani.

Wanaoandika ilani na kuwawezesha wagombea wanaopanda majukwaani ni wataalam wa fani mbalimbali. Hivyo Msukuma kuwepo kwake mle bungeni ni matunda ya hao hao wasomi anaowakejeli kisa tu ametofautiana kimtazamo na Prof Muhongo.

Ujinga kama alivyowahi kusema Hayati Mwalimu Julius Nyerere pale Karimjee miaka ya nyuma ni sawa na uchi wa akili. Ndio sababu hata wanamichezo ambao wanafanikiwa wakiwa na elimu ndogo, wakishapata pesa za kutosha huamua kutafuta elimu ambayo waliikosa hapo kabla, lengo ni kuuvalisha nguo ubongo.

Wenye elimu ya darasa wanaoweza kufika alipofika Mheshimiwa mbunge Msukuma ni wachache sana. Na sekta zetu nyingi zimekuwa zikikwama kwa kukosa maarifa sahihi ya wakati husika. Uendeshaji wa taasisi zetu nyingi ukiuchunguza kwa undani unagundua upungufu mwingi unaotokana na elimu kuwa ni ndogo pamoja na wahusika kukosa ufahamu mpana wa kitu wanachokifanya, wanakosa exposure.

Nimemuelewa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kumkabidhi wizara ya mambo ya nje Mama Liberata Mulamula, anataka aitumie exposure yake kubwa katika kujenga taswira chanya ya Tanzania kimataifa. Inakuwa ni aibu unapomsikia mbunge anakejeli elimu wakati ndio silaha namba moja ya mataifa yaliyoendelea.

Kejeli anazokutana nazo Prof Muhongo zinawahusu pia maprofesa wengi ambao wamefanya mengi ya maana na yenye kuonekana kwa faida ya taifa. Ni mawazo fulani duni kuiponda elimu eti kwa sababu ya kutofautiana mitazamo na msomi mmoja
Well said my friend!!!!

Kwakweli kitu kinachoendelea kwa Mbunge Msukuma na Lusinde kuhusu Ma-Professor na ma-Doctor sio sahihi, it is very unethical kwa wabunge kama kutoa lugha za dharau kwa wao kama wabunge.

Kinachoonekana ni kama vile wana personal jealous dhidi ya hao wasomi kwa kiasi cha kutumia lugha chafu na matusi dhidi ya hao wasomi. Inaonekana wana lao jambo nyuma ya carpet kitu ambacho sio kizuri kwa ustawi wa bunge lenyewe na Taifa kwa ujumla. Namshauli Spika Ndugai kuwa makini na kauli zinazotolewa na Msukuma na Lusinde la sivyo itaonekana wewe Spika Ndugai ndie unaewatuma kutoa lugha za hovyo hapo bungeni bila staha yoyote.

Cha ajabu alichoongea Prof. Muhongo ni kipi?? Yeye kama msomi alitoa ushauli wake kuhusu project ya Nyerere Hidro Electric Power ambapo Msukuma na Lusinde wngekuja na hoja thabiti za kumpinga Prof. Mungo kitaalamu na sio kuleta lugha za dharau na kihuni kuhusu wasomi wetu. Dr. Kimei kajitahidi kulikemea hilo lakini wewe Spika Ndugai umemu-ignore Dr. Kemei na bapo nachelea kuamini kuwa wewe Spika Ndugai ndie unaewatuma akina Msukuma kuharibu na kuchafua utu wa watu.

Naomba Msukuma na Lusinde wasitumie kutokwenda wao shule iwe ndo defensive mechanism ya kuwachafua wenzao, this is completely hopeless kabisa!!

Ikumbukwe kwamba, watu kama akina Muhongo wametoa mchango mkubwa sana kwa Taifa hili ikiwa ni pamoja na huko duniani kwa fani aliyonayo.

Niwakumbushe tu kuwa nafasi ya Ubungo ni Uongozi!!!. Na Uongozi ni pamoja na nidhamu na kuvumiliana!!

Asante!!!
 
Kama professor kazingua acha aambiwe ukweli mda mwingine wasomi tuliowasomesha kwa kodi zetu hutugeuka Watanzania kwa maslahi yao binafsi huku rasilimali zetu zikiporwa na Mabeberu.
1618489917709.png

Badala ya chadema sasa kambi rasmi ya upinzani bungeni mnawaona ni kina nani??
WASOMI !

Akina Assad
Akina Muhongo
Akina Kichere
Etc
 
Gas ya Mtwara siyo yakwetu bado turudie huu upuuzi tukimaliza umeme wa maji tutaenda kwenye gas tena kwa pesa zetu za ndani.
Ndo walichokueleza na ukaamini... USISAHAU HAO HAO WALIKUELEZA NDEGE ZETU MWAKA 2018 ZILITENGENEZA FAIDA NA WENGINE WAKAMWAGA NA MAGAWIO SERIKALINI...
 
Well said my friend!!!!

Kwakweli kitu kinachoendelea kwa Mbunge Msukuma na Lusinde kuhusu Ma-Professor na ma-Doctor sio sahihi, it is very unethical kwa wabunge kama kutoa lugha za dharau kwa wao kama wabunge.

Kinachoonekana ni kama vile wana personal jealous dhidi ya hao wasomi kwa kiasi cha kutumia lugha chafu na matusi dhidi ya hao wasomi. Inaonekana wana lao jambo nyuma ya carpet kitu ambacho sio kizuri kwa ustawi wa bunge lenyewe na Taifa kwa ujumla. Namshauli Spika Ndugai kuwa makini na kauli zinazotolewa na Msukuma na Lusinde la sivyo itaonekana wewe Spika Ndugai ndie unaewatuma kutoa lugha za hovyo hapo bungeni bila staha yoyote.

Cha ajabu alichoongea Prof. Muhongo ni kipi?? Yeye kama msomi alitoa ushauli wake kuhusu project ya Nyerere Hidro Electric Power ambapo Msukuma na Lusinde wngekuja na hoja thabiti za kumpinga Prof. Mungo kitaalamu na sio kuleta lugha za dharau na kihuni kuhusu wasomi wetu. Dr. Kimei kajitahidi kulikemea hilo lakini wewe Spika Ndugai umemu-ignore Dr. Kemei na bapo nachelea kuamini kuwa wewe Spika Ndugai ndie unaewatuma akina Msukuma kuharibu na kuchafua utu wa watu.

Naomba Msukuma na Lusinde wasitumie kutokwenda wao shule iwe ndo defensive mechanism ya kuwachafua wenzao, this is completely hopeless kabisa!!

Ikumbukwe kwamba, watu kama akina Muhongo wametoa mchango mkubwa sana kwa Taifa hili ikiwa ni pamoja na huko duniani kwa fani aliyonayo.

Niwakumbushe tu kuwa nafasi ya Ubungo ni Uongozi!!!. Na Uongozi ni pamoja na nidhamu na kuvumiliana!!

Asante!!!
1618490586970.png
 
Mheshimiwa Msukuma amepata umaarufu mkubwa siku za karibuni haswa kwa kumkejeli Profesa Muhongo mwenye kuamini kwamba umeme wa gesi ni suluhisho la suala zima la nishati hiyo. Ni mawazo ya Profesa Muhongo na anao uwezo wa kuyatetea kwa hoja kila anaposimama na kuongea bungeni...
Yeye anapoona Kila siku Joni anabeba daftari kwenda kuchukua hesabu za mabasi take anafikiri wote duniani wanafanya Kama yeye
 
Back
Top Bottom