Tukimbilie wapi? Mtetezi wetu CHADEMA amekaa kimya!

Tukimbilie wapi? Mtetezi wetu CHADEMA amekaa kimya!

Huu utegemezi uliopitiliza kwa Chadema sasa ndio umezidi kunifungua macho, tuliwaegemea viongozi wa Chadema kwa kiasi kikubwa sana wawe wasemaji wetu, huku sisi tukibaki nyuma na kuwaacha wao mstari wa mbele.

Matokeo yake tumedumaa, Chadema wakiwa kimya hatujui cha kufanya, na bahati mbaya wakati mwingine hata Chadema wakituambia nini tufanye, bado hatufanyi, tuliwaacha wakazoeleka wazungumzaji wa kila siku kwa press zao.

Muhimu tu tutambue, press bila vitendo ni bure, sasa ni wakati wa kila mmoja wetu kutimiza jukumu lake, kama kweli mnawapenda Chadema wasiachwe peke yao kufanya kila kitu, mabadiliko yanaanzia hapo ulipo.
 
Mkuu kuwa neutral tu kama mimi.

Wenzako wako field wewe unataka matamko ili upate cha kuandika huku mitandaoni.

Yani ni kama Chadema wanafurahi sisi wananchi tunavyopata shida ya hayo yote uliyoyataja maana shida zetu zinawasaidia wao kujijenga.

Hivi mwenye tatizo ni Nani? CCM ama chadema?
 
Bro kuwa makini na propaganda,CCM Wanajitahidi sana siku hizi kuonesha kuwa CHADEMA imekaa kimya kwasababu wanafaidi urais wa Samia.
Sasa ni wakati wa kudai katiba mpya kwa nguvu zote ili asije kichaa mwingine akavuruga sheria kama jiwe.
Kutokuoanda mishahara ni matokeo ya udikteta wa jiwe kwa kutokufuata sheria ya ongezeko la mshahara na kuamua kadri ya anavyoona.
Tuache CHADEMA ipambanie mambo makubwa kama KATIBA MPYA na MARIDHIANO YA KITAIFA.
Mambo ya wafanyakazi viachiwe vyama vyao sasa vifanye kazi yake na wafanyakazi wenyewe waamue kuamka.
 
" Funga mdomo , lamba asali "

Asilisikika akisema , Baada ya bwana yule kuondoka
 
Bado nina Imani kubwa na Chadema. Toa neno Mh. Mbowe katika hizi vurugu za "kudanganywa "mishahara, Kingai (mbambikaji wa kesi kupanda cheo) and many other hot issues!
Nendeni Chaltle Kaburini,..
 
Bro kuwa makini na propaganda,CCM Wanajitahidi sana siku hizi kuonesha kuwa CHADEMA imekaa kimya kwasababu wanafaidi urais wa Samia.
Sasa ni wakati wa kudai katiba mpya kwa nguvu zote ili asije kichaa mwingine akavuruga sheria kama jiwe.
Kutokuoanda mishahara ni matokeo ya udikteta wa jiwe kwa kutokufuata sheria ya ongezeko la mshahara na kuamua kadri ya anavyoona.
Tuache CHADEMA ipambanie mambo makubwa kama KATIBA MPYA na MARIDHIANO YA KITAIFA.
Mambo ya wafanyakazi viachiwe vyama vyao sasa vifanye kazi yake na wafanyakazi wenyewe waamue kuamka.
Unaacha kupambania mambo unayoyaona ya msingi ya kitaifa badala yake unapeleka nguvu Kuwapambania ambao mishahara ingeongezwa pengine kwa hata laki tu, ingekuwa hongo ya kutosha kuwanyamazisha kwenye yale ya msingi. Unafuu wa muda kwa watumishi wasofika milioni, au haki, utawala bora, maendeleo kwa wote na actual progress ya society, chaguo ni rahisi mbona?
 
Bado nina Imani kubwa na Chadema. Toa neno Mh. Mbowe katika hizi vurugu za "kudanganywa "mishahara, Kingai (mbambikaji wa kesi kupanda cheo) and many other hot issues!
Ustaarabu ni kutoongea Wakati wa kulamba asali kaka
 
Back
Top Bottom