Bado nina Imani kubwa na Chadema. Toa neno Mh. Mbowe katika hizi vurugu za "kudanganywa "mishahara, Kingai (mbambikaji wa kesi kupanda cheo) and many other hot issues!
Mkuu 'Retired', umeuliza swali muhimu kweli kweli ambalo linahitaji mjadala wa maana sana kupata jibu/majibu yanayoeleweka.
Mimi nitachangia hapa kwa kuwa upande wa 'devil's advocate', kuwateyea CHADEMA; lakini kiuhalisia hapo baadae nitageuka na kuonyesha kukosa ukomavu upande wao.
CHADEMA na viongozi wake wote wamepitia katika hali ngumu sana katika miaka hii ya karibuni iliyopita. Wamefanya kila juhudi kutetea maslahi ya wananchi huku mapigo yakielekezwa kwao.
Badala ya wananchi (nina maana ya umma wa waTanzania) kuunga juhudi hizo na kuleta mabadiliko, ikawa kama CHADEMA na viongozi wao ndio wanaojitafutia maumivu bila ya sababu. Ni kama juhudi za CHADEMA zilipuuzwa na wananchi wengi. Au hawakuona maana ya kazi iliyokuwa ikifanywa na CHADEMA kwa niaba ya wananchi.
Viongozi wanapigwa risasi, wananchi kwa wingi wao kimya!
Viongozi wanawekwa ndani hovyohovyo tu, wananchi wanapuuza, hawanyooshi hata kidole!
Hebu niambie ukweli wako, ingekuwa ni wewe usingejiuliza maswali juu ya mambo kama haya? Mtu unajitoa juu maslahi ya watu wasiotambua maana ya kujitoa kwako, huwezi hata ukastuka kuna nini?
Hapa nimetiririka tu, kama kuna mahali hapakunyooka vizuri, tafadhari naomba uelewe maana yangu kuu.
Viongozi wanazushiwa kesi za ugaidi, wananchi wanacheka tu