Tukinunua umeme wa TANESCO units ziende automatically kwenye mita ya kisasa. Tuachane na habari za kuingiza TOKEN. Is this feasible and implementable?

Naunga mkono hoja unakuta umeme umeisha halafu umenunua umeme kwenye simu unapewa minamba uingize na mita haina chaji unaenda kupiga hodi kwa jirani ili uingize umeme .....ni kero tupu ......


Naomba tanesco wafikirie wazo lako

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi hawajaja tu kujibu? Ngoja niwaite TANESCO TANESCO manaake kweli ni shida sisi hapa kwetu nyumba ya kupanga mita iliharibika kitambo hawaleti mita mpya eti mpaka tujichange tununue umeme mwingi wanakuja na kimita chao wanatuwekea umeme hao wanasepa nacho. Yani usumbufu toka mwezi wa kwanza.

Inakua kama tupo karne ya 17 bwana.

Njooni huku TANESCO
 
Bora wa kwako unaingia kwa jirani. Sisi imeharibika token haziingii kabisa na hawataki kuleta mpya eti zimeisha. Tunawapigia simu wanakuja pengine baada ya siku3 wanatuwekea umeme eti ukiisha tupige simu tena waje na kimita chao. Wanakera sana yani umeme inakua kama vile fadhila wakati mi huduma/biashara

Mkuje huku nyie bwana umeme TANESCO TANESCO
 
Hizi meter zipo,mimi nina kadi za hizi meter nilikuwa natumia nchi fulani huko duniani zipo kama zile za bank just unaandika ka bei ka umeme unachanja umeme unawaka,je Tanzania tutaweza kuendesha hizi meter maana tutahitaji internet...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
LISHAANZA MITA ZA SASA ZIKO HVYO MKUUU WASILIANA NAO..
 
Excellently thought out! Tanesco walifanyie kazi hili hakuna haja ya kuanza kubofya bofya rimote au kwenye mita mradi token zimetoka umeme uingie moja kwa moja kwenye mita
 
Kijana akili zako ziko mbele sana kuliko hata uwezo wa maphd na maprofesa hakuna aliyewahi kuwaza hivyo. Ina bidi upewe nishani ya mawazo murua na uingizwe kwenye kitengo cha IT cha Tanesco. Hebu copy na kupest huu uzi kwenye kwenye special thread ya Tanesco walifanyie kazi
 
Mchakato wa kuingiza umeme automatically kama unavyohitaji si rahisi kama unavyofikiria maana zipo variables kibao zinazohusika hadi pale units zinapoingia ktk mita yako. Hivi unaponunua airtime token kwa ajili ya simu yako, zile credits ulizonunua je uingia moja kwa mmoja ktk simu yako bila kuzi punch in physically?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi zipo
Feasible and implementable. Lakini tunasubiri mpaka huko duniani watengeneze watuleteee
na zinafanya kazi, ila itabidi za ss zingólewe ziwekwe mpya. So wkianza wataanza na wateja wapya nyie wengine muendelee kusubiria mpaka ije phaseout.
 
Good idea. Lakini ukumbuke, awamu hii, hapangiwi cha kufanya. Labda tuligeuze liwe wazo lake na fasta tuanze mapambio ya kumsifu.
 
Poleni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi mita za tanesco hazina CARD.. meaning zingekuwa zimekuwa linked ktk system na kuwa ktk network ingekuwa nzuri sana.. Yaani meter hz labda wabadili zooooooote ndio walete mpya, hapo idea yako itafanya kazi..!! Na hilo it will take years..!! Labda wateja wapya waanze na meter mpya of which ni ghali kidogo..!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…